OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Yanga wamezoea kuishi kwa propaganda kudanganya mashabiki. Kibaya zaidi nao hawana hata akili ya kushtuka. Walidanganywa sana kuhusu Chama, wakadanganywa kuhusu ubingwa VPL na FA. Leo hii bado wananogewa kudanganywa.
Japo Simba haijaweka wazi, lakini ni kwamba, Miquissone ameuzwa kwa Al Ahly kwa Dola 1,000,000 ambazo ni zaidi ya Sh2.3 bilioni na atakuwa akipokea mshahara wa Dola 34,000 kwa mwezi sawa na Sh80 milioni - pesa ambazo kwa msimu uliopita zingeweza kulipa mishahara ya kikosi chote cha Simba.
Nje ya mkwanja huo, pia imeelezwa Miquissone atakuwa anapewa Dola 20,000 (sawa na Sh46.3 milioni) kama bonasi ya kufanya manunuzi yeye na familia yake. Hapo bado hayajatajwa marupurupu mengine atakayoyapata akiwa ndani ya Al Ahly.
Sasa jiulize Yanga wanaweza kuvunja huo mkataba? Labda wauze figo za mashabiki, viongozi na wachezaji ndio wapate hela ya kuvunja mkataba