Yanga kwenda kucheza CAF champions Zanzibar, JKU na UHAMIAJI wamekataa kuchezea Zanzibar, Kuna nini?

Yanga kwenda kucheza CAF champions Zanzibar, JKU na UHAMIAJI wamekataa kuchezea Zanzibar, Kuna nini?

mambo mengine tunayakuza. nyie ndio mkizeeka mnakua visirani. mambo madogo hayo. siku wakicheza kwetu arumeru mtasema pia ama kisa kwa wanywa urojo?
Kabla ya kuhamisha mechi wape sababu wenye timu yao, na sababu lazima iwe ya kiufundi na kiuchumi, nothing more nothing more. Sio kwasababu za kisiasa Wala kupigia kampeni chama au mtu. Maana ni hatari sana Simba na Yanga kuziingiza kwenye siasa zetu za vyama.
 
Wenye timu yao ni akina nani?
 
50 mil sio za bure bure zile
Simba na Yanga ni madubwana makubwa ambayo hayakai chumba kimoja, ukilitumbukiza moja huku lingine linakwenda kule. Wewe huogopi!?

Wazee wetu kwa makusudi kabisa walizificha siri na asili za timu hizi mbili, lakini sasa hivi mtu ashindwa kupata cha kuongea, utamsikia hii imeleta uhuru, fulani ndiye kafanya nini, herere, herere, kajenga, alikuwa mpinzani, mwarabu, sijui nini!! Yule alikuwa mwanachama wetu, huyu ni mwanachama wetu!! Wakati wenyewe wamekufa hawajaweka hadharani walikuwa timu gani kati ya hizi mbili. Unajiuliza tunatakiwa kuelekea. Wapi? Wanaziekekeza wapi hizi timu?
 
Dar es

Kwani imesajiliwa wapi?

Timu hizi zisitumbukizwe kwenye siasa, ni hatari sana, ziachwe zicheze mpira. Wazee wetu walijizuia na jambo hili kwakuwa timu hizi
We jamaa nimejaribu kufatilia hoja zako zimekaa kibaguzi sana hauna hoja ya maana. Unasema kabla ya kuhamisha wawape taarifa wenye timu yao. Sijui kama unajua wenye timu ya Yanga ni akina nani, unajibu Dar es 😂😂😂sasa Dar es ni mtu? Hata kiswahili tu kinakupiga chenga.

Unakuja kumalizia kuwa timu hizi zisitumbukizwe kisiasa, kwani umeanza leo kufatilia mpira wa Simba na Yanga? Yanga na Simba zipo kisiasa tokea zinaanzishwa. Sasa unashangaa leo kutumika kisiasa? Siku ya Simba day na siku ya mwananchi hukuona raisi akiongea live? Mechi za kimataifa hushuhudiagi viongozi wa CCM wakiwa ni wageni rasmi kwenye michezo? Hiyo siasa umekuja kuiona leo kisa mechi kupelekwa Tanzania visiwani? Tafuta hoja zenye mashiko mzee.
 
Kwa mujibu wa zff walisema Kuwa caf wamesema uwanja wa Amani hauna vigezo maybe kibali kimetoka kwenye raundi ya pili
 
Labda kama nimesahau, sijawahi kuona picha ya Nyerere, Mzee mwinyi, Mkapa, Kikwete, au magufuli Iko kwenye fulana za mashabiki wa mpira viwanjani Wala bango lenye picha zao viwwnjani. Sasa tumenza kidogo kidoogo pooolepooole,

Siku moja nilikuwa namuuliza mwl Nyerere kuwa unazionaje siasa zetu kama nyinnyi wakongwe mtakosekana? Akasema, natamani kuona kabla sijaondoka kuwe na vyama vikubwaaa 2 vyenye uzani unaokaribia vikikosoana vyewewe kwa vyenyewe kwa sera safi na tabia na kupokezana kuiongoza nchi. Ataendelea kusema "watu binafsi watakaoweza kuwakemea watawala kama mimi watakuwa adimu sana" Na mwenyewe alikuwa anaiona kidooogo CHADEMA kama vile ilikuwa ikielekea kuwa na sifa hizo. Lakini sasa, loooh!!

Ndio sisi tusio rasmi tunaonya na tunajitopokea TU kuhusu mustakabali wetu kama tusipokuwa makini huko mbeleni.

Historia ya Yanga na Simba sio nzuri sana, walioanzisha Simba/sunderland enzi hizo hawakuwa na nia nzuri.
 
Kaka Man U ni timu ya Manchester hata kama ina mashabiki dunia nzima, Liverpool ni timu ya Liverpool, Real Madrid ni ya jiji la Madrid, Barcelona iko pale Catalunya; Al-Ahly iko pale Cairo, watu wa miji hiyo ndiyo starehe yao na uchumi wao; wengine waende huko kama wakitaka kuzishuhudia zikicheza au wazisubiri zikija kucheza mechi zao na timu nyingine kwenye ligi au ngao ya jamii au pre-season. Marketing na kuwasogezea mashabiki wengine timu kunafanyika wakati wa pre-seasons tu.
Wakati 5imba na Yanga zinaenda kucheza dabi uwanja wa Tanganyika, Kigoma, kuna aliyeuliza? Wakati Yanga na Coast wanacheza Sheikh Amri Abeid, Arusha, kuna aliyeuliza? Wakati 5imba na Azam wanacheza pale Nangwanda Sijaona, Mtwara, kuna aliyeuliza? Wakati 5imba na Yanga wanacheza Mkwakwani Tanga kuna aliyeuliza? etc. Hizo timu zote tajwa hapo juu zilicheza nje ya 'nyumbani' kwao..!! Kwanini hii leo iwe nongwa hao ambao nyumbani kwao ni ZENJI kucheza nje ya ZENJI..!!??
 
Hiyo ni tofauti sana na hiyo. Safari hii imekwenda Zanzibar, nchi jirani kisoka bila sababu za msingi. Wakati wanakwenda kigoma na Arusha sababu zilikuwepo, lakini huko kigoma na Arusha ni himaya ya TFF pia, Zanzibar Kuna ZFF.
 
Huna ulichokisema cha maana. Yanga ni timu ya dar es Salaam, wanataka kufaidika na timu yao directly na indirectly. Kuna wanaonufaika directly kama waajiliwa, serikali (mapato na Kodi), uwanja, TFF, DRFA, TEFA nk na Kuna wanaonufaika na mechi za kimataifa za Yanga indirectly ( mahoteli, mamalishe, daladala, bodaboda, machinga, nk). Hawa wooooote huwezi kuwapiga mswaki eti kiongozi mmoja wa timu ana mahaba na kwao. Aliyesema Yanga ni timu ya Muungano ni nani?
Usipotoke kama babu Magoma, anayepotoka kuwa Yanga ni mali yake.
Yanga ni ya mali ya wanachama ambao wametapakaa Tanzania yote, ikiwemo Unguja na Pemba.

Klabu ina dhima na sababu ya kuwajibika kuwapelekea burdan wanachama wake kwa kadri fursa inavyopatikana.
 
Wakati 5imba na Yanga zinaenda kucheza dabi uwanja wa Tanganyika, Kigoma, kuna aliyeuliza? Wakati Yanga na Coast wanacheza Sheikh Amri Abeid, Arusha, kuna aliyeuliza? Wakati 5imba na Azam wanacheza pale Nangwanda Sijaona, Mtwara, kuna aliyeuliza? Wakati 5imba na Yanga wanacheza Mkwakwani Tanga kuna aliyeuliza? etc. Hizo timu zote tajwa hapo juu zilicheza nje ya 'nyumbani' kwao..!! Kwanini hii leo iwe nongwa hao ambao nyumbani kwao ni ZENJI kucheza nje ya ZENJI..!!??
Achana nao hao Makolo wenye husda! Yanga ndiyo inayoonesha njia tangu zama za kale
dahali zilizopita... wengine wataiga tu!
 
kama tim nzur inafany vizr ipongez tuh sio unaanz kutoa manen makal au kisa jina la makolo ndy linakup kero
 
Usipotoke kama babu Magoma, anayepotoka kuwa Yanga ni mali yake.
Yanga ni ya mali ya wanachama ambao wametapakaa Tanzania yote, ikiwemo Unguja na Pemba.

Klabu ina dhima na sababu ya kuwajibika kuwapelekea burdan wanachama wake kwa kadri fursa inavyopatikana.
Tusidanganyane watu. Wakati Yanga inazaliwa 1935 Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi 2 tofauti kabisaaaaaa. Ukiacha Mzee Karume kusaidia ujenzi wa lile jengo hakuna kingine. Mwaka 1964 Yanga haikuwa kati ya Yale mambo ya muungano. Hata Man U, arsenal, Liverpool, Chelsea ziko ulaya lakini Zina mashabiki hata kule mfaranyaki, mbona hatuletewi mechi za man u?
 
Kwanini Karume asaidie jengo la Yanga kama sio mshabiki/ mwanachama wa Yanga? Yanga ni timu ya wanachama na hao wanachama wapo hadi Zanzibar unalinganisha vipi na Man united?
Kuna kosa gani wanachama wa Yanga waliopo Zanzibar kuona timu yao ya Yanga? Akili yako inawaza kama vile Yanga ni timu ya jamii fulani ya watu wakati Yanga ni timu ya wanachama na mmoja ya mjumbe wa baraza la wadhamini anatokea Zanzibar. Hauna hata moja ya maana
 
Kama ni 50m ni nyingi sana
Ndio maana nimesema natengua kauli, maana hz 50m ingewezekana Kila timu za Yanga, Simba, coastal na Azam zote zikapata. Zilikuwa ni kwa wote, sio Yanga TU.

Nimesema Wacha ikachezwe Zanzibar kama ikibainika kuwa Yanga inaweza kutumika kuuboresha na kuimarisha muungano wetu. Rais Mwinyi na Rais Samia Wana nia safi na werevu mkubwa sana, inawezekana Simba na Yanga zikauboresha muungano wetu kuwa Bora zaidi kuliko ulivyokuwa huko nyuma.
 
Michezo siku zote ina imarisha udugu
 
Back
Top Bottom