Yanga FC yaingia mkataba mpya na SportsPesa wa miaka 3 wenye thamani ya Tsh Bilioni 12

Yanga FC yaingia mkataba mpya na SportsPesa wa miaka 3 wenye thamani ya Tsh Bilioni 12

Sasa kwa akili ndogo uliyonayo, kwa nini unadhani mdhamini hastahili kuweka fedha ndefu kuliko mwekezaji? Unadhani kwa nini Simba walikataa udhamini wa GSM kwenye ligi ya Bara pale alipoweka sh. 2B (bilioni mbili tu) kwa timu 16?
kwani mdhamini sportpesa amedhamini ligi??? mo mwekezaji hizo bil 20 anawekeza kila mwaka au ndo kashanunua timu??? mbet wameweka sh ngapi??? mbona mkataba haujasema au ndo akijua MO inatosha
 
Yanga leo inakwenda kuweka historia nyingene, Futilia live hapa

Ni mKataba wenye thamani ya tshs bilioni 12 na Milioni 300 kwa miaka 3, Kila Mwaka Yanga itakuwa inapata bilioni nne, pia yanga akichukuwa ligi milioni 150, na ikifika Fainali FA itapata Tshs Milioni 75.

---

Mabingwa wa kihistoria na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Dar Young Africans (Yanga) leo wamesaini mkataba mpya wa udhamini na kampuni ya michezo ya kubashiri ya Sport Pesa mkataba ambao unaweza kuwa wenye thamani zaidi kwa timu za Ligi Kuu nchini Tanzania.

Mkataba huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 12.335 wa miaka mitatu unaifanya SportPesa kuwa mdhamini mkuu wa Yanga kuanzia msimu mpya unaoanza wa Ligi.

Katika mkataba mpya kwa Mwaka Yanga watachota zaidi ya Shilingi Bilioni 4 tofauti na mkataba uliopita ambapo Yanga walikuwa wanapata Bilioni 1 pekee kwa Mwaka, hii ina maana hili ni ongezeko la zaidi ya Bilioni 3 kwa mwaka.

Maboresho mengine katika mkataba huo ni kuwa "Bonus" ya Ubingwa wa Ligi Kuu imeongezeka kutoka Milioni 100 hadi 150.

Huku Bonus ya kombe la FA ambayo haikuwepo hapo awai ikiongezwa ambapo Yanga watapata Milioni 75 kwa kufika hatua ya Fainali.
Wapi Manara hapo au keishapew barua? Ahahahahah!
 
Tofauti ya Bilioni 4 kwa mwaka na Billion 1.5 kwa michezo ya loosser tu...akitolewa ndo mwisho wa mfereji...
Apo mmechemka
 
Mmhh mbona hakukuwa na bonus za mashundano ya kimataifa?
 
Back
Top Bottom