Yanga inatakiwa iache kushiriki kwa kukariri


Mkuu sijui unachanganya vp mambo? Ngoja nikupe mfano halisi Katumbi pale Mazembe ana hisa 60%,Narudia ana hisa 60%. Katumbi hamiliki Mazembe 100% kuna wamiliki wengine pia. Katumbi akiamua anauza hisa zake. Timu zina endeshwa na mwenye major shares ila zinamilikiwa na wengi ndio maana kuna board of trustee's inazisimamia.

Simba ndio imeingia kwa mara ya kwanza kwenye mfumo huu wa Uendeshaji lazima kwa mara ya kwanza Hisa uuziwe na club moja kwa moja. Mfano hivi karibuni Voda waliuza hisa zao DSE zilipoisha ukitaka hisa unanunua kwa watu walionunua mwanzo. Yes Mo anaweza Kuiuza Simba (49% shares) akiamua, concept ni ile ile tu.
 
Yanga haifanani na Simba kwa kila kitu, Yanga ni timu hoyahoya inayojiendesha kwa michango ya watu mbalimbali na kutegemea mapato ya milangoni.
.
Mnacheza michezo ya kirafiki Moshi na Arusha mengine mmekwishacheza Zanzibar zote zilikuwa fund raising tu na wala si kutafuta muunganiko wa timu.
.
Kingine Simba kwa sasa ni timu ya daraja la juu Yanga si timu ya daraja la juu, Yanga haina pesa Simba ina pesa, kulingana na club licensing Simba inakwenda kukidhi vigezo vyote kwa maana ya kuwa na viwanja vyake, timu za vijana zinazojitegemea n.k.
.
Mo dewji hatengenezi misingi ya timu kumtegemea yeye kama mtu anatengeneza misingi ya timu kujiendesha kisasa hata leo hii akitoka (kitu ambacho mnatamani kitokee) atakuja mwingine tu he'll invest more than Mo did kwa sababu kuna faida
.

B20 bado hajazitoa na hajazitoa kwa sababu bado mfumo haujaanza kufanya kazi japo nyie mnaona unafanya kazi, Mo alisema anafanya kwa mapenzi yes kwa sababu yeye ni mwanachama wa Simba ukiacha wadhifa alionao sasa ulitaka afanye kwa mapenzi ya Yanga?
 
Timu ilikuwa na urasimu mkubwa sanaaa viongozi walikuwa wanapiga hela usijifanye hujui kina aveva na wenzao unajua waliko.
.
Umesema kina Abrahamovich hata wakifa timu zitabaki chini ya familia zao unadhani Mo hana familia watu wenye uwezo mkubwa kama yeye unamjua Fateema Dewji? Wanaweza kwa sababu Simba ni fursa kuna pesa iko pale.
.
Hahaha, Mo ni mwanachama wa Simba sports club anaweza akafanya uhuni wowote ila kwa kuwa anaipenda club hawezi kufanya lolote.
.
Anaweza akafanya hivi, ana hisa 49% akaamua kuzimilikisha kwa kampuni yake yoyote kisha kwenye zile 50% akanunua pia! Akaimiliki club kwa namna hii.
.
Abramovich Chelsea hamiliki kila kitu kuna wamiliki wa uwanja n.k ambao ni wengine, Katumbi hamiliki Tp mazembe yeye peke yake.

Abramovich akaiamua kuiuza chelsea anaweza, Grazers hawawezi kuiuza Manchester united japo wanamiliki 98% ya hisa zote hii klabu bado ni ya wanachama ndio maana kuna membership cards za Man united watapata wakati mgumu.
 
Reactions: RTI
Concept ni ile ile ila themes ni tofauti Abramovich kainunua chelsea kutoka kwa Ken Bates kwa £60 million (hajauziwa hisa kama Mo) Sheikh Mansour kainunua Man city mwaka 2008 kwa £210 million (hajanunua hisa kanunua timu) wenzetu mifumo yao ya soccer ina waruhusu kufanya hivyo ndio maana nikasema kuna tofuati kati ya aina ya umiliki wao na Mo mfano chelsea Abramovich ndiye mtu mwenye maamuzi ya mwisho akiamua kufukuza kocha anafukuza anytime lakini Mo ni kwa simba hawezi kua muamuzi wa mwisho waamuzi wa mwisho ni wanachama wenye 51%

Labda haukumsikiliza Mwakyembe au kama ulimsikiliza basi haukumuelewa alisema Simba na Yanga ni timu za wanachama hivyo hatuwezi kuruhusu mtu mmoja akawa na uwezo wa kutoa maamuzi kwenye club au akawa na sauti kuliko wanachama ndio maana akasema muwekezaji iwe mtu binafsi au makampuni yeye atachukua 49% na wanachama 51%
Mfumo huu wame u copy kutoka ligi ya Ujerumani Bundersiliga (kwa Bourssia Dortmund sina uhakika 100% kwa timu zote ila nadhani ni mfumo wa timu nyingi niliwahi kusikia clouds kua ni kwa timu zote)

Sasa ukimfananisha Mo na Hao kina Sheikh Mansour, Abramovich, Glazer hata mzee wetu Bhakressa unakua unakosea sana na hapa ndipo hoja yangu ilipo, mfumo mzima unaweza kua sawa kwa kufanana lakini katika ku function hauwezi kua sawa, Abramovich akiamua kuiuza chelsea kama timu sio kuuza hisa zake anaweza ila Mo hawezi kuiuza simba kama timu ila anaweza kuuza hisa zake 49% kwa mtu mwingine na zile 51% za umiliki zinakuepo mikononi mwa wanachama wa simba, nadhani mkimuita Mo muwekezaji kama mnavyomuita ni sahihi zaidi kuliko kusema mmiliki, hata siku moja mmiliki wa kitu hawezi kuzidiwa hisa katika umiliki wake.

Pia unasema kwa kua huu mfumo simba ni mara ya kwanza ndio maana Mo kauziwa hisa na timu ya simba hii ndio tofauti sasa kati yake na hao wengine ,, kina Abramovich na kina Mansour wao wamenunua timu nzima hawajanunua hisa wala kuuziwa hisa na chelsea au man city ndio maana Abramovich alipoinunua chelsea akaishape mwenyewe kwa jinsi anavyotaka akamleta Mourinho na mabadiliko mengine anayotaka yeye the same thing kwa Mansour

Nahitimisha mkuu kama huoni tofauti kati ya Mo na hawa watu katika mifumo njoo katika utendaji na power of decision making, Mo ni just kama investor na sio owner anamiliki hisa ila hamiliki club hao wengine wanamiliki club, Chelsea japo wanatumia uwanja wa mashabiki wake (kama sikosei) ila ile sio timu ya wanachama kama ilivyo dortmund au simba na yanga the same thing to Man city mtu kama Glazer (amefariki tayari) anaimiliki Man utd kwa zaidi ya 90%+ unadhani hizo asilimia 10 hawezi kuzichukua akitaka, jibu ni anaweza ila anazigawa au anaziuza kwa watu au mashabiki ili nao wawe sehemu ya timu lakini sio kwamba hizo 10% zitamzuia kuiuza timu hapana ndio maana yule mwana mfalme arabuni huko alipotaka kuinunua Man utd familia ya Glazer ilikataa kwa kusema hawapo tayari kuiuza Man utd sababu bado wangependa kubaki nayo, na sio sababu ya hio membership ya 10% membership ni njia tu ya kufanya watu wawe karibu na timu na wachangie timu zao kwa kulipia kadi na kununua au kupewa vitu vya timu lakini kwetu huku membership si sehemu ya wamiliki wa timu bali ndio wenye timu, hasa hizi zetu simba na yanga

Kama hutaielewa point yangu na hapa basi sidhani kama nitahangaika kuja kujibu tena hiki kitu wakati utofauti huu unajionyesha wazi kabisa kua simba na yanga ni timu za wanachama sasa Mo kutoa tu pesa keshakua miaka hii miwili mmiliki tayari, Mo ni sehemu ya umiliki wa simba ila sio mmiliki (owner) ila wamiliki ni wanachama wenye hisa 51%
 
Anaweza akafanya hivi, ana hisa 49% akaamua kuzimilikisha kwa kampuni yake yoyote kisha kwenye zile 50% akanunua pia! Akaimiliki club kwa namna hii.

Mkuu umeandika vizuri sana ila hapo [emoji115] juu umetunywesha chai bila kitafunio [emoji23] unadhani hisa wananunua ni kama tu mtu unavyonunua boxer hapana hisa zinauzwa kwa mifumo maalumu hicho kitu ulichokiandika hapo ni uongo 100% kwa mfumo wa mpira wetu hakiwezekani labda kwa nchi nyingine ila sio Tz

Kwanini haiwezekani tayari nishaeleza kwenye comment nyingine, Kupitia waziri wa michezo ni kwamba simba na yanga ni mali ya wanachama hivyo asilimia 51% za hisa ni lazima zimilikiwe na wanachama then 49% atapewa mtu au kampuni yoyote hata wewe kama ukiwa na uwezo wa ku negotiate na mkaelewana, kitendo tu cha huu mfumo ku exist hapa kwetu tayari kishamnyima Mo au muwekezaji yoyote kua mmiliki wa timu ila kinamruhusu tu kua sehemu ya umiliki wa timu.

Pia narudia tena hakuna mahala sisi tumepinga hii aina ya uendeshaji wenu maana ni kweli wapigaji walikua wengi sana kabla ya aina hii ya uendeshaji kuanza kutumika, vilevile pia hakuna mahali nimesema kua nimetaka Mo aje awekeze yanga labda ulinielewa vibaya au emotion zako zilikutuma useme hivyo

Kina Abramovich kina Mansour hata wakifa timu zao chelsea na man city zitabaki mikononi mwa familia zao kwa sababu wao sio sehemu ya wamiliki wa timu kama Mo kwa simba, ila zitabaki kwa familia zao kwa sababu wao ndio wenye timu, wao hawamiliki hisa kama Mo wao wanamiliki timu zenyewe halafu ndio wataamua kama wauze hizo hisa au wabaki individual wao kama wao

Sasa unavosema kwani wanafamilia wa Mo hawapo nakushangaa kwa sababu mfumo tayari ushamnyima Mo sifa ya kua mmiliki (ila ni sehemu ya umiliki) hivyo mfano Mo akifariki hisa zake 49% kama atakua hajaziuza basi zitabaki kwa familia yake na familia yake haitakua wamiliki wa simba bali itakua sehemu ya wamiliki, nadhan mpaka hapo utakua umeona tofauti kati ya aina ya umiliki kwa familia za kina Abramovich, Mansour na itakavyokua kwa familia ya Mo

Kama lengo ni kuelewa nadhani hapa hata mtoto wa form one ataelewa lakini kama lengo ni kubishana huwezi kuelewa, niongeze mfano mwingine mdogo Mo alikua anataka hati ya simba kutoka kwa Mzee Kilomoni, toka lini mmiliki wa kitu ukawa hauna hati miliki ya kile unachokimiliki

Kama hautanielewa na hapa basi sitarudia tena kuandika au kujibu kitu ambacho kipo wazi

Nahitimisha kwa kusema

Wenzetu mifumo yao inawaruhusu kumiliki timu individual kwetu kwa Simba na Yanga mfumo huo serikali imeukataa ndio maana umiliki upo kwa wanachama ambao watakua na 51% ya umiliki na 49% kwa wawekezaji hivyo unavomfananisha Mo na kina Abramovich binafsi nabaki nakushangaa sana maana wao hawabanwi na mfumo wowote ila huku Mo huu mfumo wa 49% tayari ushambana na yeye mwenyewe Mo baada ya watu wa simba kulalamika wakati Mwakyembe kasema hivo, Mo mwenyewe alisema mfumo huo aliosema waziri ndio mfumo wetu na upo kutoka zamani hivyo watu watulie.
 
Jadili mada kuu
 
Mo mwenyewe ali tweet halafu leo mtu kutoka linguse nguse unataka useme Mo ni mmiliki wa simba, na siandiki haya sababu ya wivu hapana ila naandika haya kwa sababu ndio hoja ambayo tuna i jadili tu
 
Jadili mada kuu
Hii maada nishaijadili kutoka juu nimeiita upuuzi kama hukuona huko juu basi ni uvivu wako wa kusoma hii maada imetufikisha kwenye mjadala wa Mo kufananishwa na kina Abramovich jambo ambalo nimelipinga na ninaliita upuuzi kama nilivyoiita hii maada upuuzi
 
Yanga imezidiwa na Simba kila kitu kwa sasa kuanzia fedha, hamasa za wapenzi hadi wanachama, wachezaji wakali wenye viwango bora.
.
Morali ya timu kutaka kufanya vizuri, malengo ya klabu ya Simba ni makubwa mara elfu 1 kuliko ya Yanga timu ina malengo ya kufika Semifinals msimu huu CAF champions league yenu ina malengo gani?
.
Huu ndio unapaswa kuwa mjadala twende kazi
 
Hili ndio tatizo lenu watu wa mkia fc mnatuchokonoa sana mnalazimisha tuwape heshima yetu na kuwakubali kwa lazima mna force sana tuwa appreciate jambo ambalo ni impossible, mkifanya vizuri tutawapongeza napo tukitaka au tukiamua sisi wenyewe na sio kulazimishwa
Ukitaka tuijadili hii mada fungua uzi wako then wachangiaji wengi watakuja na mimi mwenyewe nikiiona nitakuja kuchangia kwa hiari yangu mwenyewe pasi kulazimishwa wala kushurutishwa na mtu yoyote kama ulivofanya wewe hapa
 
Wajinga wameigawa timu kwa wajanja, ujinga mzigo. Namkumbuka zuzu aliyeuza almasi kwa pipi
 
Hivi nyie tatizo lenu ni nini?
Mpaka sasa Mo dewji hajaweka zile billion 20 kwenye account ya Simba kwa kuwa mfumo bado haujaanza kufanya kazi nyinyi vyura mnahisi unafanya kazi tayari poleni
Kwa hiyo unatumia mfumo gani kwa sasa? Mambumbumbu fc
 
Wajinga wameigawa timu kwa wajanja, ujinga mzigo. Namkumbuka zuzu aliyeuza almasi kwa pipi
Tumeigawa alafu tumefika robo fainali caf champion league na tumechukua ubingwa ligi kuu tanzania msimu huu na wachezaji hawajagoma sababu ya kukosa mishahara na tunajenga uwanja wetu bunju nyasi bandia na natural ground...haya ni mafanikio ya mwaka mmoja tu ya wajinga wlioigawa timu yao kwa wajanja ,werevu naona timu lenu bovu linafungwafungwa tu,njaa kali mpaka wachezaji wanagoma...timu mpaka liitishe harambee na kutembeza bakuli ndo linalipa mishahara...TUTAELEWANA TU
 
Teh teh wanakuja na Mfumo wao ambao haupo duniani.

Kutakuwa na wawekezaji na bado club itabaki ya wanachama.
 
Teh teh wanakuja na Mfumo wao ambao haupo duniani.

Kutakuwa na wawekezaji na bado club itabaki ya wanachama.
Wawekezaji vs mwekezaji, the difference is clear now!! Long live monsieur Kilomoni
 
Hahaha we jamaa vipi hii ndio mada ya uzi huu kuwa Simba ni bora kuliko mbute imezidi kila kitu, mashabiki, hamasa, viwango bora vya ndani ya uwanja na nje ya uwanja.
.
Tumewazidi hadi kuwa na msemaji mwenye ushawishi na bora zaidi na huu uzi haya maneno ni ya Ally mayai tembele mchezaji wa zamani na mwanachama wa yanga ww una hata kadi?
 
Hayo maneno ya mropokaji manara wa mambumbumbu fc. Umewahi sikia timu yenye mfumo mzuri ina mzee wa mipasho mwimba taarabu? Tulikuwa huko tukatoka ujingani. Msemaji wa klabu ni kocha. Endeleeni na mipasho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…