Yanga inatakiwa iache kushiriki kwa kukariri

Yanga inatakiwa iache kushiriki kwa kukariri

Uwe unatafakari kabla ya kuandika, huoni Simba wanaitoa timu yao(na mpira) kwenye Siasa, yaani kutegemea makomandoo na wanachama badala yake unafanyika uwekezaji? Wakati sisi bado tupo kwenye slogan za kisiasa. Viongozi wa Sasa wa Yanga hawana uwezo wa kutuvusha muda utaongea.
Tumia akili kuandika, nani alikwambia makomandoo ndio wanasiasa? Halafu unaposema mikia wako hawategemei wanachama unatumia nini kufikiri? Ni timu gani isiyotegemea mapato yake kutoka kwa wanachama na mashabiki? Unajua kwa nini African
Lyon na Singida utd zilimshinda Mo? Kweli Rage hakukosea...
 
Mbumbumbu utamjua tu, lililoandika hapa ni Mamluki la Mikia sio Ally Mayai hawezi andika upupu huo
Huoni aibu wewe kumuita Ali Mayai mamluki???Huwezi kufikia hata kidogo alichoifanyia Yanga.Sidhani hata kama wewe ni mwanachama wa Yanga.Tabu ya wapenzi maandazi kama wewe mkiambiwa ukweli kwenye hizi timu mbili mnakimblia kumuita aliyesema ukweli mamluki badala ya kujibu hoja kwa hoja.
 
Mbumbumbu utamjua tu, lililoandika hapa ni Mamluki la Mikia sio Ally Mayai hawezi andika upupu huo
Wewe ndio uliyemuita mamluki. Uwezo wako wa kufikiri unayumbishwa na upepo unapoelekea.Sasa unamtetea??Mbutembute.
 
.......as long as timu inafanya vizuri ndipo lilipo tatizo. Wewe ufahamu wameshaelewa
Sisi timu yetu inaendeshwa kwa mfumo mpya uliopitishwa na wanachama so tunaendesha timu kwa katiba yetu wenyewe tulioipitisha...nyinyi yanga mnaendesha timu kwa mfumo wa harambee na mabakuli ambao mumeamua wenyewe...cha msingi kila timu ikomae na mfumo wake....WAJINGA NDI WALIWAO
 
Mkuu tambua Yanga ilikua kwenye misuko suko kwa miaka 2,huu uongozi mpya ndio kwanza una miezi 5,mambo mengi mazuri yanakuja ikiwemo hiyo hisa ambayo Yanga wala ahitaji kubadilisha katiba,mfumo wetu tutakaokuja nani ule wawekezaji zaidi ya mmoja,na hao wawekeza wapo,yashatukuta sie kumtegemea mtu m1 hlf mnaanza kumuabudu km Mungu!
Ni vzr sana... sio wengine kusifia bakuli
 
Kama makomandoo wa yanga wamewasilisha barua ya malalamishi yao kwa uongozi na mmepublish kwenye akaunti ya club,kumbe mayai kupublish maoni yake yuko sawa inaonekana ni utamaduni wenu
Huyo mjinga anapangia watu sehemu ya kutoa maoni yao sjui yeye kama nani?
 
Ally anaonekana kuwa na point moja muhimu. Hakuna ujinga unaozidi ule wa kila siku Mikia wakifanya jambo Yanga nao wanajaribu kuonyesha kuwaliwahi kufanya enzi zile. Mbumbumbu akijaza uwanja Yanga wanalilia haki ya wao kujaza uwanja enzi za Manji, what for? Mbumbumbu wakifurahia kupanda ndege Yanga nao wanadai walizipanda mpaka wakachoka!!

Sehemu moja muhimu nitakayompinga Ally ni kwenye kuteka soko. Ukiangalia kwa makini soka la Tanzania linavuma na upepo. Kilichopo Simba kwa sasa ni kile kile kilichopata kuwapo isipokuwa kimeboreshwa kiasi. Wakati Simba inakwenda kwa ya mtu mmoja, siku akisusa kama ilivyotaka kutokea mpaka waziri na rais wakaingilia, mfumo mzima wa club utaanguka. Kwa maoni yangu si vema timu ikaendeshwa kwa kivuli cha wanasiasa ambao hubadilika mara kwa mara. Ingawa hoja ya Mwakyembe kuhusu kuwa na wawekezaji zaidi ya wawili ilipingwa sana, lakini faida yake itaonekana siku Mo akijikuta hana nguvu tena ya kuendeleza ufadhili wake. Kwa sasa Simba wanafurahia mafanikio ya muda mfupi kulingana na upepo wa kisiasa uliopo, ndio maana mpaka mashabiki wake wanatamba kuwa Simba ni serikali. Sasa kumbukeni yaliyopo yamekwisha kuwapo.

Kwa upande wa Yanga, mfumo uliopendekezwa na Rostam nadhani ndio sahihi kwa nature ya vilabu hivi. Tukubali tukatae, Mikia na Wananchi ni timu zenye mtazamo wa kisiasa zaidi kuliko michezo. Mkono wa siasa una nguvu mno kuliko uhalisia wa michezo, kiasi kwamba wanasiasa wamejinasibu wazi kuwa hawawezi kuziacha timu hizo. Sasa mwenendo huu ni adui mkubwa wa mafanikio ya muda mrefu kwenye michezo. Timu ya Yanga ijikite kuhamasisha wanachama, waanzishe kanzi data kama timu, wapate mapato kutokana na wanachama hao. Mfuno huu utafaa sana kwa muda mrefu, kama timu itaacha kusaka mafanikio ya muda mfupi ili kushindana na Simba.

Habari ya kuteka soko kwa soka la bongo ni upepo tu, siasa ndizo zitaamua.
Simba tunalimiliki soka la Tanzania utake usitake
 
Upuuzi mtupu huu, simba mna kitu gani cha ajabu zaidi ya kutegemea pesa za Mo... Mo nae ni binadamu (siombei) lakini mtoa uzi umewahi kujiuliza mfano Mo akifariki sasa hivi timu ya simba hali yake itakuaje yani kitu ulichokifanya hapa ni sawa na kwenda na v8 ya baba yako kumchimba mkwara kijana mwenye ist yake binafsi

Narudia tena upuuuzi mtupu na wote waliokuunga mkono ni fans wa mkia fc
Hadhi ya klabu yako kuwa mtani wa Simba imeshapotea hivyo ni kheri ukaacha hata kuiita mikia klabu ya Simba
 
Mfumo wa hizo klabu unaujua? Hivi unajua Chelsea ni kama Azam? Unajua timu kama Man U ina wanahisa kadhaa walioweka mzigo mezani? Simba ina wanahisa wawili, Mo na wanachama wasiotoa hata senti moja zaidi ya kuandamana.
Umeshawahi kujiuliza kwamba BAKULI LOTE PAMOJA NA KUBWA KULIKO' .. kwa nini wachezaji bado wanadai pesa zao?
 
Tofauti ya Manji na Mo ni tofauti ya muda na support ya serikali sasa hivi au niseme elimu kwa lugha nyingine, unadhani kwanini Mwakyembe aliposema.muwekezaji asimiliki 50% za hisa watu wa walianza kusema kua anataka kuwaharibia timu yao
Vyovyote mtakavyomuita Mo , muwekezaji au mfadhili ila haipingishi kua kitu anachokifanya ni zaidi ya uwekezaji/ufadhili kifupi ni mapenzi binafsi jambo ambalo kama siku likikoma kwa sababu yoyote ile (auze hizo hisa, afariki, au abadilishe mawazo) piga ua ni lazima simba ita shake tu hivyo mtoa uzi anapokuja na maneno yake ya kipuuzi kuwashambulia yanga namuona kama kituko maana kitachowatokea simba hakitakua na tofauti na kilichoikuta yanga wakati ule wa manji (japo mnasema kuna tofuati kati yake na Mo)
Simba haina mwanachama tajiri mmoja tu wapo wengi sanaa, yani unazungumza vitu vya kizamani sana (zilipendwa) kama sio mtu wa mpira bwana.
.
Roman abrahamovich anaimiliki Klabu ya Chelsea siki akifa na klabu nayo itakufa au itashuka daraja?
Moise Katumbi siku akiondoka Tp mazembe unadhani itaacha kuwa timu tishio Africa? Come on
 
Huoni tofauti kati ya Mo na Abramovich? Acha utani wewe Abramovich ile timu kainunua mwenyewe kwa ela yake miaka ya 2003 huko kweli huoni tofauti mzee au unaongelea ushabiki, Tp mazembe kumbuka ni ya huyo huyo Katumbi mwenyewe , kuwe na mfumo wa hisa au hakuna ila Abramovich ndiye mwenye timu ya chelsea tofauti na huku simba,

Kwani simba ni timu ya Mo? kainunua au kaanza kuimiliki mwaka gani, navojua mimi simba ilikua kama yanga tu timu ya wananchi hasa ukiniambia huoni tofauti kati ya Abramovich na Mo nakushangaa sana sababu Abramovich muda wowote hata huyo katumbi wakiamua kuziuza hizo timu wanaweza je Mo anaweza kuiuza simba akiamua?

Afu labda lugha ndio imekuchanganya naposema Mo kuondoka namaanisha hata akibadilisha maamuzi au kutoendelea na huo unaouita uwekezaji... Sasa suala la kusema kusema nimekazania hapa Mo akiondoka hio ndio hoja yangu ukitaka niache kusimamia hapo basi tusingekua tunajadili hapa maana ake wote tungekua side moja
Nimesoma comments zotee nilivyofika hapa nikacheka sasa wewe unabisha nini?
.
Huko mwanzo umesema Mo anatengeneza mifumo Simba ya kumtegemea yeye siku akifa au kujitoa itakuwaje hapa naona unamsifia abrahamovich kwake hujafikiria akifa au kuikacha Chelsea itakuwaje ila kwa Mo umefikiria maskiniiii roho mbaya tu.
.
Timu yako haina hadhi ya kupambana na Simba tena
 
Endeleza mipasho wewe. Hivi Katumbi ni mwekezaji mazembe au mmiliki? Unamlinganisha Mazembe na huo upuuzi wenu? Mwenye hisa 49% ndio mwenye nguvu, what a joke!! Nikutoe tongotongo ewe mkia, Kaumbi ni mwekezaji. Ndio Yanga inaweza kuwa nyuma kwa sasa lakini elewa model wanayokuja nayo ni nzuri zaidi kuliko mlivyokurupuka ninyi mikia. Mo juzi tu alikaribia kususa mlianza kulialia hapa. Halafu umlinganishe na Katumbi!!

Haya tueleze Simba imeweka shilingi ngapi kwenye huo uwekezaji wa 51% kwa 49%?
Hivi nyie tatizo lenu ni nini?
Mpaka sasa Mo dewji hajaweka zile billion 20 kwenye account ya Simba kwa kuwa mfumo bado haujaanza kufanya kazi nyinyi vyura mnahisi unafanya kazi tayari poleni
 
Nimesoma comments zotee nilivyofika hapa nikacheka sasa wewe unabisha nini?
.
Huko mwanzo umesema Mo anatengeneza mifumo Simba ya kumtegemea yeye siku akifa au kujitoa itakuwaje hapa naona unamsifia abrahamovich kwake hujafikiria akifa au kuikacha Chelsea itakuwaje ila kwa Mo umefikiria maskiniiii roho mbaya tu.
.
Timu yako haina hadhi ya kupambana na Simba tena
Mkuu njia za utafutaji wa masikini zikigonga mwamba na asiporizika na hali yake anaamua kuwa Mchawi au mwizi.
Hawa wenzetu wamechagua Uchawi.
 
Simba haina mwanachama tajiri mmoja tu wapo wengi sanaa, yani unazungumza vitu vya kizamani sana (zilipendwa) kama sio mtu wa mpira bwana.
.
Roman abrahamovich anaimiliki Klabu ya Chelsea siki akifa na klabu nayo itakufa au itashuka daraja?
Moise Katumbi siku akiondoka Tp mazembe unadhani itaacha kuwa timu tishio Africa? Come on
Tatizo mnashindwa kutofautisha kati ya kina Abraimovich, katumbi, wao ni wamiliki wa timu hata wakifa timu zitabaki chini ya utawala wa familia zao, Mo sio mmiliki wa timu ya simba kama alivo mzee Bakhressa kwa azam kwanini hii tofauti hamtaki kuikubali, hao matajiri wengine wa simba miaka ile yanga anachukua ubingwa mara tatu mfululizo au kabla ya Mo walikua wapi?

Abromovich na Katumbi wao ndio wamiliki wa timu wakiamua wanaamua kuuza hisa kwa asilimia kadhaa kwa watu wenye interest lakini Mo yeye hisa zake kauziwa na simba tena itakua hio 49% kama alivosema Mwakyembe sasa unapolinganisha Abraimovich /Katumbi na Mo nakuona wa ajabu

Abramovich muda wowote akiamua kuiuza chelsea anaweza, familia ya Glazzer ikiamua.kuiuza Man utd inaweza, Mmiliki wa newcastle alitaka kuiuza newcastle kwa ndugu yake Sheikh Mansoor bahati mbaya business ikakwama, sasa kama hawa watu wanafanana na Mo katika umiliki je Mo anaweza kuiuza simba?
 
Hapa ndo utajua nani mbumbumbu Kati ya Vyura FC aka Yeboyebo na Simba Dume!
 
Nimesoma comments zotee nilivyofika hapa nikacheka sasa wewe unabisha nini?
.
Huko mwanzo umesema Mo anatengeneza mifumo Simba ya kumtegemea yeye siku akifa au kujitoa itakuwaje hapa naona unamsifia abrahamovich kwake hujafikiria akifa au kuikacha Chelsea itakuwaje ila kwa Mo umefikiria maskiniiii roho mbaya tu.
.
Timu yako haina hadhi ya kupambana na Simba tena
Hio comment ya Mo kutengeneza mfumo wa simba kuitegemea yeye sijaisema mimi kuna mtu kaisema na nika i like na kuiunga mkono kwa sababu ukiangalia kwa jicho la tatu kuna ukweli ndani yake sisi hatuna roho mbaya na simba wengi tulichopinga hapa ni simba kutuponda na kuona ni kama sisi ni wajinga fulani wakati wote tunafanana kwa kila kitu na tumetofautishwa na tofauti ndogo tu nyie mna mtu Mo Dewji lakini yanga hawana huyo mtu ndio maana nikasema kua siku simba nayo ikikosa mtu kama Mo Dewji lazima mtayumba tu kama yanga huenda wakaja watu wengine lakini kupata watu wenye support kama ya Mo kwa kiwango kilekile ni ngumu sana (sio kwamba haiwezekani) inawezekana lakini ni ngumu sana, ukitaka kuanza kunielewa jiulize kabla ya Mo hao watu walikua wapi, Mo mwenyewe aliwahi kusema kwa waandishi wa habari kua anafanya hivyo simba kwa sababu ya mapenzi makubwa aliyokua nayo kwa simba maana klabu inajiendesha kwa hasara na hizo bilion 20 (sijui kama amaezitoa ama laah) angeweza hata kununua timu ya mpira daraja la chini huko Marekani lakini hataki hivo anataka kuitengeneza simba imara
 
Mo
Hakuna mtu anaye jitambua anayeweza kuja kuwekeza kwenye timu ya watu wasio jielewa kama yanga.
Tegemeo lenu lilikuwa ni R.Azizi na mwenyewe akachomoa.
amewekeza kitu gani Yanga,rostam atawekeza ni mmoja kati ya wawekezaji 4 walio tayari,rostam,gsm,sayona na riz1,subirini somo kutoka kwetu muone namna uwekezaji unavyokua,sio ule usanii wa friends of mikia
 
Mo

amewekeza kitu gani Yanga,rostam atawekeza ni mmoja kati ya wawekezaji 4 walio tayari,rostam,gsm,sayona na riz1,subirini somo kutoka kwetu muone namna uwekezaji unavyokua,sio ule usanii wa friends of mikia
Haaaa ngoja tusubiri tuone huo uwekezaji.
 
Huoni aibu wewe kumuita Ali Mayai mamluki???Huwezi kufikia hata kidogo alichoifanyia Yanga.Sidhani hata kama wewe ni mwanachama wa Yanga.Tabu ya wapenzi maandazi kama wewe mkiambiwa ukweli kwenye hizi timu mbili mnakimblia kumuita aliyesema ukweli mamluki badala ya kujibu hoja kwa hoja.
Vyura wa juzi hao!achana nao mkuu
 
Back
Top Bottom