Haiwezi kuwa hivyo, unataka kusema Iko siku Man U wanawezakupeleka mechi zao Afrika kwakuwa Wana wapenzi wengi pia?
Kwenye mechi kama hizi Kuna vitu ambavyo ni zaidi ya mpira. Kuna watu wanafanyabiashara, kunawatu wanaenda kufurahi na Kuna taasisi zinapata makusanyo kutokana na mechi hizi, sio maswala ya kuhamisha mechi TU. JKU na UHAMIAJI hawakuona faida ya kiuchumi kwa wageni kuja Zanzibar kulala, kula, kusafiri, viingilio na furaha kwa watanzania hasa wa Zanzibar wenzao, badala yake wanataka kazi hiyo kuiachia Yanga timu ya Tanzania bara. Hii haiwezi kuwa sawa . Yaani unamtuma mwanangu kwenda kulinda mpunga wako wakati mwanao kaenda beach kuogelea. Yanga ni timu ya dar es salaam ya watu wa dar es salaam kwa maslahi ya watu wa dar es Salaam.