uran
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 10,392
- 15,948
Twende kwa mifano zaidi ili usomeke.Kwakua umetaka kueleweshwa ngoja nikueleweshe, Holding midfielder sio namba 8, holding midfielder huwa pale mbele ya mabeki, ni kama DM lkn tofauti ni majukumu yao.
DM majukumu yake namba 1 uwanjani ni kukaba, hawa hawana majukumu ya kushambulia lbda kama ziada tu , ila jukumu lao namba 1 ni kukaba, DM huwa anazunguka sana uwanjan kuutafuta mpira na ndo jukumu lake namba 1 uwanjani ila eneo lake ni pale mbele ya mabeki mfano halisi muanglie ngolo kante .
Holding midfielder na yeye eneo lake ni hilo hilo kama DM ila majukumu yake ni tofauti, Holding midfielder yeye majukum yake ni kuichezesha team kutokea huku chini na huwa hana movement nying uwanjan kama DM. Alafu holding midfielder sio lazma awe na mwili au manguvu ila at awe na uwezo wa kupiga ndefu na fupi, ni mtu anayeanzisha mashambuliz kutokea chini, mfano kwa bongo ni mkude au alonso kama ulimuona enzi zake.
Sasa kitu kingine kila kocha na mfumo wake anaouamini, kuna makocha wanapenda kutumia holding midfielder na kuna ambao wanapenda kutumia DM au wapo ambao huwatumia wote kwa pamoja.
Kwa mfano yanga ya nabi ilikua ikimtumia bangala kama holding midfilder wakicheza na aucho eneo hilo wakiwa na majukumu sawa.
Kama ulivyofanya kwa kutoa mfano wa Ngolo Kante,
by the way wewe ni analyst mzuri.
Unawazidi kwa mbali wachambuzi wengi uchwara.