kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Sera ya Yanga ya kuachana na wachezaji wake walioumia viwanjani inaidhoofisha yanga. Mwenzako akinyolewa tia zako maji ndicho kinachoendelea kwenye akili za wachezaji.
Wachezaji Yanga wameingiwa na hofu ya kucheza kwa kujituma kwa kuhofia kupata majeraha mabaya, na hii ndio sababu wachezaji wa Yanga wanakuwa wakali sana na hata kujichukulia hatua mkoni dhidi ya wachezaji wanaowachezea vibaya uwanjani. Hofu hii inasababishwa na utamaduni wa yanga wa kuchukia na kuwakataa wachezaji wanaopata majeraha makubwa wakiwa kwenye mazoezi na kwenye mechi. Hawajitumi kwa kuogopa kupata majeraha mabaya yatakayowafukuzisha kibarua.
Yanga imeachana na wachezaji kibao wa aina hiyo wakiwemo akina Mahadhi, Balama, Yacouba na Kambole. Tabia hii haikubaliki kwa wachezaji hasa wale wageni, maana inawafanya wafikirie mara mbilimbili wanapokuwa kiwanjani.
Hakuna namna nyingine ya kukabiliana na wachezaji wenu wanaoumia badala ya kuachana nao?