Yanga imepata wachezaji imepoteza team

Yanga kacheza mechi ngapi hadi sasa?

Wachezaji wa Yanga ukiacha mechi za klabu yao, ni wangapi waliopo 1st 11 na wametumiwa na timu zao za taifa?

Kumekuwa na muda wa miili kurecover?

Hao KMC wamecheza mechi ngapi hadi sasa?

Wachezaji wangapi wa KMC waliotumikia timu zao za taifa?
 
Kuhusu boka ni Mchezaji mzuri kwenye mikimbio kutoka eneo la chini kwenda eneo la juu ila mipira yake mingi haina usahihi, anaweza kupiga cross 6 ikafika moja zingine zinatoka nje, zinakuwa blocked na mabeki au ziende kwa kipa, bado hana pass accuracy.

Kuhusu viungo vya juu kwa sasa wamekosa ubunifu, tukimtoa pacome the rest wanategemea kutumia mbinu ya mwalimu kwa asilimia 98 ili kuleta production kwenye timu ila pacome na max huwa wanajaribu kufanya vitu binafsi nje ya mfumo wa mwalimu kitu ambacho huwafanya waonekane ni wachezaji wenye umuhimu mkubwa na hatari zaidi kwenye timu.

Ila kingine ninachokiona kwa yanga uwepo wa mastar wengi wenye uwezo mkubwa kunamchanganya Mwalim hajui aanze na nan na nan ili apate kitu kilichobora kitu ambacho kinampelekea kila siku kurotate kikosi akitafuta 11 bora.

Hadi sasa Yanga haina first 11 inayotambulika.
 
Kwa hiyo tatizo ni timu za taifa?

Ova
 
Sisi tuliwaambia CBE sio kipimo

Sasa mmejionea wenyewe yani mmekuja kusumbuliwa na timu zile ambazo hazijawahi kushinda mechi yeyote.

Yani kwa haraka haraka tunaweza kusema CBE sio level ya Ken Gold wala KMC.
 
Utetezi huu si bora hata autumie shabiki wa Simba.

Yanga ilikuwa na ratiba ambayo ni too fair kuanzia ugumu wa mechi na kipindi cha mapunziko.

Simba imecheza mechi ngumu za CAF imepumzika siku 3 na kurudi tena NBC dhidi ya mechi nyingine ngumu na Azam.

Imetoka hapo imeshinda siku 1 tu Dar siku ya oili yake imesafiri kwenda mkoani na kesho yake ambayo ndio jana ndio mechi yenyewe.

Wakati huo Yanga anacheza na Ken Gold alikuwa na siku 4 za mapumziko ili kujiandaa na mechi ya jana

Tofauti na Simba ambaye alikuwa anasiku 2 za kujiandaa licha ya kutoka kucheza mechi ngumu.
 
kweli mkuu ndio maana marefa wanakuja na matokeo yao
 
bahasha kama za marefa wa mechi mbili zilizo pita za nyau
 
Kwa taarifa yako, Boka jana ndiye kachukua mchezaji bora wa mechi! Yaani Profesa leo aje afundishwe na mtu wa ngumbaru kwenye kupanga timu? Ajabu la karne hili!
 
Sahihi...
๐Ÿ’ฏ๐Ÿ’ฏ๐Ÿ’ฏ
 
Kwamba simba yako inayomilikiwa na tajiri zaidi afrika mashariki walihongwa kile kipigo cha 5? Halafu kwa akili hizi ndio munajiita wasomi๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
 
Kwamba simba yako inayomilikiwa na tajiri zaidi afrika mashariki walihongwa kile kipigo cha 5? Halafu kwa akili hizi ndio munajiita wasomi๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
Walihongwa kina Manura, Chama, Baleke, Inonga & company.

Hukuona hao niliowataja baada ya mechi wakawa wanashangilia na wenzao Yanga huku kina Hussein na Kapombe wakilia kwa uchungu wenzao kuwasaliti.

Chama hadi alisimamishwa na uongozi baada ya mechi ile. Unadhani uongozi wa Simba ni wajinga hadi kuwatuhumu baadhi ya wachezaji?
 
Kwamba simba yako inayomilikiwa na tajiri zaidi afrika mashariki walihongwa kile kipigo cha 5? Halafu kwa akili hizi ndio munajiita wasomi๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†
Simba hata mbovu kiasi gani hawezi kufungwa na Gongowazi hata goli 3 achilia mbali 5.

Simba amekuwa mbovu takribani misimu mitatu nyuma lakini hakuna mechi aliyofungwa 3 hadi bahasha ya kueleweka ilipotembea kwa baadhi ya wachezaji wenye tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ