Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Wakati benchi la ufundi likijipanga kupata Ushindi, VIGOGO na matajiri wa klabu ya Yanga nao hawalali wakiendelea na mipango ya nje na sasa wachezaji wa timu hiyo wamewekewa mzigo wa Sh 500milioni mezani kama njia ya kuongeza mzuka wa kupata ushindi mbele ya Mazembe.
Matajiri na vigogo hao wamewatamkia mastaa wa Yanga milioni mia tano katika kuwapandisha mzuka ili wakausake ushindi kesho Kwa Mkapa, baada ya kutofurahishwa na kipigo cha mchezo wa kwanza wa nyumbani dhidi ya Al Hilal uliowatibulia hesabu mapema kabla ya kupoteza tena ugenini kwa MC Alger.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo, amesema uongozi wa klabu hiyo unaridhishwa na maendeleo ya mabadiliko ya kikosi chao na sasa wanasubiri kuona timu yao inapata ushindi wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa chini ya Ramovic.