Yanga inahitaji sajili 4 bora za uhakika ili kuwa na timu kamili

Yanga inahitaji sajili 4 bora za uhakika ili kuwa na timu kamili

Me kama mwana yanga napendekeza au kutoa ushauri kwa rais hersi kufanya sajili za wachezaji kama ifuatavyo.

1. Striker, yanga inahitaji mfungaji mwenye ubora anaeweza kumililiki mpira,kufunga na mwenye nguvu. Hawana kina mzize sio wa wabovu ila ligi ya mabingwa hawana uwezo huo.

2. Kiungo mkabaji halisi au holding midfielder, sana sana apatikane holding midfielder mwenye ubora, aucho anapendeza kucheza kama Central midfielder na sio kama anavotumika pale yanga kama holding midfilder.

Kabla sijaendelea nieleze kidgo tofauti ya holding midfielder na Central midfielder na sifa zao.
-Holding midfielder ni kiungo ambaye eneo lake ni mbele ya mabeki na majukumu yake kuichezesha team kutokea chini na kusaidia kukaba, sifa zao wanakuwa na uwezo mzuri wakupiga pasi fupi na ndefu .

Central midfielder huyu ni kiungo wa kati na majukumu ya ni kuichezesha team kupitia yeye hapo kati kati ya uwanja, kiungo huyu huunganisha team team kutoka nyuma kwenda mbele na sifa zake ni awe mzuri ktk kupiga pasi za uhakika fupi fupi na ndefu, huyu ndo anaamua team ichezeje kutokana na uwezo wake wa kulitawala dimba na pasi zake za uhakika.

Ukiangalia sifa zao hapo utagundua kwanza aucho ni mzuri wa kupiga pasi sahihi na ni mchezaji anayelazimisha team iende mbele kwa pasi zake, ni mara chache sana aucho kupiga back pass.

Aucho hana kasi sana kumchezesha nyuma ndomna mara nyingi anapigwa sana kadi za njano akipitwa anacheza rafu,

Asajiliwe holding midfielder ili aucho apogee awe Central midfielder na pacome acheze eneo la aziz ki.

Winga mbunifu, moloko ni winga wa kizaman sana anapswa kuachwa haraka sana anaziba nafasi za wachezaji wa kimataifa, tunahitaji winga mwenye uwezo wa kulifata box la adui akiwa na mpira na mwenye kasi. Muangalie yule hussein el shehat wa Al ahly hawa ndo mawinga wa kisasa. Yanga itafute winga wa maana iachane na huyu moloko.

Beki 3 mwenye nguvu za kupanda na kushuka kama yao, huyu lomalisa mzuri sawa lkn nafikir anahitajika mbadala wake kama yule haji mwinyi.

Kingine kocha aache kukariri kwamba lazima aziz ki acheze, mechi hizi za kimatafa kwa uchezaji wa aziz ki wa kuchelewa kufanya maamuz tutamlaumu tu. Mechi kama Al ahly mtu kama max anapaswa kucheza lile eneo la aziz ki kwasabab max yupo faster sana hapotez muda kukaa na mpira na ana maamuz ya haraka sana kwenda mbele.
Nungunungu The Great anawatosha!
 
Quality kweli huzungumza, wale jamaa (ahly) hata wakifungwa unaona kabisa ubora wa watu walionao hii inanikumbusha mazembe ilee, quality zipo ni scouting nzuri na kumwaga pesa.
 
Umenena vema sana bro! japo kwa kipindi cha dirisha dogo walau watuletee striker wa maana,hayo mapungufu mengine wanaweza kuyajaza kipindi cha dirisha kubwa. Striker ni tatizo kubwa sn Yanga kwa sasa.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app

Hata siku moja popote duniani huwezi kupata striker au hata kocha bora kwenye dirisha dogo! Utapata makabradha tu!
 
Skudu, konkoni na moroko wanatoka
Tunaingiza majembe mengine
Azizi ki ni mchezaji mkubwa pale yanga ndo maana coach hamfanyii sub ovyo
Anaweza fanya chochote muda wowote hadi ukashangaa
Ndo maana hata game imkatae Mesi au Ronaldo coach hafanyi sub kuwatoa
Coach Gamondi ni supper
Jana aziz ki alitakiwa atoke mchango wake ulikuwa Mdogo na ameshatoka mara nyingi sana mechi zilizopita , sijui gamondi alimsahau vipi akamtoa nzengeli 😁ni maajabu ya Mpira wakati mungine kama yale ya mchezaji kufanya rafu kadi akapewa mungine.

Moloko ni mchezaji mzuri wa ku press asitolewe .
Skudu Naye hajapata nafasi ya kutosha

Konkoni out
 
Jana aziz ki alitakiwa atoke mchango wake ulikuwa Mdogo na ameshatoka mara nyingi sana mechi zilizopita , sijui gamondi alimsahau vipi akamtoa nzengeli [emoji16]ni maajabu ya Mpira wakati mungine kama yale ya mchezaji kufanya rafu kadi akapewa mungine.

Moloko ni mchezaji mzuri wa ku press asitolewe .
Skudu Naye hajapata nafasi ya kutosha

Konkoni out
Hivi mfano angetoka Aziz Ki je nafasi yake angechukua nani pale benchi?
 
Baada ya kufungwa na Medeama week ijayo tutamlakamikia pia hersi, mdhamini, na tff
 
Yanga imepata pengo la Mayele tu
Timu ibaki hiyohiyo umrejeshe Mayele tu ubingwa wa Africa mnachukua.
Jana Yanga ilicheza na mshindani mwenye misuli mikubwa ndio maana mmeyaona hayo mapungufu.
 
Quality kweli huzungumza, wale jamaa (ahly) hata wakifungwa unaona kabisa ubora wa watu walionao hii inanikumbusha mazembe ilee, quality zipo ni scouting nzuri na kumwaga pesa.
Ile kauli kuwa Ahly ni wachovu mnaikana?!
 
Aziz Ki anataka kila mara afanye dribbling, take on, badala ya kufanya quick one touch passing.
Anapokaa na mpira muda mrefu adui wanjipanga, wanarudi kuziba nafasi.

Max mzuri sana lakini siyo big game player. Anapotea kwenye big occasions, kama jana na Al Ahly alipotea alitakiwa afanyiwe substitution mapema sana.
Pacome ni big game player.
 
Jana aziz ki alitakiwa atoke mchango wake ulikuwa Mdogo na ameshatoka mara nyingi sana mechi zilizopita , sijui gamondi alimsahau vipi akamtoa nzengeli [emoji16]ni maajabu ya Mpira wakati mungine kama yale ya mchezaji kufanya rafu kadi akapewa mungine.

Moloko ni mchezaji mzuri wa ku press asitolewe .
Skudu Naye hajapata nafasi ya kutosha

Konkoni out
Wakati nzegeli anasaidia sana kukaba alafu nzegeli ni mzuri akicheza lile eneo la aziz ki kuliko akicheza winga
 
Back
Top Bottom