Yanga ichukuliwe hatua kwa uharibifu iliyofanya juzi uwanja wa Mkapa

Yanga ichukuliwe hatua kwa uharibifu iliyofanya juzi uwanja wa Mkapa

Weka hapa, ila hao wanarukaruka juu ya viti nazani umewaona ni mashabiki wa 5imba ......... au nao wanasingiziwa. Maana mechi haiwahusu za kwenu mnasusa,basi tizameni burudani mshangilie kiustaraabu mnaruka juu ya viti,plus mafataki.Then lawama wanatupiwa Yanga.

Ila wabongo waharibifu sana ustaarabu zero sio poa kung'oa viti bado wanapanda juu ya viti kushangilia
Bungeni kwenyewe wakishangilia wanagonga meza. Hapa tunaongelea kuleta vurugu kwa kurusha viti kwa mashabiki wengine.

Hiyo clip haionyeshi mshabiki hata mmoja wa Al Ahly akirusha kiti, wote wako kwenye vibe la kushangilia tu hawana shida na mtu.
 
Juzi katika mechi ya Yanga vs Al Ahly uwanja wa Mkapa, mashabiki wa Yanga waling'oa viti na kuwarushia mashabiki waliokuwa wanaishangilia Al Ahly. Inteligensia yangu imeniambia kuwa mashabiki wa Yanga walifanya hivyo baada ya kuudhiwa na kitendo cha mashabiki wa Al Ahly kuwasha moshi uliosambaa upande walilokuwa.

Nakumbuka mwishoni mwa msimu uliopita, Yanga walifanya gwaride na kwa wingi wao walipita mtaa wa Msimbazi ili kuikebehi Simba na wakawasha fataki na moshi. Wengine walidai ule ni utani wa jadi ila tunasahau busara huwa inatumika hata viwanjani kuwatenganisha mashabiki wa pande mbili pamoja kwamba huo utani wa jadi upo.

Nakumbuka baada ya gwaride la Yanga niliwahi kusema, siku mashabiki wa Simba wakisherehekea kwa kupita makao makuu ya Yanga na kufanya kile kile walichofanya Yanga, mashabiki wa Yanga watawafanyia vurugu. Leo maneno yangu yanathibitisha kuwa hilo litakuja kutokea.

Tukio walilofanya mashabiki wa Yanga kupita na kuwasha moshi mtaa wa Msimbazi lingeweza kuleta maafa makubwa sana, tushukuru tu ustaarabu ulioonyeshwa na mashabiki wa Simba. Kama maafa yangetokea, wa kulaumiwa wangekuwa ni vyombo vya ulinzi na usalama vilivyoruhusu jambo lile kufanyika.

Kitendo walichofanya Yanga kimelitia dosari taifa. Tunategemea Mwenyekiti wa chama cha vilabu Afrika ambaye uzuri alikuwepo uwanjani, atoke hadharani aikemee klabu ya Yanga kwa kitendo hicho na pia TFF waipigishe faini klabu ya Yanga na kupewa onyo kali.
Wenye akili ni wawili tu
 
Bungeni kwenyewe wakishangilia wanagonga meza. Hapa tunaongelea kuleta vurugu kwa kurusha viti kwa mashabiki wengine.

Hiyo clip haionyeshi mshabiki hata mmoja wa Al Ahly akirusha kiti, wote wako kwenye vibe la kushangilia tu hawana shida na mtu.
Na wanasimama juu ya viti huko bungeni?Halafu wanapigaga na mafataki huko bungeni?

Naona wapo na mashabiki wengi wa Al Ahly wa mkopo,waliokula tano wazee wa kususia mechi zao.

Umeambiwa uweke hiyo video ya mashabiki wa Yanga unazunguka zunguka.
 
Yanga haijawahi kuwa na tabia za kishamba kama hizi,hawa 5imba wanafosi Yanga ionekane mbovu au ifanye vibaya ili tu wapate pa kupumulia,Yanga tuliisapoti timu yetu wakati inatembeza bakuli na si kuisusa hawa wajinga 5imba wataweza!
Na mlikuwa mnaenda airport kupokea wageni kweli yanga wana roho nzuri sana.
 
Na wanasimama juu ya viti huko bungeni?Halafu wanapigaga na mafataki huko bungeni?

Wapo na mashabiki wengi wa Al Ahly wa mkopo,waliokula tano wazee wa kususia mechi zao.
Umesoma mada lakini au umekurupuka tu? Mlitoka huko mabondeni mkaenda hadi mbele ya makao makuu ya Simba mkafanya hivyo hivyo, kama haukuwa uchochezi ule ni nini halafu leo mmegeuka polisi wa CAF kuzuia watu kuwasha moshi viwanjani kwa vibe lao?

Halafu hiyo hukumu unayowapa ya kuwasha fataki viwanjani inawahusu nyie pia, unadhani tumesahau?Inanikumbusha maneno ya mtu mmoja aliwahi kusema mswahili kwa chuki zake yuko tayari naye akose zaidi ili mradi asiyempenda akose.
 
Manara amewakamata vibaya sana mnaamini kila kitu anachosema manara yule jamaa ni mchonganishi wa hatari na anajua tu atawakamata.

Tangia yanga warudi kimataifa wamekuwa walifanya Mambo ya aibu Sana, inaonyesha hii timu ilizoea mechi za ndondo
Dunia ilikuwa bora zaidi walipokuwa wanaishia hatua za awali. Nilisema kabla ya mechi na Al Ahly, hawa viumbe wako na msongo mkubwa wa mawazo, nikasema baada ya mechi watakuwa kwenye hali mbaya. Weekend inayokuja tutajionea mengi zaidi na utaona uhuni watakaowafanyia Medeama watakapokuja.
 
Umesoma mada lakini au umekurupuka tu? Mlitoka huko mabondeni mkaenda hadi mbele ya makao makuu ya Simba mkafanya hivyo hivyo, kama haukuwa uchochezi ule ni nini halafu leo mmegeuka CAF Police kuzuia watu kuwasha moshi viwanjani kwa vibe lao?

Halafu hiyo hukumu unayowapa ya kuwasha fataki viwanjani inawahusu nyie pia, unadhani tumesahau?Inanikumbusha maneno ya mtu mmoja aliwahi kusema mswahili kwa chuki zake yuko tayari naye akose zaidi ili mradi asiyempenda akose.
Nimekurupuka mimi au wewe ulivyo kuwa kiazi,mimi nimecomment kutokana na clip ile iliyopostiwa ambayo inaonyesha reality. .

Lini tumeenda mbele ya makao makuu yenu? Yaani tuache kupita barabara ya serikali,kisa kuna makao makuu ya 5imba.

Haya tumepita karibu na makao makuu,umeona sehemu tumeharibu kitu chochote cha serikali?

Sasa adhabu anapewa Yanga au hao waarabu na fataki zilianza kiwasha baada ya Al Ahly kupata goli.

Yaani fujo wafanye waarabu na wazee watano haafu adhabu apewe Yanga.Yaani mnapenda kujifariji kwa matukio ya Yanga.

Sisi tunawakaribisha kwenye mechi zetu,ila msifanye fujo kama fujo mkafanye kwenye timu yenu. Au unafikiri tumesahau mlivyo ng'oaga viti NBC huku, tatizo timu lenu halina ustaarabu kuanzi mashabiki mpaka wachezaji walio choma nyasi za Wasouth kwa kuota moto.Mshazea kuharibu vitu vya watu.
 
Huyo aliepiga teke kiti hadi kung'oka ni shabiki wa Yanga?
Kwanza ungejitahidi kujua mtiririko wa matukio, hao walishambuliwa kwa viti na vitu vingine na ili kujihami ndiyo nao wakarusha viti. Waarabu wanakuja kila siku hapo kwa Mkapa, umewahi kuwaona wakifanya fujo? Mashabiki wa Wydad si waliwasha hizo fataki, uliona mashabiki wa Simba wakiwafanyia vurugu?
 
Back
Top Bottom