Ally anaonekana kuwa na point moja muhimu. Hakuna ujinga unaozidi ule wa kila siku Mikia wakifanya jambo Yanga nao wanajaribu kuonyesha kuwaliwahi kufanya enzi zile. Mbumbumbu akijaza uwanja Yanga wanalilia haki ya wao kujaza uwanja enzi za Manji, what for? Mbumbumbu wakifurahia kupanda ndege Yanga nao wanadai walizipanda mpaka wakachoka!!
Sehemu moja muhimu nitakayompinga Ally ni kwenye kuteka soko. Ukiangalia kwa makini soka la Tanzania linavuma na upepo. Kilichopo Simba kwa sasa ni kile kile kilichopata kuwapo isipokuwa kimeboreshwa kiasi. Wakati Simba inakwenda kwa ya mtu mmoja, siku akisusa kama ilivyotaka kutokea mpaka waziri na rais wakaingilia, mfumo mzima wa club utaanguka. Kwa maoni yangu si vema timu ikaendeshwa kwa kivuli cha wanasiasa ambao hubadilika mara kwa mara. Ingawa hoja ya Mwakyembe kuhusu kuwa na wawekezaji zaidi ya wawili ilipingwa sana, lakini faida yake itaonekana siku Mo akijikuta hana nguvu tena ya kuendeleza ufadhili wake. Kwa sasa Simba wanafurahia mafanikio ya muda mfupi kulingana na upepo wa kisiasa uliopo, ndio maana mpaka mashabiki wake wanatamba kuwa Simba ni serikali. Sasa kumbukeni yaliyopo yamekwisha kuwapo.
Kwa upande wa Yanga, mfumo uliopendekezwa na Rostam nadhani ndio sahihi kwa nature ya vilabu hivi. Tukubali tukatae, Mikia na Wananchi ni timu zenye mtazamo wa kisiasa zaidi kuliko michezo. Mkono wa siasa una nguvu mno kuliko uhalisia wa michezo, kiasi kwamba wanasiasa wamejinasibu wazi kuwa hawawezi kuziacha timu hizo. Sasa mwenendo huu ni adui mkubwa wa mafanikio ya muda mrefu kwenye michezo. Timu ya Yanga ijikite kuhamasisha wanachama, waanzishe kanzi data kama timu, wapate mapato kutokana na wanachama hao. Mfuno huu utafaa sana kwa muda mrefu, kama timu itaacha kusaka mafanikio ya muda mfupi ili kushindana na Simba.
Habari ya kuteka soko kwa soka la bongo ni upepo tu, siasa ndizo zitaamua.