Kwenye ile mechi ya Al Ahly, kwenye benchi ukiachana na Mudathir na Musonda nitajie wachezaji wengine wenye uwezo na ubora wa kubadilisha mchezo kwa siku ile. Wachezaji wengi tu wa Yanga walikuwa wamechoka na hakuwa Aziz Ki peke yake, hata huku nyuma mabeki walikuwa wanapiga pasi za ovyo na wengine kudondoka dondoka hovyo. Maxi pia alichoka kule mbele, lakini ni nani ataingia mwenye quality sawa na au kumzidi Maxi? Al Ahly wakitoa mtu anaingia chuma kingine.
Wachezaji ambao hawajacheza muda mrefu huwa kuna aina ya mechi na pia kuna dakika za kuingia. Kocha yeye ndiye anayejua ni mechi ipi atawapanga hao wengine fixtures bado ndefu sana. La mwisho kocha ndiye huwa na timu mazoezini hivyo ndiye anayejua utimamu wa wachezaji. Ulimuongelea Farid Mussa, hivi ulishawahi kumuona hata mazoezini kama wengine wanavyoonekana?