Yanga Kumsajili Mchezaji nyota wa timu kubwa, Bango lake kuwekwa kwenye Jengo linalotazamana na Timu hiyo

Ala kumbe Simba Kuna wachezaji nyota mpaka kuatamaniwa na utopolo? Maana mitopolo inatuaminisha hakuna mchezaji wa Simba anayeweza kusajiriwa kwao kwani itakuwa hasara, mana ni wazee au hawana viwango. Kweli wenye akili ni wawili na Sasa injia ni watatu maana anawaburuza anavotaka
Wapi imetajwa simba?
 
Wapi imetajwa simba?
Una ubishani wa kitoto sana, kwahiyo injinia ameiongelea lipuli ya iringa. Kama hujui chagizo za hizi club mbili kwenye kutengeneza content za kwenda viral kaa mbali na mpira wa bongo
 
Upuuzi tuu...bila,Simba hiyo utopolo haina content...
Mkuu Simba hii hii ambayo Kibu anawanyanyasa? Kiukweli imeniuma sana kuona hadi Kibu anawavimbia Simba......mmefika pabaya sana
 
Hivi ni mimi tu ninayeona au ni kama Yanga wanalazimisha sana undugu na Simba wakati hawana hata time nao.

Kila siku wanapiga kelele Simba ina wachezaji wabovu ila hao hao wabovu wanawatamani hadi kupanga kuwawekea mabango wakiwasajili.
Kwani wakilazimisha undugu kuna raia yeyote ni atakufa? Kama hamna basi acha waendelee tu
 
Una ubishani wa kitoto sana, kwahiyo injinia ameiongelea lipuli ya iringa. Kama hujui chagizo za hizi club mbili kwenye kutengeneza content za kwenda viral kaa mbali na mpira wa bongo
Sawa basi tutamsajili huyo mchezaji wa Simba ili acheze bolingo kama makudubela
 
Ala kumbe Simba Kuna wachezaji nyota mpaka kuatamaniwa na utopolo? Maana mitopolo inatuaminisha hakuna mchezaji wa Simba anayeweza kusajiriwa kwao kwani itakuwa hasara, mana ni wazee au hawana viwango. Kweli wenye akili ni wawili na Sasa injia ni watatu maana anawaburuza anavotaka
Waongo hao, nungunungu wamemtoa wapi?
 
Hivi ni mimi tu ninayeona au ni kama Yanga wanalazimisha sana undugu na Simba wakati hawana hata time nao.

Kila siku wanapiga kelele Simba ina wachezaji wabovu ila hao hao wabovu wanawatamani hadi kupanga kuwawekea mabango wakiwasajili.
Ni ww tu
 
Hapo Yanga kinachofanya ni kuwavuruga Simba,hata wale wachache wazuri kuwanunua ili tu Simba iwe mbovu zaidi,hilo ndo lengo lao.
 
Kutoka insta live ya ally Kamwe , Leo engineer HERSI ametupa wananchi breaking news ya moto [emoji28][emoji28]

Engineer HERSI amesema kuwa katika msimu huu wa usajili dirisha kubwa , Kuna mchezaji mmoja uyo fundi akisajiliwa , itatengenezwa bango kubwa lenye picha ya mchezaji huyo alafu litabandikwa opposite na jengo la timu moja hapa nchini[emoji28]

Yani kwenye moja ya jengo la timu Fulani, yanga itakodisha jengo linalo angaliana na jengo la timu hiyo alafu ilojengo liliokodiwa na yanga itabandikwa bango kubwa la mchezaji huyo, ili hiyo timu itakayo kuwa jirani apo Iwe inamuona ona kwenye picha
Na picha hiyo itaishi kwenye jengo Hilo Kwa muda wa miezi 6 [emoji91][emoji28][emoji28][emoji28]

Unadhani atakua mchezaji gani huyo na hiyo picha itawekwa jirani na jengo la timu gani?!!
#travellerwayanga
duh na mimi nilimsikia
 
Back
Top Bottom