Timu ilikuwa na urasimu mkubwa sanaaa viongozi walikuwa wanapiga hela usijifanye hujui kina aveva na wenzao unajua waliko.
.
Umesema kina Abrahamovich hata wakifa timu zitabaki chini ya familia zao unadhani Mo hana familia watu wenye uwezo mkubwa kama yeye unamjua Fateema Dewji? Wanaweza kwa sababu Simba ni fursa kuna pesa iko pale.
.
Hahaha, Mo ni mwanachama wa Simba sports club anaweza akafanya uhuni wowote ila kwa kuwa anaipenda club hawezi kufanya lolote.
.
Anaweza akafanya hivi, ana hisa 49% akaamua kuzimilikisha kwa kampuni yake yoyote kisha kwenye zile 50% akanunua pia! Akaimiliki club kwa namna hii.
.
Abramovich Chelsea hamiliki kila kitu kuna wamiliki wa uwanja n.k ambao ni wengine, Katumbi hamiliki Tp mazembe yeye peke yake.
Abramovich akaiamua kuiuza chelsea anaweza, Grazers hawawezi kuiuza Manchester united japo wanamiliki 98% ya hisa zote hii klabu bado ni ya wanachama ndio maana kuna membership cards za Man united watapata wakati mgumu.
Anaweza akafanya hivi, ana hisa 49% akaamua kuzimilikisha kwa kampuni yake yoyote kisha kwenye zile 50% akanunua pia! Akaimiliki club kwa namna hii.
Mkuu umeandika vizuri sana ila hapo [emoji115] juu umetunywesha chai bila kitafunio [emoji23] unadhani hisa wananunua ni kama tu mtu unavyonunua boxer hapana hisa zinauzwa kwa mifumo maalumu hicho kitu ulichokiandika hapo ni uongo 100% kwa mfumo wa mpira wetu hakiwezekani labda kwa nchi nyingine ila sio Tz
Kwanini haiwezekani tayari nishaeleza kwenye comment nyingine, Kupitia waziri wa michezo ni kwamba simba na yanga ni mali ya wanachama hivyo asilimia 51% za hisa ni lazima zimilikiwe na wanachama then 49% atapewa mtu au kampuni yoyote hata wewe kama ukiwa na uwezo wa ku negotiate na mkaelewana, kitendo tu cha huu mfumo ku exist hapa kwetu tayari kishamnyima Mo au muwekezaji yoyote kua mmiliki wa timu ila kinamruhusu tu kua sehemu ya umiliki wa timu.
Pia narudia tena hakuna mahala sisi tumepinga hii aina ya uendeshaji wenu maana ni kweli wapigaji walikua wengi sana kabla ya aina hii ya uendeshaji kuanza kutumika, vilevile pia hakuna mahali nimesema kua nimetaka Mo aje awekeze yanga labda ulinielewa vibaya au emotion zako zilikutuma useme hivyo
Kina Abramovich kina Mansour hata wakifa timu zao chelsea na man city zitabaki mikononi mwa familia zao kwa sababu wao sio sehemu ya wamiliki wa timu kama Mo kwa simba, ila zitabaki kwa familia zao kwa sababu wao ndio wenye timu, wao hawamiliki hisa kama Mo wao wanamiliki timu zenyewe halafu ndio wataamua kama wauze hizo hisa au wabaki individual wao kama wao
Sasa unavosema kwani wanafamilia wa Mo hawapo nakushangaa kwa sababu mfumo tayari ushamnyima Mo sifa ya kua mmiliki (ila ni sehemu ya umiliki) hivyo mfano Mo akifariki hisa zake 49% kama atakua hajaziuza basi zitabaki kwa familia yake na familia yake haitakua wamiliki wa simba bali itakua sehemu ya wamiliki, nadhan mpaka hapo utakua umeona tofauti kati ya aina ya umiliki kwa familia za kina Abramovich, Mansour na itakavyokua kwa familia ya Mo
Kama lengo ni kuelewa nadhani hapa hata mtoto wa form one ataelewa lakini kama lengo ni kubishana huwezi kuelewa, niongeze mfano mwingine mdogo Mo alikua anataka hati ya simba kutoka kwa Mzee Kilomoni, toka lini mmiliki wa kitu ukawa hauna hati miliki ya kile unachokimiliki
Kama hautanielewa na hapa basi sitarudia tena kuandika au kujibu kitu ambacho kipo wazi
Nahitimisha kwa kusema
Wenzetu mifumo yao inawaruhusu kumiliki timu individual kwetu kwa Simba na Yanga mfumo huo serikali imeukataa ndio maana umiliki upo kwa wanachama ambao watakua na 51% ya umiliki na 49% kwa wawekezaji hivyo unavomfananisha Mo na kina Abramovich binafsi nabaki nakushangaa sana maana wao hawabanwi na mfumo wowote ila huku Mo huu mfumo wa 49% tayari ushambana na yeye mwenyewe Mo baada ya watu wa simba kulalamika wakati Mwakyembe kasema hivo, Mo mwenyewe alisema mfumo huo aliosema waziri ndio mfumo wetu na upo kutoka zamani hivyo watu watulie.