Yanga mjitathmini na ubingwa wenu wa kihistoria

Yanga mjitathmini na ubingwa wenu wa kihistoria

Kalpana

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2017
Posts
32,603
Reaction score
62,269
Wasalaaam wana jukwaaa..kwanza nipende kuwapongeza watani kwa kuchukua kombe msimu huu baada ya kuhenyeka kwa miaka minne bila bila? Yani achana tu na kukosa kombe walipigwa na uhaba wa pesa si mchezo yani kiufupi walihenya hivyo basi kwa heka heka hizo hatuna budi kuwapongeza. .mimi Simba dada

Nije kwnye lile nalotaka kulizungumzia..Yanga mnajikweza na kujimwambafy na kujiona mmefika eti kisa tuuu mmechukua kombe mara 28 hivi hili nalo ni la kuliongelea kila leo? Wakati makombe mengine mmechukua hata member wengine hawajazaliwa humu kiasi kwamba mnaridhika na matokeo haya ya ligi kuu kimataifa mnatupwa huko.

Sasa unajisifu ww ni bingwa mara 28 hujulikani hata kwny ramani ya soka la Africa huoni kwamba unapoteza muda na mashabiki zako humu humu au wenzetu hamtaki soka la biashara soka la kiushindani?.yani nyie kombe la ligi kuu mkichukua mnanyanyua miguu juu hebu amkeni safari hii hatutaki aibu hayo makombe yenu yasadifu uhalisia.

Halafu hivi hapa nchini timu zetu zina kombe moja tuu ambalo linahesabiwa?.ukijumuisha yote Simba baba lao ana makombe mengi zaidi au nyie hayo hayawahusu? Mimi nakerwa sana mtu unamkuta anaanza kwa kusema sisis Yan'ga mabingwa wa kihistoria sasa nani anaetaka kujua historia hapa wakati hata shule somo la historia limefutwa. Tunachotaka kujua maendeleo ya timu hapa namaanisha timu kwa sasa inavyoperfom na matokeo yake,uwekezaji wake, na inatuwakilishaje kimataifa na sio porojo za sisi ni mabingwa kihistoria.

Hapa pia mjifunze kwa Simba hawadharau mechi au mashindano yoyote kama kuna mashindano ya kugombea kombe lolote inajitoa na sio kukamia ligi kuu ndo maana wanawazidi kwa makombe ya mjumuisho. Sema tuu upepo mbaya umeipitia timu yangu msimu huu tumeondoka na kombe la mapinduzi pekee.

Mwisho niwakumbushe msimu ujao utakua wa motoooo yani motooo mjiandae kisaikolojia msikariri kuwa kila msimu tunaachiana misimu 4 mi 4 safari hii huu mmoja unawatosha.

Adhuhuri njema.

Kalpana
 
Wasalaaam wana jukwaaa..kwanza nipende kuwapongeza watani kwa kuchukua kombe msimu huu baada ya kuhenyeka kwa miaka minne bila bila?...
Kesho tunakabidhiwa rasmi kombe pale Sokoine kwa ushindi mnono kama kawaida yetu. Sasa wewe endelea tu kulalamika.

Sisi ndiyo Mabingwa wa wakati wote! Mabingwa wa Kihistoria! Timu ya Wananchi! The 2021/2022 Champions of NBC Premier League 🏆🥇💪

Na msimu ujao tutawapelekea pumzi ya moto kama kawaida yetu. Maana hakuna namna.
 
Una option ya kulia au kucheka lkn haita badili ukweli Yanga bingwa
Sijakataa ni bingwa ila.neno wa kihistoria linatumika vibaya. Either linawafanya mvimbe bila sababu la linawafanya mbweteke..kuna watu waliongoza miaka yote ya shule ila haimaanishi kule kuongoza kwao kumewasaidia lolote au kuwapa cha maana imebakia historia tuu fulani jamani alikua anaongoza ila kwa sasa ni chapombe.
 
Back
Top Bottom