Yanga kwenda kucheza CAF champions Zanzibar, JKU na UHAMIAJI wamekataa kuchezea Zanzibar, Kuna nini?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Timu za JKU na UHAMIAJI ni timu za Zanzibar kindaki ndaki kuliko Yanga. Hatukuelezwa kwanini JKU na UHAMIAJI hawakutaka mechi zao za mashindano ya CAF wachezee Zanzibar, lakini Yanga wanataka kwenda kucheza CAF championship mzunguuko wa pili Zanzibar. Kuna nini hasa hapo?

Ufafanuzi unahitajika juu ya jambo hili. Michezo ni furaha, uchumi na undugu, kwanini JKU na UHAMIAJI walihamisha furaha, uchumi na undugu unaotokana na michezo kwenda Egypt na Libya na Yanga kupeleka Zanzibar furaha, uchumi na undugu Zanzibar kutoka dar es salaam?

Je, unawaweza kuwa mkatoliki safi kumzidi Pope?; muislam fafi kuliko mufti?
 
Timu za JKU na UHAMIAJI ni timu za Zanzibar kindaki ndaki kuliko Yanga
Hao Uhamiaji na JKU kuhamisha mechi zao walipopangwa na waarabu wanajua wao nini kilichowasukuma kufanya hivyo. Lakini kikanuni uwanja wa Amani hauna changamoto yoyote kutumika katika mashindano ya CAF. Yanga hutumia uwanja wa Mkapa lakini kwasasa umezuiwa kutumika sababu ya kupisha ukarabati unaoendelea. Hivyo wana option ya kutumia uwanja wa Azam complex.

Kuamua kwenda Zanzibar kuchezea mechi yao, inaweza kuwa ni kutokana na uwepo wa mashabiki pia kwa idadi kubwa Zanzibar wanaoshabikia Yanga. Hata Zanzibar kuna shabiki wa Yanga pia
 
Hao Uhamiaji na JKU kuhamisha mechi zao walipopangwa na waarabu wanajua wao nini kilichowasikuma kufanya hivyo. Lakini kikanuni uwanja wa Amani hauna changamoto yoyote kutumika katika mashindano ya CAF. Yanga hutumia uwanja wa Mkapa lakini kwasasa umezuiwa kutumika sababu ya kupisha ukarabati unaoendelea. Hivyo wana option ya kutumia uwanja wa Azam complex.

Kuamua kwenda Zanzibar kuchezea mechi yao, inaweza kuwa ni kutokana na uwepo wa mashabiki kwa idadi kubwa Zanzibar wanaoshabikia Yanga. Hata Zanzibar kuna shabiki wa Yanga
Haiwezi kuwa hivyo, unataka kusema Iko siku Man U wanawezakupeleka mechi zao Afrika kwakuwa Wana wapenzi wengi pia?

Kwenye mechi kama hizi Kuna vitu ambavyo ni zaidi ya mpira. Kuna watu wanafanyabiashara, kunawatu wanaenda kufurahi na Kuna taasisi zinapata makusanyo kutokana na mechi hizi, sio maswala ya kuhamisha mechi TU. JKU na UHAMIAJI hawakuona faida ya kiuchumi kwa wageni kuja Zanzibar kulala, kula, kusafiri, viingilio na furaha kwa watanzania hasa wa Zanzibar wenzao, badala yake wanataka kazi hiyo kuiachia Yanga timu ya Tanzania bara. Hii haiwezi kuwa sawa . Yaani unamtuma mwanangu kwenda kulinda mpunga wako wakati mwanao kaenda beach kuogelea. Yanga ni timu ya dar es salaam ya watu wa dar es salaam kwa maslahi ya watu wa dar es Salaam.
 
Ni unafiki na kujipendekeza kwa serikali ndio maana namwona Magoma ana akili.
Hizi timu wamenyang'wanya wenye nazo waliozichukua wanazitumia kwa manufaa binafsi kisingizio vya kijinga.
Huwezi kuwaondolea furaha na uchumi (hotels, wauza madhaifu, wauza vuvuzela, wauza maji, bodaboda, DRFA, TEFA, nk) wao watu wa dar es Salaam kihuni na kwasababu zako wewe. Klabu hizi ni zaidi ya kombe,
 
Yanga ni timu ya dar es salaam ya watu wa dar es salaam kwa maslahi ya watu wa dar es Salaam.
Mbona hukuleta uzi kulalamikiia Yanga walipochagua uwanja wa CCM KirumbaMwanza kuwa uwanja wao wa nyumbani kama Yanga ipo kwaajili ya watu wa Dar es Salaam pekee.?
2) kama Yanga ingekuwa kwaajili ya watu wa Dar es Salaam pekee, isingekuwa inapokea mashabiki na wanachama wa nje ya Dar es Salaam kwanini imekuwa timu inayoenda kusajili mashabiki hadi Afrika kusini?

Manchester united haiwezi kuhamisha uwanja kutokana na kanuni zao za mashindano ya FA yao na UEFA. Lakini kwa mashindano yaliyopo CAF ni ruhusa kwa timu mwenyeji kuamua kuchezea mechi yake wapi. Ndio maana unaona timu ya Sudani inaenda kucheza mechi yake Rwanda au timu ya Djibouti inaenda kuchezea mechi yake Tanzania.
 
Timu za JKU na UHAMIAJI ni timu za Zanzibar kindaki ndaki kuliko Yanga. Hatukuelezwa kwanini JKU na UHAMIAJI hawakutaka mechi zao za mashindano ya CAF wachezee Zanzibar, lakini Yanga wanataka kwenda kucheza CAF championship mzunguuko wa pili Zanzibar. Kuna nini hasa hapo?

Ufafanuzi unahitajika juu ya jambo hili. Michezo ni furaha, uchumi na undugu, kwanini JKU na UHAMIAJI walihamisha furaha, uchumi na undugu unaotokana na michezo kwenda Egypt na Libya na Yanga kupeleka Zanzibar furaha, uchumi na undugu Zanzibar kutoka dar es salaam?

Je, unawaweza kuwa mkatoliki safi kumzidi Pope?; muislam fafi kuliko mufti?
hauna hoja, ila wapo watakaokuunga mkono.

Maelezo yako yameegemea ubara na Uzanzibari kisha ukristo na uislamu.

Unaweza ona mtoa mada ni mteja mzuri wa vibanda umiza kuliko kuangalia mpira akiwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ngoja nikufundishe, tena kaa kwa kutulia, kuna kipindi uefa walipendekeza baadhi ya mechi za uefa zichezwe nje ya ulaya kwenda kwenye nchi kama vile Marekani na Morocco, tp mazembe walicheza mechi za mashindano yaliyoratibiwa na FIFA hapa Tanzania, na mifano mingine mingi tu ipo.
Mwisho nikuweke sawa kuhusu kuwa na imani thabiti dhidi ya viongozi wa imani husika, kuwa pope/mufti hakumfanyi mtu kuwa bora zaidi kiimani kuliko wengine, imani ya mtu ni siri kati yake na mola wake, unaweza kuwa pope/muft na ukafanya machafu makubwa zaidi kuliko waumini wako.

Kama unaipenda Yanga ifuate unguja.
 
Umelopoka tu .. hao To mazembe walikuja Tz pasina sababu au kutokizi vigezo?. Ni utahira wa viongozi.
 
Mbona hukuleta uzi kulalamikiia Yanga walipochagua uwanja wa CCM KirumbaMwanza kuwa uwanja wao wa nyumbani kama Yanga ipo kwaajili ya watu wa Dar es Salaam pekee.
2) kama Yanga ingekuwa kwaajili ya watu wa Dar es Salaam pekee, isingekuwa inapokea mashabiki wa nje ya Dar es Salaam lakini imekuwa timu inayoenda kusajili mashabiki hadi Afrika kusini?

Manchester united haiwezi kuhamisha uwanja kutokana na kanuni zao za mashindano ya FA yao na UEFA. Lakini kwa mashindano yaliyopo CAF ni ruhusa kwa timu mwenyeji kuamua kuchezea mechi yake wapi. Ndio maana unaona timu ya Sudani inaenda kucheza mechi yake Rwanda au timu ya Djibouti inaenda kuchezea mechi yake Tanzania.
Yanga ni timu ya ligi ya Tanzania bara, Zanzibar Wana ligi yao. Ingekuwa sawa unachosema kama ligi ya Tanzania nzima ingekuwa Moja. Lakini kama Zanzibar imeruhusu JKU na UHAMIAJI wahamishe mechi zao Misri na Libya maana yake hawakujali faida (uchumi na kijamii) zote za timu kucheza mechi nyumbani. Faida hizo haziwezi kufidiwa na Yanga kwa mtindio wa strengthen the weakest by weakening the strongest. Unaweza kufanya hivyo kwenye ngao ya jamii, kiusalama au kupata mapato mengi kwa mechi kuchezea mji fulani.
 
H
hauna hoja, ila wapo watakaokuunga mkono.

Maelezo yako yameegemea ubara na Uzanzibari kisha ukristo na uislamu.

Unaweza ona mtoa mada ni mteja mzuri wa vibanda umiza kuliko kuangalia mpira akiwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ngoja nikufundishe, tena kaa kwa kutulia, kuna kipindi uefa walipendekeza baadhi ya mechi za uefa zichezwe nje ya ulaya kwenda kwenye nchi kama vile Marekani na Morocco, tp mazembe walicheza mechi za mashindano yaliyoratibiwa na FIFA hapa Tanzania, na mifano mingine mingi tu ipo.
Mwisho nikuweke sawa kuhusu kuwa na imani thabiti dhidi ya viongozi wa imani husika, kuwa pope/mufti hakumfanyi mtu kuwa bora zaidi kiimani kuliko wengine, imani ya mtu ni siri kati yake na mola wake, unaweza kuwa pope/muft na ukafanya machafu makubwa zaidi kuliko waumini wako.

Kama unaipenda Yanga ifuate unguja.
una maarifa, unaweza kuhamisha mechi kwenda mji, nchi au bara lingine kwasababu za kiuchumi na kiusalama TU baaasi. Yanga iliipeleka mechi kule Amani kwa sababu zipi?
 
Mbona hukuleta uzi kulalamikiia Yanga walipochagua uwanja wa CCM KirumbaMwanza kuwa uwanja wao wa nyumbani kama Yanga ipo kwaajili ya watu wa Dar es Salaam pekee.
2) kama Yanga ingekuwa kwaajili ya watu wa Dar es Salaam pekee, isingekuwa inapokea mashabiki wa nje ya Dar es Salaam lakini imekuwa timu inayoenda kusajili mashabiki hadi Afrika kusini?

Manchester united haiwezi kuhamisha uwanja kutokana na kanuni zao za mashindano ya FA yao na UEFA. Lakini kwa mashindano yaliyopo CAF ni ruhusa kwa timu mwenyeji kuamua kuchezea mechi yake wapi. Ndio maana unaona timu ya Sudani inaenda kucheza mechi yake Rwanda au timu ya Djibouti inaenda kuchezea mechi yake Tanzania.
Kaka ndio maana kila mkoa unapambana kupata timu ya ligi kuu ili kupata faida za kiuchumi na kijamii kupitia timu yao. Kilevi TU huwezi kuhamisha Fursa za watu wa dar ukazipeleka sehemu nyingi kwa utashi TU wa mwenyekiti.
 
Gharama nafuu kuliko Chamanzi Comp.
Gharama nafuu kiveepe? Timu kwenda Zanzibar maana yake utalipa usafiri wa wachezaji, benchi la ufundi na msululu wa viongozi. Watu wote hao watalipiwa malazi, chakula na fedha za kujikimu (per diem) kwa siku zote watakazokuwepo Zanzibar na wakati huohuo bill za pango za Avic ziko palepale. Lakini Kuna watu Dar ambao walikuwa wapate Fursa za kibiashara kutokana na uwepo wa mechi uwanja wa Benjamin Mkapa watakosa hiyo fursa, na watu wa DSM na mikoa jirani ambao wanakuja dar kuona mechi hawatakuja.

Timu haina uwanja wa mazoezi lazima tujali kupunguza gharama za uendeshaji ili tujenge hostels na uwanja.
 
Kaka ndio maana kila mkoa unapambana kupata timu ya ligi kuu ili kupata faida za kiuchumi na kijamii kupitia timu yao. Kilevi TU huwezi kuhamisha Fursa za watu wa dar ukazipeleka sehemu nyingi kwa utashi TU wa mwenyekiti.
Labda amefuatwa MAKAMU WA RAIS, Arafat!
 
I
Labda amefuatwa MAKAMU WA RAIS, Arafat!
Inawezekana, lakini hiyo ni kuitangua torati kusikotakiwa. Timu hizi za mpira ni zaidi ya magoli na ushindi. Kila mkoa, kila Wilaya na Kila jiji linalilia kuwa na timu ya mpira kwakua mpira ni chanzo cha mapato kwa mnyororo mrefu wa wadau. Hivyo kuhamisha mechi kwenda mkoa au nchi nyingine lazima kuwe na sababu ya wazi kabisa kama viwanja, usalama au mwaliko unaogharimiwa na mwalikaji.

Binafsi mm ni miongoni mwa waliokereka kwa ZFF kuridhia JKU na UHAMIAJI kupeleka mechi uarabuni. Kuhamisha mechi kunahamishia mapato na furaha kwa watu wengine. Ukitaka ukweli Yanga jina lake ni Dar ES salaam young africans
 
Back
Top Bottom