Yanga ina tatizo la kocha, wachezaji au viongozi?

Hakika umenena vyema! Timu yetu ilishakua na tatizo la washambuliaji tangu mwanzo wa msimu!

Cha kushangaza wakati wa dirisha dogo, uongozi wakishirikiana na mwalimu Kaze, wakasajiri washambuliaji wao ambao mpaka sasa hawajaonesha faida yoyote ile kwa timu!

Huyu Fiston sijui hata kama anastahili kuongezewa hata mkataba baada ya huo mkataba wa miezi sita aliopewa kumalizika. Kiukweli kiwango chake kimeshuka sana. Saido ndiyo kwanza anaendelea tu kula mafao.
 
Unasajiri wastaafu halafu unataka ushindi hiyo n ngumu kocha kajaza warundi wenzake ili apige 10% kaze siyo fala anajua kula na mazwazwa
 
Timu haifanyi vizuri, ushindi mwembamba, sare nyingi na sasa imefungwa, tena kiuhalisia ilipaswa iwe imefungwa na kagera sugar pia.

Tatizo la Yanga ni kocha, wachezaji, wafadhili au viongozi wa Yanga?
Yanga 70% ya tatizo ni kocha, kocha ana miez 5+ ila timu haijulikan inacheza mfumo gan na ameshindwa ku improve wachezaji, beki mbovu, kipa matatizo ni yale yale, Tuisila tokea anafika alikuwa na tatizo la mipira ya mwisho mpaka leo bado ana udhaifu huo, kiufupi siyon kitu kocha alichokifanya.
 
Nguvu ndogo ya uwekezaji...kwa modern soccer klabu kama yanga hutakiwi kuwa na watu kama Nchimbi,Niyonzima,Faridi,Zawadi,Kaseke,adeyum,Barama
dawa ni kuongeza viungo na straikers wazuri toka nje
Viwango vya wachezaji wazawa vipo chini mno tanzania
Mfano mzuri ni timu zetu za taifa,shida iko hapo tu Kaze,uongozi wapo vizuri
 
Hata dereva nae ni tatizo
 

Attachments

  • IMG-20210305-WA0040.jpg
    56.3 KB · Views: 1
Timu haifanyi vizuri, ushindi mwembamba, sare nyingi na sasa imefungwa, tena kiuhalisia ilipaswa iwe imefungwa na kagera sugar pia.

Tatizo la Yanga ni kocha, wachezaji, wafadhili au viongozi wa Yanga?
Samaleko
 
Shida ni kwamba mnataka mjifananishe na simba.
Wakati simba mwenzenu kasajili wachezaji wazuri sababu ya hela.
Binafsi yangu simba ikishinda sishtuki.ila wakifungwa uwa najiuliza wamefungwa vipi wakati wana wachezaji wazuri
 
Uelewa wako ni mdogo sana kuhusu soccer. Kwahiyo hiyo mechi yenu na coastal simba walifanya nini!!?? Waliwaroga miguu na akili!! Mitazamo kama hii ya kijingajinga ndo inafanya soka la bongo libaki gizani, mnashindwa kushughulikia mapungufu yenu mnatafuta mchawi nje!!!! Upumbavu mtupu.
 
Natamani mashabiki na wanachama wote wangekuwa wanajitambua kama wewe, mngefika mbali sana.
 
Mechi yetu na Coasta tulifungwa kwakuwa timu yetu ni mbovu sana.
Wachezaji wetu wamelegea,kwanza awalipwi mishahara yao.

Hata chakula tu kwa wachezaji ni cha kuungaunga.
Kocha mazoezini anafundisha wachezaji kurusha ngumi na kung fu.

Nisaidieni mashabiki wa Simba,kuamia Simba shilingi ngapi?
 
Tatizo la Yanga n huwo Mwiko, walouweka nyuma, wautoe haraka.
 
Mkuu upo sahihi 100%
 
Muongo, usipotishe wasomaji wa jf. hata wakati wa Malinzi Simba ilikuwa lialia sana na waamuzi wakidai wanaonewa na yanga inabebwa na tff.
 
Tatizo ni wachezaji wazawa,wengi wao kama si wote viwango vipo chini sana ..sasa kwa soka la kiwango stahili kwa level ya yanga tusitegemee wazawa hawa kutupa matokeo...
Tumeona jana makosa ya beki iliyojaa wazawa ilivyoikosti timu
Haya unamtoa Niyonzima unamuingiza zawadi yale ni makosa mengine japo hata huyo Niyonzima naye ashachoka sasa
 
Mpira ni mchezo wa wazi, kama wanaonewa ni rahisi kila mtu kuona. TFF imeishughulikia vipi kesi ya morison kwamfano,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…