Yanga ichukuliwe hatua kwa uharibifu iliyofanya juzi uwanja wa Mkapa

Ndugu kwa akili ya kawaida tu mpaka hao walioko chini kugeukia kuangalia juu sababu ilikua ni nini? Usianze tu kusema nani kaanza kurusha kwakua video yako ndio imeanzia hapo. Inaonyesha ugomvi ulitokea juu na sio rahisi wa chini kuanzisha ugomvi kutokana na hayo mazingira yalivyo.

Ushabiki usiwatie upofu tumieni bongo zenu vizuri
 
Unazungumza mambo ya kufikirika wakati uhalisia unauona. Halafu wakati huo huo unasema "Ushabiki usiwatie upofu"
 
UWANJA SI UMEFANYIWA MAREKEBISHO?? SI UNA CAMERA WAKAMATWE WAFUNGWE MIAKA 2 , 2 THN UTAONA KAMA KUNA MLEVI ATASUBUTU KUNG'OA KITI.
 
hao sio washabiki wa yanga
 
Kibonde wa mkiani uto
5imba mnajifariji kwa matokeo ya Yanga,mnazani ndio changamoto zenu za kula tano na kudroo mechi tatu mfululizo zitamalizika.

Yaani mpaka mnasusia mechi, mtazani mmelazimishwa kuwa mashabiki wa 5imba.

Maana juzi mmetoka 5000 mpaka 3000,ila hamkujaza hata robo ya uwanja. Mechi ijayo na Wydad ukiwa na MoXtra na kipande cha sabuni unaingia uwanjani,maana hata nyinyi mshaichoka timu yenu.
 
UWANJA SI UMEFANYIWA MAREKEBISHO?? SI UNA CAMERA WAKAMATWE WAFUNGWE MIAKA 2 , 2 THN UTAONA KAMA KUNA MLEVI ATASUBUTU KUNG'OA KITI.
Kibongobongo kufungia mshabiki binafsi si uamuzi unaoweza kutekelezeka. Dawa ni kuilima faini klabu husika. Hata CAF huwa wanatoza faini klabu kwa vitendo vya mashabiki wake na hawadili na mshabiki mmoja mmoja
 
Umekazania habari za kususia timu, Simba ina mashabiki wanaojitambua na ni kawaida kwa taasisi yoyote iliyo imara watu kutofautiana na wengine kuonyesha misimamo yao waziwazi. Hata mambele huko watu wanagoma kushinikiza mabadiliko. Hakuna jambo la kushangaza hapo.

Halafu haikusumbui kuandika "5imba" kila wakati? Hivi unadhani ukiandika hivyo kuna mtu anaumia?
 
Sasa kwani uwongo hamjasusa, hapo kwenye "5imba" simu yangu ikifikia hilo neno "s" hai-respond.

Taasisi imara huwaga haisusi bali washikadau wote hushikamana na kuwa pamoja, kinyume chake taasisi yenu sio imara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…