Yanga kwenda kucheza CAF champions Zanzibar, JKU na UHAMIAJI wamekataa kuchezea Zanzibar, Kuna nini?

Kumbe hoja yako ipo katika kiubaguzi wa utanganyika na uzanzibar.
mimi sio mbaguzi hata chembe moja. Dunia nzima sasa hivi inaungana kupata masoko ya pamoja, ulizi na fursa, mimi ni nani nisilione hilo?. Lakini hii hainizuii kusema ukweli ili ukweli utumike kuleta ummoja.

Wanasiasa ndio wanaotuchelewesha, sisi tuko Tayari kwa tanzania yetu

View: https://www.youtube.com/watch?v=QxKT7H_29Yo
 
Mazuri ya Tanganyika wazanzibar wanayataka, mpaka Sasa sijaona aliyejibu hoja kwanini timu za Zanzibar zikacheza mechi zao ugenini na yanga ikaenda Zanzibar .
Tra wakija kudai Kodi yao wasipige kelele wanaonewa.
Kikubwa ni kujipendekeza
 
TRA kudai kodi hakukwepeki hata wangecheza uwanja wa Mkapa, unataka watu wakujibu kwanini timu za Zanzibar zikacheze ugenini wakati hapakuwa na sababu za msingi? Uwanja umekidhi vigezo vya CAF na hakuna machafuko Zanzibar sasa unataka upewe zipi?
 
Yanga wameenda Zanzibar si Kwa sababu wanawanachama wengi kama baadhi ya watu wanavyoseme lakini ukweli wameenda Zanzibar ili kujipendekeza Kwa mheshimiwa rais.Huu ni ukichaa kabisa
Hii iko wazi.
 
Yanga inapocheza mechi pale Benjamin Mkapa niambie ni akina nani wanaopata gawio kwenye gate collections, na kwanini wanapata gawio? Je, Yanga inapopeleka mechi zake Zanzibar ni akina nani kati ya hao hawatapata sehemu ya gate collections na kwanini?

Yule mjumbe unaesema yumo ni kwasababu tu hati ya jengo ilikuwa kabatini kwake, la sivyo ondokeni tuchukue jengo letu..
Kwanini hati ikae kwa mtu wa Zanzibar kama timu haihusiani na watu wa Zanzibar?

Hao wanapata gawio kwasababu uwanja ni wa serikali na pia shirikisho husika ndio wanaosimamia mchezo husika.
 
TRA kudai kodi hakukwepeki hata wangecheza uwanja wa Mkapa, unataka watu wakujibu kwanini timu za Zanzibar zikacheze ugenini wakati hapakuwa na sababu za msingi? Uwanja umekidhi vigezo vya CAF na hakuna machafuko Zanzibar sasa unataka upewe zipi?
Timu za Uhamiaji na JKU kwenda kucheza meci zao huko ugenini Zanzibar imeingia hasara zipi na kiasi gani kwenye mapato (kodi ya serikali, mahoteli, wauza ubuyu, urojo, maji, ice-creams na sharwama, usafirishaji, utalii, fedha za kigeni) na kijamii (mtoko, starehe). na je, Yanga kupeleka mechi Zanzibar Tanzanzia imekosa nini (TRA, TFF, Uwanja, usafirishaji, mahoteli, wauza nyamachoma, bia, vyakula, jezi, utalii na nk). Faida hizi ndizo zinazosababisha kila mji na kila mkoa upambane kufa na kupona iwe na timu ya ligi kuu na timu iwekeze zaidi iweze kushika nafasi za juu ili ishiriki mashindano ya kimataifa kwakuwa wanazijua faida zake. Mlevi mmoja hawezi kupingana na hilo kwaababu zake dhaifu.
 
Kwanini hati ikae kwa mtu wa Zanzibar kama timu haihusiani na watu wa Zanzibar?

Hao wanapata gawio kwasababu uwanja ni wa serikali na pia shirikisho husika ndio wanaosimamia mchezo husika.
Yanga ina zaidi ya miaka 89 niambie ni lini mechi za Yanga ziliwahi kuhamishiwa Z'zibar? Zanzibar haikuwepo? Mzee karume hakuwepo? Hersi na wenzake ndio wanaojuwa chimbuko la Yanga?

Sio jambo baya Yanga kucheza Zanzibar lakini sio kiholela tu, lazima kuwe na hoja inayohitaji kujibiwa kwa kupeleka timu kucheza Zanzibar mechi zake kama vile kukosa uwanja, usalama au hali ya hewa, nk.

Kilichoniboa mm ni uhamiaji na JKU (taasisi za serikali) kupeleka mechi zao Misri n Lybia bila kutoa maelezo yanayoeleweka bila kujali faida nyingine za kucheza mechi kwenye uwanja wa nyumbani. Wamegoma kuutangaza uwanja wa New Amani stadium na kuiachaia Yanga ifanye kazi hiyo. Insane
 
Kwanini hati ikae kwa mtu wa Zanzibar kama timu haihusiani na watu wa Zanzibar?

Hao wanapata gawio kwasababu uwanja ni wa serikali na pia shirikisho husika ndio wanaosimamia mchezo husika.
Yaani mtu ikikusaidia kuleta zawadi ya jagi siku ya harusi ni sehemu ya familia yako au rafiki mzuri tu? Vipi kama siku Yanga ikihamishia makao yake Kigamboni na kuliacha jengo la Kariakoo? Kuna watu wanatoa misaada mikubwa kwenye taasisi lakini sio sehemu ya taasisi hizo.
 
hauna hoja, ila wapo watakaokuunga mkono.

Maelezo yako yameegemea ubara na Uzanzibari kisha ukristo na uislamu.

Unaweza ona mtoa mada ni mteja mzuri wa vibanda umiza kuliko kuangalia mpira akiwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ngoja nikufundishe, tena kaa kwa kutulia, kuna kipindi uefa walipendekeza baadhi ya mechi za uefa zichezwe nje ya ulaya kwenda kwenye nchi kama vile Marekani na Morocco, tp mazembe walicheza mechi za mashindano yaliyoratibiwa na FIFA hapa Tanzania, na mifano mingine mingi tu ipo.
Mwisho nikuweke sawa kuhusu kuwa na imani thabiti dhidi ya viongozi wa imani husika, kuwa pope/mufti hakumfanyi mtu kuwa bora zaidi kiimani kuliko wengine, imani ya mtu ni siri kati yake na mola wake, unaweza kuwa pope/muft na ukafanya machafu makubwa zaidi kuliko waumini wako.

Kama unaipenda Yanga ifuate unguja.
Umeenda mbali sana huko, katika zama hizi kuongelea udini, ukabila na ukanda ni kujirudisha nyuma sana kifikra. Hoja Yangu ilikuwa ni kwanini timu za ZFF hazikuona umuhimu wa kupromote uwanja New Amani, utalii, uchumi na furaha za wazanzibar badala yake wanataka timu ya TFF iifanye kazi hiyo, huku wakijua hata watu wa Dar es Salaam wangehitaji faida zote za timu yao kushiriki kwenye CAF champions? Michezo ni furaha na uchumi pia.
 
Timu za Uhamiaji na JKU kwenda kucheza meci zao huko ugenini Zanzibar imeingia hasara zipi na kiasi gani kwenye mapato (kodi ya serikali, mahoteli, wauza ubuyu, urojo, maji, ice-creams na sharwama, usafirishaji, utalii, fedha za kigeni) na kijamii (mtoko, starehe). na je, Yanga kupeleka mechi Zanzibar Tanzanzia imekosa nini (TRA, TFF, Uwanja, usafirishaji, mahoteli, wauza nyamachoma, bia, vyakula, jezi, utalii na nk). Faida hizi ndizo zinazosababisha kila mji na kila mkoa upambane kufa na kupona iwe na timu ya ligi kuu na timu iwekeze zaidi iweze kushika nafasi za juu ili ishiriki mashindano ya kimataifa kwakuwa wanazijua faida zake. Mlevi mmoja hawezi kupingana na hilo kwaababu zake dhaifu.
Kwa povu hili bila shaka wewe ni mchuuzi wa Yale mabarafu ya mochwari mnayoyapeki kwenye vifuko vya plastiki na kuwauzia watu Kwa Mkapa. Yanga wakukuharibi biashara Yako kesho. Usijali, washabiki wa Mnyama watafidia J'2
 
Wenye akili timamu wameelewa hoja, sema TU hata mm sina kinyongo na hili kama kwa kufanya hivi ni gundi imara ya muungano wetu. Yanga ilitumika sana kwenye harakati zetu mbalimbali sio vibaya ikiendelea na kazi yake iyo hata sasa.
 
Wewe ni mnafiki na unafiki ni mbaya sana.
 
Kaka wewe ndiye mnafiki uliyepitiliza. Kuna mtu anaendelea kusikika kuwa Yanga chimbuko lake ni Zanzibar na sauti hiyo inapazwa kwelikweli katika awamu hii ya Yanga. Huu ni uongozi unaofanana na ukweli. Timu hii imezaliwa 1935 wapi na akina nani? Wote tunamshukuru Mzee wetu Rais wa awamu ya Kwanza Zanzibar kwa "KUSAIDIA" Yanga kujenga jengo lile la Yanga, tunamshukuru wote kwa mapenzi yake kwa Yanga na Simba kutupa majengo, lakini majengo hayo hayakujengwa 1935 wakati Yanga inazaliwa Tanganyika. Kusema Yanga ina chimbuko lake Zanzibar ni kupotosha historia ya Yanga. Hata Mzee Nyerere aliikuta Yanga ipo na aliutumia kama ilivyo kwa mambo yake ya kisiasa.
 
Hao Uhamiaji na JKU kuhamisha mechi zao walipopangwa na waarabu wanajua wao nini kilichowasukuma kufanya hivyo. Lakini kikanuni uwanja wa Amani hauna changamoto yoyote kutumika katika mashindano ya CAF. Yanga hutumia uwanja wa Mkapa lakini kwasasa umezuiwa kutumika sababu ya kupisha ukarabati unaoendelea. Hivyo wana option ya kutumia uwanja wa Azam complex.

Kuamua kwenda Zanzibar kuchezea mechi yao, inaweza kuwa ni kutokana na uwepo wa mashabiki pia kwa idadi kubwa Zanzibar wanaoshabikia Yanga. Hata Zanzibar kuna shabiki wa Yanga pia
So Simba watacheza mechi ya kesho Lupaso ipi?
 
Wewe ni mnafiki na unafiki ni mbaya sana.
Wanafiki sio wale wale waliohamishia mechi za timu za serikali (JKU na Uhamiaji) uarabuni kwa maslahi yao na bila maelezo? Kuna mama mmoja mtaani kwangu niligombana nae, yeye ana watoto kama wangu lakini akitaka kutuma mtoto gengeni anawatuma watoto wangu na kuwaacha wakwake wanacheza sodo. Nikamuuliza kwanini Unafanya hivyo? Akasema wanangu mm hawarejeshi chenchi ukiwatuma.
 
Mazuri ya Tanganyika wazanzibar wanayataka, mpaka Sasa sijaona aliyejibu hoja kwanini timu za Zanzibar zikacheza mechi zao ugenini na yanga ikaenda Zanzibar .
Tra wakija kudai Kodi yao wasipige kelele wanaonewa.
Kikubwa ni kujipendekeza
Wanasiasa ndo wanatuzuga, wao wanaujua uzuri wa Muungano na wananufaika nao kwelikweli lakini ukiwagusa wanakwambia "mapinduzi daima" huku wakijua wazi wao Wana mashamba, majumba, biashara na migodi kule Tanganyika. Sisi ni watanzania tayari hakuna mjadala wa kuwa na TFF moja, ligi Moja, serikali Moja, sauti Moja na nguvu Moja ili tufaidi wote matunda ya pande zote kwa usawa.
 
Wanafiki sio wale wale waliohamishia mechi za timu za serikali (JKU na Uhamiaji) uarabuni kwa maslahi yao na bila maelezo? Kuna mama mmoja mtaani kwangu niligombana nae, yeye ana watoto kama wangu lakini akitaka kutuma mtoto gengeni anawatuma watoto wangu na kuwaacha wakwake wanacheza sodo. Nikamuuliza kwanini Unafanya hivyo? Akasema wanangu mm hawarejeshi chenchi ukiwatuma.
Wewe ni mnafiki kwasababu ukiwa moto kuwa moto na ukiamua kuwa baridi kuwa baridi sio huko kote umejifanya kutokukubali halafu tena mwishoni unakuja na comment ya namna hii "sina kinyongo na hili kama kwa kufanya hivi ni gundi imara ya muungano wetu. Yanga ilitumika sana kwenye harakati zetu mbalimbali sio vibaya ikiendelea na kazi yake iyo hata sasa"

Huo ndio unafiki na hauna msimamo na kama hiyo ulilijua uliandika uzi wa nini? Acha unafiki
 
Kaka wewe ndiye mnafiki uliyepitiliza. Kuna mtu anaendelea kusikika kuwa Yanga chimbuko lake ni Zanzibar na sauti hiyo inapazwa kwelikweli katika awamu hii ya Yanga. Huu ni uongozi unaofanana na ukweli. Timu hii imezaliwa 1935 wapi na akina nani? Wote tunamshukuru Mzee wetu Rais wa awamu ya Kwanza Zanzibar kwa "KUSAIDIA" Yanga kujenga jengo lile la Yanga, tunamshukuru wote kwa mapenzi yake kwa Yanga na Simba kutupa majengo, lakini majengo hayo hayakujengwa 1935 wakati Yanga inazaliwa Tanganyika. Kusema Yanga ina chimbuko lake Zanzibar ni kupotosha historia ya Yanga. Hata Mzee Nyerere aliikuta Yanga ipo na aliutumia kama ilivyo kwa mambo yake ya kisiasa.
Wapi nimesema chimbuko la Yanga ni Zanzibar? Nilichosema kuwa Yanga pia ina wanachama Zanzibar. Njoo ukatae hapa kama Yanga haina wanachama huko Zanzibar. La pili njoo unioneshe ni wapi nilipoandika kuwa Yanga ina chimbuko Zanzibar, usitake kunilisha maneno nisiyoyasema MNAFIKI mkubwa wewe.
 
Wanasiasa ndo wanatuzuga, wao wanaujua uzuri wa Muungano na wananufaika nao kwelikweli lakini ukiwagusa wanakwambia "mapinduzi daima" huku wakijua wazi wao Wana mashamba, majumba, biashara na migodi kule Tanganyika. Sisi ni watanzania tayari hakuna mjadala wa kuwa na TFF moja, ligi Moja, serikali Moja, sauti Moja na nguvu Moja ili tufaidi wote matunda ya pande zote kwa usawa.
Ndio maana nilikwambia wewe ni MNAFIKI, haya hayo maelezo uliyaandika hapo mtu anaweza kusema ni watu wawili tofauti na aliyetamka haya; nina kunukuu
"sina kinyongo na hili kama kwa kufanya hivi ni gundi imara ya muungano wetu. Yanga ilitumika sana kwenye harakati zetu mbalimbali sio vibaya ikiendelea na kazi yake iyo hata sasa"

Usiwe ndumilakwili
 
Back
Top Bottom