Yanga kwa sasa inafaidika nini na kumng'ang'ania Feitoto?

Yanga kwa sasa inafaidika nini na kumng'ang'ania Feitoto?

Tangulini utopolo wakawa watu wa kufuata utaratibu na kuheshimu mikataba? Chukulia tuu ya sportpesa kwavile tarimba ni mwanachama la sivyo kesi ingekua mahakamani, angalia ile ishu ya morrison
Nb utopolo ni watu wa hovyo hovyo
 
Mijitu inabadili logo za watu kimakusudi kisa rangi ndio itaweza kuheshimu vipengele vya mkataba vya mchezaji?

Nb tff wanafanya wanayofanya ili kubalance wasionekane ni simba
 
Hili Jambo tukieleza Kisheria tunaonekana mashabiki wa Yanga. Lakini Hakuna popote duniani timu/Taasisi itaruhusu mchezaji/mwajiwake aache kazi anavyojisikia bila kufuata taratibu kisa tu kalipa hela ya kununuliwa au mshahara wa mwezi mmoja.
Mkuu toa mawazo yako pasipo kufikiria watu watakuonaje au kukuelewaje.

Kauli mbiu yetu ya JF ni "We dare to talk openly".

Kwahiyo unatakiwa ufunguke as much as you can.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria za boli zinambana Fei. Hapa utopoloni kwetu Yanga hatoshinda maana club ni kubwa kuliko mtu Hilo Fei hakujua sababu ya umri mdogo , majivuno, kiburi na kukosa vidato.

Nadhani Shangazi Fatma ni mzuri mno kwani English yake Huwa ni first class na anaijua Sheria ndani nje halafu Yuko smart sana upstairs , I propose yeye Fatma na mwanae Fei waende CAS au FIFA wataeleweka and watapata haki yao.

Mbona Msuva alishinda kesi na Wydad. Fei unakwama wapi?

Wanayanga tuna haki ya kujua ni nani aliempa Fei Ile millioni 100 ya kulipa. Kuna mganga kiboko wa kushughulikia vivuruge!
Scenario ya Msuva na Wydad ni tofauti na hii scenario ya Yanga na Fei Toto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawamng'ang'anii, ni mchezaji wao halali
Yanga wameshasema kwa sasa hawamuhitaji na hawana tena mpango wa kumtumia Feitoto kwenye kikosi chao, lakini bado ni mchezaji wao. Sasa wanapata faida ipi hapo?
 
Kwa hali ilivyo sasa na hili sakata lake, hata akirudi sidhani kama anaweza kuwa na ile hali ambayo mashabiki wamezoea kuiona
Ndio maana nauliza, nini mantiki ya Yanga kuendelea kumng'ang'ania mchezaji ambaye haihitajiki tena kwao?
 
Feisal ndio ana ing'ang'ania Yanga angekua na nia ya kuondoka mbona njia zipo wazi? mtu unalazimisha kupita dirishani wakati mlango upo then unasema umezuiliwa!
 
Huenda wanaogopa wakimuachia bila yeye kufuata taratibu basi wachezaji wengine pia wanaweza kuja kufanya hivyo,

So, hapo ni sawa na kuwa wanatuma msg kuwa taratibu lazima zifuatwe.

Wataalamu wataelezea zaidi, mimi mimeandika mawazo yangu tu.
Katika hali ya kawaida, suala la ufanisi wa timu linategemea mahusiano ya hiari yaliyopo baina ya Timu na mchezaji husika. Timu ikimchoka mchezaji itatafuta namna ya kumuacha mchezaji na mchezaji akiichoka timu atatafuta namna ya kuondoka, kwa namna yoyote ile hiyo hali lazima ifikiwe.
Feitoto haitaki tena Yanga......
Yanga haina tena mpango wa kumtumia Feitoto.....

Sasa Yanga wanamng'ang'ania mchezaji wa namna hiyo wa nini?
 
Aondoke katikati ya mkataba lakini pesa iwe ndefu.
Hao wanaomtaka wakitoa pesa ndefu. Yanga watamuachia tu, kwani Yanga hawahitaji pesa?
 
Feisal ndio ana ing'ang'ania Yanga angekua na nia ya kuondoka mbona njia zipo wazi? mtu unalazimisha kupita dirishani wakati mlango upo then unasema umezuiliwa!
Ni vipi tena useme Feitoto anaitaka Yanga wakati ameshaaga na hayupo hata kambini?
Kama mchezaji ameamua kuondoka bila kufuata utaratibu (ametoroka na hataki kurudi), suluhisho ni kuendelea kumng'ang'ania au kumfukuza kabisa?
 
Aondoke katikati ya mkataba lakini pesa iwe ndefu.
Hao wanaomtaka wakitoa pesa ndefu. Yanga watamuachia tu, kwani Yanga hawahitaji pesa?
Mkataba unatakiwa useme hivyo, mkataba wa Feitoto umesema Feitoto anatakiwa kulipa around 100m ili kuvunja mkataba wake (na amezilipa tayari), issue ambayo Yanga wanasimamia ni kuwa, utaratibu wa kufikia hapo haukufuatwa na Feitoto. Sasa suala lilllopo hapa ni kuwa, ni vipi Yanga wanafaidika na Feitoto kwa sasa?
 
Hujauona mkataba wa Fei waliuweka humu jf Wewe ulikuwa Bado unanyonya!

Mkataba niliusoma humu JF unasema Fei Anatakiwa akishalipa hizo pesa 100m za usajili na mishahara 3 kisha ataje na sababu "za maana" za kuvunja mkataba ambazo kiukweli Hana na hakutaja na mkataba unasema Yanga Wana haki kisheria ya kuzikubali au kuzikataa sababu za Fei-kubwa maana dogo keshaota mapembe ATI. Yaani hata angetaja sababu za kutoka mbinguni Yanga wangesema "Si za maana" na wangeshinda kesi , Fei msaidieni kwa kumwambia awalete warubuni wake Mezani walipe hiyo 1B wasepe nae , uhuni Huwa Hauna nafasi mbele ya sheria!

Wanayanga tutajiwe aliempa Feitoto Ile milioni 100 ni haki yetu in exchange with our coming to support our team pale Chamazi
Sababu za maana ndio zipi?
Huwa zinapimwaje?
Nani wa kuzipima hizo sababu kuwa zina maana ama la?

Swali linabakia pale pale, Yanga kwa sasa inafaidika nini na kuendelea kumng'ang'ania Feitoto?
 
Mijitu inabadili logo za watu kimakusudi kisa rangi ndio itaweza kuheshimu vipengele vya mkataba vya mchezaji?

Nb tff wanafanya wanayofanya ili kubalance wasionekane ni simba
Una uchungu sana ndugu
 
Ndio maana nauliza, nini mantiki ya Yanga kuendelea kumng'ang'ania mchezaji ambaye haihitajiki tena kwao?
Yanga ni taasisi mkuu.

Wanaendesha mambo yao kutokana na ethics na principles.

Ikitokea leo yanga wakalifanya swala la Fei toto kienyeji watajenga picha gani kwa mashabiki na wadau wengine wa michezo.

Ndio maana unaona kama Yanga wamekomaa vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vipi tena useme Feitoto anaitaka Yanga wakati ameshaaga na hayupo hata kambini?
Kama mchezaji ameamua kuondoka bila kufuata utaratibu (ametoroka na hataki kurudi), suluhisho ni kuendelea kumng'ang'ania au kumfukuza kabisa?
Aje mezani tuyamalize

Sent from my Infinix X689C using JamiiForums mobile app
 
Mkataba unatakiwa useme hivyo, mkataba wa Feitoto umesema Feitoto anatakiwa kulipa around 100m ili kuvunja mkataba wake (na amezilipa tayari), issue ambayo Yanga wanasimamia ni kuwa, utaratibu wa kufikia hapo haukufuatwa na Feitoto. Sasa suala lilllopo hapa ni kuwa, ni vipi Yanga wanafaidika na Feitoto kwa sasa?
Ukiambiwa kuvunja mkataba ni 100 millions, usichukulie kirahisi kuwa unawapa hiyo hela halafu unasepa.
Na mpira siyo ndoa au mahusiano ya kimapenzi.
Unasema huna mahaba, nani anajali mahaba yako? Mashabiki wanataka ucheze mpira, mhaba yako hayatuhusu sisi.
Just be professional.
Ila tu, kila kitu kina price yake, hata ukitaka kumuona waziri mkuu kesho and you have money, utamuona tu.
 
Ni vipi tena useme Feitoto anaitaka Yanga wakati ameshaaga na hayupo hata kambini?
Kama mchezaji ameamua kuondoka bila kufuata utaratibu (ametoroka na hataki kurudi), suluhisho ni kuendelea kumng'ang'ania au kumfukuza kabisa?
Hapo kwenye bila utaratibu ndio patakapo muumiza na ata umia kweli, mpka sasa Yanga hawana shida nae ila wanataka wamtie adabu
 
Back
Top Bottom