Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Napenda niseme tu bila kupepesa macho ya kuwa yanga wanayo nafasi kubwa ya kutinga hatua ya makundi klabu bingwa msimu huu.
Nimepata ujasiri wa kusema hivyo baada ya kuwaona Al hilal iliyocheza na simba, ni timu ya kawaida ambayo kwa jicho la kiufundi nimeona bado inatafuta muunganiko baada ya kusajili wachezaji wengi wapya.
Bado timu yao inanufaika na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na sio timu kucheza kitimu zaidi, hii ni timu ambayo nilikuwa naona itaipa yanga changamoto kubwa sana lakini kwa namna nilivyowaona jana yanga wakichanga karata zao vizuri kianzia mechi ya nyumbani nawaona wakiwaondosha matajiri hawa mapema sana, labda kama watabadilika haraka vinginevyo yanga nawaona wakitoboa na kusonga mbele.
Pia naiona mechi yao na St george ikiwa ngumu kwa aina ya mchezo ambao timu zote zinacheza, Yanga watanufaika na muunganiko wa kikosi chao ambacho imekaa pamoja kwa muda mrefu huku wakiongeza quality chache sana kwenye kikosi.
Wakati al hilal wanaanzisha takribani wachezaji 6 wapya kwenye kikosi chao cha kwanza yanga wao wanaweza kumuanzisha Aziz ki peke yake kwenye kikosi cha kwanza, kilichopo yanga wajipange kimbinu zaidi toka kwa Profesa Nabi kuimaliza mechi kwa mkapa