Yanga inahitaji sajili 4 bora za uhakika ili kuwa na timu kamili

Nyie vigeugeu sana. Si mlisema mna timu bora haya maneno yote yanatoka wapi? Tena mlisema Al Ahly anakufa nje ndani🤣🤣
 
Namaanisha aucho asogee awe Central midfielder atoke huku kwenye holding, asajiliwe holding midfielder akikosekana holding basi asajiliwe deffensive midfilder wa viwango
Hivi au mm ndo sielewi hizi position za wachezaji?
Umeongelea Central Midfielder, Holding Midfielder na Defensive midfielder.

Navyofaham mm, CDM ndo number 6 mwenyewe na hucheza mbele ya back 4, Holding ndo number 8 mwenyewe nae hucheza mbele ya no 6 au nyuma ya no 10 ingawa 6 na 8 wote hucheza interchangeably.

No 8 kazi yake ndo ile umesema kupiga pass fupi fupi na ndefu kuichezesha tem ndo maana anaitwa holding. Huamua tem ichezeje na ndo kazi anaifanya Aucho pale yanga ingawa pia hucheza kama CDM kwenye double pivot wakisaidiana na Mudathir au Mauya.

Labda mnisahihishe wajuzi wa boli.
 
Kufundisha soka bongo taabu kwelikweli. Kila shabiki ni kocha. Sijui kwanini vilabu vinaingia gharama kubwa kuleta makocha wa bei mbaya wakati vingeweza kuchukua shabiki kama wewe ukawa kocha.
Mimi nimecheza mpira ligi daraja la pili kwahiyo naujua mpira kuliko wewe hapo,na pia mimi ni shabiki wa yanga kuna upuuzi mwingi huwa unafanyika huo lazima tuukemee
 
Wakati nzegeli anasaidia sana kukaba alafu nzegeli ni mzuri akicheza lile eneo la aziz ki kuliko akicheza winga
Half time yanga iliongoza possession 54% Ahly 46% sababu ya nzengeli na Pacome katikati .
Hata hivyo sub ya musonda ilichangia kwa kutoa assist lakini ingependaza atoke aziz ki badala ya Musonda.
 
Kabla ya lomalisa kutoka Max alikuwa akicheza vizuri kutoka kwa lomalisa kuliharibu game plan na role ya max kupotea
 
Pacome angeshuka chini acheze na aucho max acheze nafasi ya azizi ki
 
Umeshauri kitaalam sana. Na maoni yako ni sahihi kwa 💯%.
 
Acha ushabiki mandazi
Mimi sio shabiki mpuuzi kama wewe ambao munageuzwa na wapuuzi wakina alikamwe na privaldinho wasioujua hata kupiga danadana mara muvae msuli mara dakika ya saba musimame mara kuweka bango la goli 5 huu ni zaidi ya upuuzi na ujuha,unajua kabisa unataka kushiriki champion league halafu eti una wachezaji kama mzize,musonda na konkon
 
Nyie vigeugeu sana. Si mlisema mna timu bora haya maneno yote yanatoka wapi? Tena mlisema Al Ahly anakufa nje ndani[emoji1787][emoji1787]
Nilisema lini? Angalia hapa niliongea nini tangia mwezi wa nane baada ya mechi ya gao ya jamii nilisema kipi.

 
Kwakua umetaka kueleweshwa ngoja nikueleweshe, Holding midfielder sio namba 8, holding midfielder huwa pale mbele ya mabeki, ni kama DM lkn tofauti ni majukumu yao.

DM majukumu yake namba 1 uwanjani ni kukaba, hawa hawana majukumu ya kushambulia lbda kama ziada tu , ila jukumu lao namba 1 ni kukaba, DM huwa anazunguka sana uwanjan kuutafuta mpira na ndo jukumu lake namba 1 uwanjani ila eneo lake ni pale mbele ya mabeki mfano halisi muanglie ngolo kante .

Holding midfielder na yeye eneo lake ni hilo hilo kama DM ila majukumu yake ni tofauti, Holding midfielder yeye majukum yake ni kuichezesha team kutokea huku chini na huwa hana movement nying uwanjan kama DM. Alafu holding midfielder sio lazma awe na mwili au manguvu ila at awe na uwezo wa kupiga ndefu na fupi, ni mtu anayeanzisha mashambuliz kutokea chini, mfano kwa bongo ni mkude au alonso kama ulimuona enzi zake.

Sasa kitu kingine kila kocha na mfumo wake anaouamini, kuna makocha wanapenda kutumia holding midfielder na kuna ambao wanapenda kutumia DM au wapo ambao huwatumia wote kwa pamoja.

Kwa mfano yanga ya nabi ilikua ikimtumia bangala kama holding midfilder wakicheza na aucho eneo hilo wakiwa na majukumu sawa.
 
Kiufupi ni kwamba holding midfielder na DM wote eneo lao ni hapo mbele ya mabeki ila tofauti ni majukum yao uwanjani.

Alafu huo mpira wa kutaka sijui namba 8 ni mpira wa kizaman na ilitokana mfumo maarufu wa enzi hizo 4 4 2.

Kwasasa mifumo ndo inacheza, mfano Makocha wengi hutumia wachezaji wawili mbele ya mabeki, hata simba na yanga wanapenda kutumia hii mifumo,mechi za ligi gamond huwatumia aucho na mudathir eneo hilo.. mudathir huwa ana movement nying sana uwanjan ila aucho huwa hana movement nying uwanjan, anachokifany ni kuchezesha team kutokea huku chini na mudathir anakaba zaid na kusaidia ktk kushambulia.

Lkn maoni yangu yanabaki pale pale aucho ni mzuri akicheza central midfielder. Kwasababa atakua eneo la kati pale ataichezesha team vzr kutokana na uwezo wake wa pasi fupi fup na pia ataepuka kadi nying za njano.
 
Taratibu naiona yanga ikiua vipaji vya sure boy na moloko.
Sure boy anakalia mbao akina mauya wanapata namber maajab haya.
 
Hivi kwann wabingo tukishapata matokeo tuliokua hatutarajii basi ndio tunaona ubovu wa kikosi au mapungufu ila kabla ya hapo mtu anajiamini na kusifu timu imekamilika inakikosi kipana
Ni mashabiki wa soka dunia nzima hasa nchi za mpira tena si tuna nafuu lakini nchi zote zenye amsha amsha za mpira huwa mechi ikiisha lazima maoni yawe mengi
Ndio maana Bayern Kila Leo wanabadili kocha Chelsea ndio kabisa PSG nadhani mwenyewe huwa unaona
Ni kwamba mashabiki Wana push kupata kilicho bora kama haya huyapendi shabikia Azam hutasikia shida
 
Mimi nimecheza mpira ligi daraja la pili kwahiyo naujua mpira kuliko wewe hapo,na pia mimi ni shabiki wa yanga kuna upuuzi mwingi huwa unafanyika huo lazima tuukemee
Hata usingecheza haki ya kutoa maoni ni Yako na ndio inayoleta mabadiliko kuliko kukaa kimya kama mtu anataka team isiyokosolewa basi Azam IPO
Ila Jana yanga Kuna makosa yalikuwa wazi sana kama ilivyokuwa kule Algeria lazima yasemwe
Sub zilichelewa
Strikers bado hawatoshi
Winga alihitajika sana
Beki namba 3 anahitajika sana kibabage ni level ya ligi kuu na FA
 
Huyuhuyu Aziz K au mwingine?!?? Uto ktk ubora wako!
 
Tulikubaliana Simba ni mbovu ila nyie mko imara mtampiga yoyote, vipi nini kimetokea?.
Ulikubaliana na nani?
Mashabiki wengine wasimba ni washamba sana.
Wenzio wanaongea point wewe unaleta upupu.
Mnaifanya Simba yetu kuonekana ina mashabiki mbumbumbu.
 

Yanga haina Tatizo lolote kwa Sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…