mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Kila la heri wananchi japo nyie mna roho mbaya!!View attachment 2847530
Ki ukweli japo mi shabiki wa Simba nataka pia Yanga apite robo, sababu itakuwa heshima kwa TZ kuwa na timu mbili robo fainali, katika timu 8 (Hata Misri ni mara chache anafanikiwa kuingiza timu 2 robo fainali)
Ili Yanga awe na nafasi ya kufuzu robo sio tu amfunge Medeama bali anatakiwa kumfunga kwa goli 5 au zaidi
Likely Scenario ipo hivi
Yanga anagombea nafasi ya pili na C.R.B huku yanga akiwa na goal difference ya -3 wakati CRB ana +2
Yanga akishinda goli 5 atakuwa na pointi 5 na G.D ya +2 na CRB akitoa draw na Ahly kule Algeria (likely scenario) naye atakuwa na pointi 5 na G.D yake ikibaki +2 na Yanga kuwa nafasi ya tatu
Mechi ya 5 Yanga dhidi ya Ahly kule Misri akijitahidi akifungwa 2-1 bado atakuwa na pointi zake 5 bado na goal diffence ya +1
CRB akimfunga Medeama kule Algeria 2-0 naye atakuwa na pointi 8 na G.D ya +4
Mechi ya mwisho Yanga dhidi ya CRB anamfunga goli 3-0 kwa Mkapa anakuwa na pointi 8 na G.D ya +4 huku CRB akibaki na pointi nane pia na G.D ya +1 na Yanga anapitaa kwa kuwa na magoli mengi
So mechi ya kesho ndio mechi pekee ambayo Yanga ana nafasi kubwa ya ushindi, ushindi basi uwe mnono....
Wakilingana pointi wanaangalia mlipokutana nyie nani alikuwa mbabe? Walipokutana wao Yanga alikula kichapo cha 3 kwa sifuri!! Ili kulifuta hilo watakapokutana tena kwa Mkapa Yanga inabidi amshinde CRB goli 4 kwa bila!! Je ubavu huo anao?Itaishiaje hapo wakati atakua na point tano kama Yanga?
Mkumbuke kuwa Al Ahly alishindwa kabisa kumshinda CRB akiwa nyumbani, je atakapokuwa ugenini ataweza? Mahesabu ya Al Ahly ni kumfunga Yanga wala si kumfunga CRB. Al Ahly hana ubavu wa kumfunga CRB ugenini!!