Yanga imejipeleka Al Hilal; itapigwa kama ngoma

Yanga imejipeleka Al Hilal; itapigwa kama ngoma

Watani wanaweza kutoboa wana hitaji tu mipango mizuri. Wapinzani wana historia nzuri ila ndio wanajenga team mwaka huu. Wana wachezaji na kocha mzuri ila sio team tishio sana.
 
Hawa ndio wafalme wa Soka la Sudan, Ndio klabu iliyobeba mataji mengi zaidi nchini humo na Ndio Wawakilishi Bora zaidi wa CECAFA kwenye CAF.

Hilal imeshacheza Fainali za CAF mara 2 zote Ilipoteza, Ilikua 1987 Kwa Ahly ya Misri na 1992 Kwa Wydad Casablanca ya Morocco.

Imecheza nusu Fainali ya michuano ya CAF mara nyingi zaidi ya klabu yoyote ya CECAFA, ikifanya hivyo mara 5, Robo Fainali nyingi.

Makundi 'Business as usual' Mara mwisho Msimu Jana, 2021/22, Hilal Kwa Sasa Wana nguvu ya Kiuchimi. Kwanini ?

Wana kikosi kinachokaririwa kua na thamani ya Dola za marekani $ Million 2.75 zaidi ya Tsh Bilioni 6.3.

Baada ya Misimu kadhaa kutofanya makubwa kimataifa, Hilal Walimuomba Tycoon, Bilionea Turk El Sheikh wa Saudia Arabia kua raisi wa heshima wa klabu hiyo.

Huyu Mwamba ndiye aliyeinunua Pyramid FC ya Misri kutoka Al Assiyout kitaka kuifanya klabu hatari zaidi Misri na Afrika, Baadae akaiuza.

Mwamba huyu anayemiliki klabu ya Almeria ya Hispania aliweka mzigo Kwa kuongeza nyota wenye uwezo ili Hilal ifanye vizuri zaidi Afrika.

Aliingia Msimu uliopita ila Msimu huu akaweka Mkwanja, Ambao Umenunua Nyota wengi kama Issa Fofana kutoka San Pedro ya Ivory Coast, Cloud Singone kutoka Asec Mimosas ya Ivory Coast pia.

Imoro Ibrahim kutoka Asante Kotoko ya Ghana, John Mano(aliwafunga Simba, Kirafiki), Makabi Lilepo kutoka DRC, Lamine Diedhou kutoka Senegal.

Wakarudisha mtambo wao wa mabao Waleed Bkhet aliyekua Kuwait akitoke Hilal na amerejea tena.

Kama haitoshi Kocha mwenye taji la Shirikisho Afrika Msimu Jana Frolent Ibenge wa DRC. Mpango wao ni Operation Semi Finals, Next destination is Jangwani.
Nahisi hawa nao mechi zao zote watacheza kwa Mkapa
 
Haya maneno ya kudharau timu zetu hayakuanza leo, hata simba alipoingia robo fainali alipoifunga As vita, kila neno la kujidharau lilikua limeshazungumzwa.
 
Back
Top Bottom