Yanga ina tatizo la kocha, wachezaji au viongozi?

Wote. Ila kwa mechi ya Tanga, Coastal Union walituzidi kwenye commitment na team work. Yanga timu iligawanyika vipande vitatu. Footwork ya wachezaji wa coastal ilikuwa superb. Kocha wetu kila mechi yeye anajaribu jaribu tu. Sioni kama tutatoboa this season.
 
Mindset za viongoz wetu mkuu n tatizo hawawez kutuvusha.

Msola + mwakalebela never ever hatuwezi toboa.
 
Mpira wa Bongo ukiacha umuhimu wa pesa,kocha mzuri na wachezaji wazuri, kuna swala la fitna.

Siku ukiona Simba kwenye msimamo wa ligi hana dalili ya kubeba ubingwa, kaachwa kwa points nyingi,na mwenye nafasi ya kuchukua ubingwa ni Yanga au Mbeya City.

Alafu mechi ya mwisho iwe Simba na Mbeya City na Mbeya City akishinda anabeba ubingwa, basi Simba watafungwa magoli 10-0 na Thadeo Lwanga akiwemo, Pascal Wawa, Chama akiwemo, yani full mkoko.

Amini nakwambia my frend kuboronga kwa Yanga ni mkono wa Al Ahly ya East Africa.
 
Yanga hawana tatzo lolote.wapewe muda.80% timu ni mpya tukumbuke.

Pili yanga ni nani hata asifungwe.pia malawama yamekuwa mengi mno. Tena mengne hayana msingi eti timu inapata ushindi mwembamba.

Ushauri tu, viongozi wa yanga wasiwe driven na malawama yasiyo na msingi na mihemuko ya washabiki. Kule uingereza mikel arteta anavurunda kila siku, timu ipo nafasi ya 10..mashabk pamoja na kulalamika lakn uongozi haupangiwi cha kufanya.

Yanga wawe wavumilivu.wapo vizuri.zipo timu nyingi tu duniani kwasasa hazifanyi vizuri.ila mashabiki wao wamebaki watulivu.

Liverpool, Gor Mahia, TP mazembe, Kaizer Chiefs, Man U, Dortmund, Barcelona ni mifano tu ya vigogo wanaosuasua kwny ligi zao. Mbona zahera aliachwa huru.
 
Viongozi wa yanga wana wadharau na kuwachukukia poa sana mashabiki wa yanga wana waburuza wanavyo taka wana waongopea wanavyo taka

Zaidi ya yote na wao wanaenda enda tuu kama mazombi

Me nadhani tatizo namba moja la yanga ni mashabiki wao

Kwa mechi ya Coast Union wote tuneona football imechezwa lakini kama kiongozi wa yanga akatoka na kusema tulionewa basi mashabiki na waao wataenda humo humo bira kutafakari

Kitu amabcho kwa simba sc ni tofauti sana timu yao inapo fanya vibaya mtuhumiwa wakwanza ni mchezani na kocha mapungufu ya marefa ni mara chache zana kukuta simba waki ya lalamikia
 
Yanga hawana tatzo lolote.wapewe muda.80% timu ni mpya tukumbuke...
Huwezi kufananisha management za timu kama Arsenal na Yanga bro ni mbingu nabardhi

alaf kingingine yanga hakuna mchezaji alie wahi kukaa zaidi ya misimu mi3 hivyo kusema eti kikosi kipya haina mashiko kwasababu am sure msimu ujao lazina kuna wachezaji zaidi ya wa5 wataondoka zao kwahyo wata rudi kule kule ?

Kwahyo cicle itakua ile ile
 
Tatzo ni washabiki wao. Hawana msimamo, wanadance na kauli za viongozi na kocha. Timu ikifungwa wanailaumu simba, tff, serekali n.k na wao wanaingia kwenye mkumbo huohuo. Wasingeukubali huo upuuzi tokea muda lazma viongozi wangekuja na mkakati makini
 
Tatizo la yanga ni mashabiki wao.Wengi hawana akili vizuri na wanawapa kichwa sana wachezaji. Wanawasifu wachezaji kama vile mastaa wa viwango vya dunia.

Kwa hiyo kisaikolojia hata wachezaji wasipojituma, inajulikana lawama ni kwa TFF,bodi ya ligi,waamuzi,Simba wanatia mkono wao(sijui hata wanatiaje), na serikali.

Sasa kibaya zaidi ni wale wachambuzi waliojaa kwenye media.Hawa ni mashabiki wakubwa wa utopolo na huwa hawawaambii ukweli.Na haya matokeo ya yanga,hutaona yanajadiliwa sana zaidi ya historia sijui mtu alizikwa baharini akasahailika. Sijui makomandoo wa coastal, na ujinga mwingine kama huo tunaouona nje ya uwanja kama ulivyo kwenye ndondo cup.

Unategemea kuna mabadiliko ya kiufundi yatafanyika kweli ndani ya uwanja?
 
Mpira wa Bongo ukiacha umuhimu wa pesa,kocha mzuri na wachezaji wazuri, kuna swala la fitna...
Inawezekana pia lakini siyo sababu ya msingi. Yanga Ina matatizo kwa pande zote kuanzia kwa kocha, wachezaji, uongozi pia, na sisi Wapenzi na washabiki

1. Kocha
Toka kupumzika kwa kocha Mwambusi benchi la ufundi limekuwa likishindwa kuusoma mchezo husika na kupanga kikosi mahususi. Hata ikiwa tayari imeonyeaha kuelemewa, kocha na bench zima wamekuwa si wepesi wa kusoma na kutambua tatizo ili kufanya sub ya maana kwa wakati. Refer mechi dhidi ya Mbeya city, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar hata hile ya kirafiki dhidi ya African sports madhaifu ni yake Yale kwa upande wa benchi la ufundi. Kiufundi naliona bench Hili la ufundi likizidiwa kwa mbali na like la papa Zahera Mwinyi.

2. Wachezaji
Kiukweli katika vitu ambavyo vimaiangusha timu Ni haina ya wachezaji tuliokuwa nao Sasa. Yaana ubinifu zero. Ukimtoa Mkoko na Tuisila Hawa wengine walioletwa na Eng. Hersi hawafai hata kuchezea Mbao fc. Lazima tufike mahalo tuambiane ukweli wale tumeletewa Mizigo tu, Ni Mara Mia tungesajili wachezaji wa ndani tu kuliko hii Mizigo. Hebu tumlinganishe Sarpong na Yusuf Mhiru, muangalie huyu Eric Msagati, Kuna huyu mchezaji yuko Gwambina anaitwa Meshaki Abeli na wengine wengi wanawazidi kwa mbali Sana Hawa tunaoaminishwa kuwa Ni mapro. Kiufupi Hawa kina Sarpong nawafananisha na watumishi hewa. Ni kheri tungebaki na Moringa David kuliko Hawa walioletwa kwa mbwebwe.

3. Viongozi Mikakati ya mafanikio ni Zero
Hawa Ni tatizo kubwa, kwa kiasi kikubwa Hawa wamefeli kabisa. Wanakosa Mission na Vision. Hadi Sasa nashindwa kuelewa Ni Yanga ya aina gani wanayoitengeneza na watafanikiwa kuifikia kwa njia zipi na kwa muda gani. Timu yoyote duniani lengo kubwa Ni KUSHINDA vikombe kwa uelewa wangu mdogo, au niseme Ni kutengeneza timu yenye ushindani. Sasa hebu tujiulize Yanga pamoja na kuongoza ligi tuna timu ya kushindana? Kwangu Mimi jibu Ni Hapana. Sasa Kama jibu Ni Hapana uongozi ndiyo umeboresha timu kwa kutuletea wachezaji Kama Fiston, alafu tunadanganyana tutunishe vifua ubingwa Ni wetu mwaka huu? Kwa wachezaji Hawa wa kuokoteza? Kazi viongozi imekuwa ni kulalamika tuuu badala kuangalia tunajikwamua vipi. Anyway labda Mimi peke yangu ndiyo sielewi.

4. Washabiki na Wapenzi

Tuna tatizo la kuhemuka, tunaaminishwa mambo mengine ambayo kiukweli hayawezekani nasi tunakubali. Tuungane kuwaambia ukweli Hawa viongozi ndiyo watabadilika. Tukiendelea hivi kuwapa support wanaona sawa tu, mwishowe mtaikuta timu Hiko nafasi ya kumi huko au inastruggle isishuke daraja. Tafadhari tuwe wamoja katika hili. Wakifanya vizuri tuwape sifa, wakiboranga tuwape ukweli wao.

NB:
Ukweli utaniweka huru. Tatizo kubwa la Yanga ni mfumo wa uendeshaji wa klabu. Tufanye haraka twende kwenye mabadiliko ambayo yatafanya timu kuwa vizuri kiuchumi hivyo kutuwezesha kutengeneza timu bora ya ushindani. Wakati Ni sasa Wala hatujachelewa.

Msimu ujao napendekeza Hawa wachezaji wa kigeni tubaki na wachache tu wenye tija, tusajili wachezaji wa ndani na wenye uwezo, hii iatatusaidia kupunguza gharama za uendeshaji kabla ya mabadiliko wakati Mikakati wa mabadiliko ukiendelea.

Mwisho nasisitiza tuwe na Mikakati ya kuutafuta ushindi, kiufundi ndani na nje ya uwanja. Tusiwe wa kulalamika kutafuta huruma. Tuige kwa wenzetu wanafanyaje, tutafika tu. Samahani uandishi nao Ni kipaji na Ni taaluma pia, inawezekana mipangilio na uandishi wangu siyo mzuri Ila nadhani nimeeleweka.

Yanga daimambele, nyuma mwiko,

Asanteni
 
Kama vile ki George Ambangile ni kishabiki cha Utopolo nimeamini. Eti jana kinasema mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi, hata Simba watapoteza tu. Nadhani kuna baadhi ya vichambuzi vya soka vipo kwenye payroll ya GSM.
 
Kama vile ki George Ambangile ni kishabiki cha Utopolo nimeamini. Eti jana kinasema mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi, hata Simba watapoteza tu. Nadhani kuna baadhi ya vichambuzi vya soka vipo kwenye payroll ya GSM.
Kiranja wao ni Kijola aka Kidoti yule aiyekuwa na kichogo.
 
Mindset za viongoz wetu mkuu n tatizo hawawez kutuvusha

Msola + mwakalebela never ever hatuwez toboa
Hili la Msola na Mwakalebela tumeonya sana kuwa hawa jamaa wapo kwa maslahi yao, hivi lile tumbo la Mwakalebela mnafikiri linatosheka na mshahara?
 
😝😫hakuna point ulioongea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…