Wazo zuri sana, it is said, to get to the top is easier than to stay at the top. Hivyo Yanga ijitafakari, mwenendo ni wa kusuasua, kikosi ni kipana wengine pia kina Shehani, Baleke, Nondo, Gift, Kibwana, Kibababage na Mkude pia wacheze maana hawajulikani sana uchezaji wao na hawatakamiwa. Kuchezesha wachezaji wale wale kila siku nao ni binadamu wanachoka na pia wanajisahau, kugombea namba husaidia kuboost morale!!
But ni vizuri pia kuona timu zikiikamia sana Yanga maana zinaiimarisha na kuwa timu ngumu zaidi kuifunga. Dawa ni Yanga kuvifunga kibabe hivi vitimu na kuwa imara kama chuma sababu makombe yote mali ya Yanga.
Huu ni wakati Yanga itangaze kwa wachezaji kuwa kila mechi mbele yao ni fainali na kombe liko uwanjani.
Mkakati wa kuchukua points 6 za Simba uanze sasa muda huu now now maana Azam si competitor tena hajiwezi. Points 6 za Simba ndo zimebeba ubingwa wetu wa nne maana Simba kila mechi inabebwa.