Yanga kwenda kucheza CAF champions Zanzibar, JKU na UHAMIAJI wamekataa kuchezea Zanzibar, Kuna nini?

Yanga kwenda kucheza CAF champions Zanzibar, JKU na UHAMIAJI wamekataa kuchezea Zanzibar, Kuna nini?

Wapi nimesema chimbuko la Yanga ni Zanzibar? Nilichosema kuwa Yanga pia ina wanachama Zanzibar. Njoo ukatae hapa kama Yanga haina wanachama huko Zanzibar. La pili njoo unioneshe ni wapi nilipoandika kuwa Yanga ina chimbuko Zanzibar, usitake kunilisha maneno nisiyoyasema MNAFIKI mkubwa wewe.
Nakiri hukusema hayo, lakini msikilize Ally Kamwe na wenzake wakiwa wamelewa supu ya pweza na maduriani.

Pale Zanzibar mpira wa miguu ni pahala kwake tangu kale, Kila mchezaji analo jina la mchezaji wa ulaya. Sio Yanga TU bali Kuna mashabiki na wanachama wa timu za ulaya pale pia. Hata Simba inao wanachama na mashabiki wengi pia, Liverpool na Manchester united hivyohivyo.

Kama tunaweza kutumia michezo kuimarisha umoja na udugu wetu ni jambo zuri sana.
 
Mechi ya ligi Azam vs Simba tarehe 26 inapigwa Zanzibar haya kaanzishe na uzi mwingine utoe mapovu
 
Mechi itakayofuata wataenda kuchezea katika sayari ya Mars

Ni suala la uamuzi tu na Uwezo

Ujue YANGA ni dude flani kuuubwa sana

Tunasubiri uulize swali lingine Kalpana
 
Mechi itakayofuata wataenda kuchezea katika sayari ya Mars

Ni suala la uamuzi tu na Uwezo

Ujue YANGA ni dude flani kuuubwa sana

Tunasubiri uulize swali lingine Kalpana
Ukweli utabaki palepale kuwa Yanga sio timu ya ZFF, kinachofanyika ni nia njema, mapenzi, hekima na uadilifu wa viongozi wetu wakuu wa nchi. Mechi hii imewaunganisha wa Zanzibar badala ya muda wote kufikiria siasa TU za CCM na ACT/CUF na bara na Zanzibar.
 
Timu za JKU na UHAMIAJI ni timu za Zanzibar kindaki ndaki kuliko Yanga. Hatukuelezwa kwanini JKU na UHAMIAJI hawakutaka mechi zao za mashindano ya CAF wachezee Zanzibar, lakini Yanga wanataka kwenda kucheza CAF championship mzunguuko wa pili Zanzibar. Kuna nini hasa hapo?

Ufafanuzi unahitajika juu ya jambo hili. Michezo ni furaha, uchumi na undugu, kwanini JKU na UHAMIAJI walihamisha furaha, uchumi na undugu unaotokana na michezo kwenda Egypt na Libya na Yanga kupeleka Zanzibar furaha, uchumi na undugu Zanzibar kutoka dar es salaam?

Je, unawaweza kuwa mkatoliki safi kumzidi Pope?; muislam fafi kuliko mufti?
Huku bara wanaogopa watatekwa, Kizimkazi kuko salama sana hamna matukio ya kihuni kama haya yanayofanywa na Mafwele
 
Umezuiwa kwa yanga pekee? Mbona simba anacheza pale?
Tuwaombe wenzetu turudishe Tena ligi kuwa moja, wenzetu ndio waliotukimbia na kuanzisha ligi yao na kutaka kuomba uwanachama wa FIFA. Hawataki kuitwa watanzania hata kidogo. Lakini watu wenye fikra kama hizo sio wengi sana pale Zanzibar na wanazidi kuzeeka na kufa. Jina la Tanzania limebeba majina ya Tanganyika na Zanzibar, haifai Tena kuita Tanzania bara na Tanzania Zanzibar.
 
Huku bara wanaogopa watatekwa, Kizimkazi kuko salama sana hamna matukio ya kihuni kama haya yanayofanywa na Mafwele
Yanga walipeleka mechi kule kienyeji TU kwa kutanguliza nia njema ya viongozi wetu wakuu wa nchi, lakini Yanga kupeleka Zanzibar mechi Kuna consequences kwenye mapato ya TRA, uwanja wa Mkapa, TFF, wafanyabiashara na wananchi wa Tanzania bara kwa ujumla. Kama Mtu akienda mahakamani kudai hili atakuwa na hoja yenye mashiko.
 
Utamsikia mtu kala bakuli la urojo na kusema Mama karume ni mwanzilishi wa yanga.
 
Timu za JKU na UHAMIAJI ni timu za Zanzibar kindaki ndaki kuliko Yanga. Hatukuelezwa kwanini JKU na UHAMIAJI hawakutaka mechi zao za mashindano ya CAF wachezee Zanzibar, lakini Yanga wanataka kwenda kucheza CAF championship mzunguuko wa pili Zanzibar. Kuna nini hasa hapo?

Ufafanuzi unahitajika juu ya jambo hili. Michezo ni furaha, uchumi na undugu, kwanini JKU na UHAMIAJI walihamisha furaha, uchumi na undugu unaotokana na michezo kwenda Egypt na Libya na Yanga kupeleka Zanzibar furaha, uchumi na undugu Zanzibar kutoka dar es salaam?

Je, unawaweza kuwa mkatoliki safi kumzidi Pope?; muislam fafi kuliko mufti?
hivi uhamiaji ni timu ya nchi gani? sijawahi sikia.
 
Utopolo Wameshaufanyia upembuzi yakinifu kuwa hata majini 70 yanaweza kukaa...mengine ya ziada wakayaweka kiembe samaki hapo...😀😀😀😀😁😁😁😁
 
Mechi ya ligi Azam vs Simba tarehe 26 inapigwa Zanzibar haya kaanzishe na uzi mwingine utoe mapovu
Nia sio mbaya, lengo ni watu wote wajue kuwa Zanzibar iko Tanzania na ni Tanzania, hivyo hakukua na haja ya kuwa na ligi mbili tofauti au vyama 2 vikuu vya mpira (TFF na ZFF), for what? Ingekuwa kuiboresha TFF ikawa na sura ya muungano baaasi na boli litembee. Siku zote na mara zote umoja ni nguvu. Badala yake ZFF wanazitaka timu za TFF kinyemela bila utaratibu unaoeleweka. Wanawakataa watoto wao (JKU na UHAMIAJI) kwa ugonjwa wa pale tu.

Na ni vizuri historia ya Simba na Yanga zikatunzwa na kusimiliwa vizuri kwa vizazi ambavyo havikuwepo. Mtu akisimama mbela ya kamera na kipaza sauti na kusema kuwa Yanga ina chimbuko lake Zanzibar au kusema Mama yetu na Baba yetu Mzee Karume ni mwanzilishi wa Yanga lazima tumjibu haraka ili historia isipindishwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi. Mchango uliotukuka wa familia ya Mzee Abeid Karume kwa Simba na Yanga lazima usimuliwe ili watu wajue kuwa majengo ya Kariakoo ya Simba na Yanga yana uhusiano na Mzee wetu huyu; Yanga walikuwa na kiwanja chao wakapata ufadhili wa kujengewa jengo lile kwenye kiwanja chao, lakini Simba hawakuwa na kiwanja lakini wakasaidiwa kununua jengo lao la club na Mzee wetu (RIP).

Kama upo Mchango wa Yanga na Simba katika siku za kuusaka uhuru wa Tanganyika na Zanzibar pia lazima usimuliwe kwa ufasaha na viongozi wa timu hizi kama upo. Na sio vibaya timu zetu hizi kupitia michezo zikatumika kuleta umoja wa watanzania na watanzania. Hata ule utani wao usiwe wa kupitiliza udugu na umoja.
 
Hao Uhamiaji na JKU kuhamisha mechi zao walipopangwa na waarabu wanajua wao nini kilichowasukuma kufanya hivyo. Lakini kikanuni uwanja wa Amani hauna changamoto yoyote kutumika katika mashindano ya CAF. Yanga hutumia uwanja wa Mkapa lakini kwasasa umezuiwa kutumika sababu ya kupisha ukarabati unaoendelea. Hivyo wana option ya kutumia uwanja wa Azam complex.

Kuamua kwenda Zanzibar kuchezea mechi yao, inaweza kuwa ni kutokana na uwepo wa mashabiki pia kwa idadi kubwa Zanzibar wanaoshabikia Yanga. Hata Zanzibar kuna shabiki wa Yanga pia
Zanzibar wanapenda mpira, walikuwa na vituo bora vya radio na television kabla ya Tanganyika. Walikuwa na uwanja Bora kabisa wenye taa za kucheza mechi usiku siku nyiingi kabla ya Tanganyika. Zanzibar ni ndogo lakini wametenga sehemu nyingi sana za wazi watoto kucheza. Zanzibar sio TU wanazipenda Simba na Yanga bali wanapenda timu inayotandaza ball watakwenda kuingalia kama sehemu ya starehe baada ya swala ya Insha.

Hata hivyo Yanga ni timu ya Kariakoo 100%, haina chimbuko Wala mwanzilishi Zanzibar bali ina uhusiano na Zanzibar kwakuwa mmoja miongoni mwa wafadhili wake alitokea Zanzibar na Zanzibar ni Tanzania, hivyo hakuna tatizo kabisa Yanga kwenda kucheza Zanzibar. Tatizo ni wale walioitoa Zanzibar kutoka TFF na kwenye ligi ya Tanzania na kuanzisha ZFF na ligi ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom