Kwanza poleni sana mashabiki wa nyuma mwiko kwa kipigo ilikuwa ni suala la muda TU, mmebebwa vya kutosha Leo ilikuwa hakuna namna mmegongwa!!
Kadi ya Khalid Aucho ( ya njano ) aliyopata Leo ni wazi mechi ijayo hatocheza.....bila kupepesa huyu ni mchezaji muhimu sana kwenye timu yenu pengine kuliko mchezaji yoyote ni pengo( kama unabisha, muulize gamondi, usiporidhika na majibu panda ndege mfuate nabi sauzi atakupa majibu )
Msingi wa hoja yangu ni kuwa huenda mechi ijayo yanga akapelekewa moto vilevile na ikawa mechi ngumu zaidi.....kwann??
1..pressure kubwa kwa wachezaji baada ya kupoteza mechi Vs Azam ( hawajazoea )
2..kumkosa wachezaji muhimu ( Aucho na baka )
3...kuwaza mechi ya club bingwa Vs Al hilal Omdurman ya Sudan
4...fitness na fatigue ya wachezaji...mfano: mwamnyeto mechi ijayo huwezi muamini coz mda wowote anatoa Boko
5...mwisho na muhimu: nilishawahi kusema hapa jf kuwa gamondi ilikuwa suala la muda TU watu kuelewa mbinu zake mkanitukana Sanaa....Sasa mnadhani hizi Moja Moja ni bahati mbaya??? Shauri yenu
Alafu jinsi mlivyo hamna akili eti mnajipa moyo sijui " hatutaki kushinda nyingi, kimoja TU kwa yoyote".....bila kujua timu yenu inashuka kwa Kasi kubwa
Bila kusita najua kituo kinachofuata ni kocha kumla kichwa....na Mimi kama metronidazole 400mg natamani sana hili litokee shenzi!!!
Haya mkakojoe mlale
Unatumia hisia zako kujenga hoja na sio uhalisia, unachokiwaza wewe wenzako walishakifanyia kazi kwenye maandalizi ya msimu mpya, maandalizi ayo ni pamoja na usajili Bora kwa wachezaji wasiozidiana ubora Kila eneo, Leo hii yanga aiwezi kumkosa aucho alafu eti kocha akaumiza kichwa juu ya nani anaenda kucheza eneo ilo, yanga walishatoka uko kitambo ndio maana nakwambia unatumia hisia na ushabiki wako wa kuwa kolo kuwasilisha hoja mfu!
Khalid aucho alikosa mechi na mamelod lakini uliona pengo lake?
Itakuwaje kwa timu za hapa Tanzania Kuna timu yoyote Ina uwezo wa kupishana na yanga ata akicheza mkude au sure boy au abuya?
Upande wa baka bado yupo mwamnyeto na jobu Wana uwezo mzuri tu kucheza mechi yoyote iwe klabu bingwa ama mechi za ligi ivyo iyo hoja yako Haina mashiko imejifia kifo cha kawaida!
Suala la fitness na fatique umeshindwa kuliona kwenye mechi dhidi ya Azam utakuja kuliona kwenye mechi dhidi ya tabora united? Kabla ya kucheza na Azam yanga kasafiri kwenda kucheza Arusha na coast union karudi kaenda kucheza na singida Zanzibar kapumzika siku mbili kacheza na Azam kwaiyo mechi ngumu zaidi ya Azam ndio ulitakiwa uione fatique ya yanga lakini Mpira umeona Azam ndio alikuwa kama vile Yuko pungufu badala ya yanga!
Sasa timu inapumzika angalau siku 4 kabla ya kuvaana na Tabora united ndio unategemea fatique iwasumbue?
Hoja yako ya presha kubwa kwa wachezaji kwakuwa wamefungiwa na Azam usiifananishe yanga na timu ndogo bro, yanga inao wachezaji wakubwa ambao washacheza kwenye mazingira yoyote yale na wakapata matokeo aijalishi wanacheza na nani ivyo icho unachokitegemea kitokee umeshaferi mapema tafuta kingine!
Na cha mwisho yanga aijashuka kama unavyojiaminisha, kufungwa na Azam isiwe kichaka chako cha kufufukia hapo, timu iliyoshuka imepoteza mechi ngapi?