Yanga mjitathmini na ubingwa wenu wa kihistoria

Yanga mjitathmini na ubingwa wenu wa kihistoria

Sijakataa ni bingwa ila.neno wa kihistoria linatumika vibaya. Either linawafanya mvimbe bila sababu la linawafanya mbweteke..kuna watu waliongoza miaka yote ya shule ila haimaanishi kule kuongoza kwao kumewasaidia lolote au kuwapa cha maana imebakia historia tuu fulani jamani alikua anaongoza ila kwa sasa ni chapombe.
Kunywa maji kwanza wewe kolo
 
Wasalaaam wana jukwaaa..kwanza nipende kuwapongeza watani kwa kuchukua kombe msimu huu baada ya kuhenyeka kwa miaka minne bila bila? Yani achana tu na kukosa kombe walipigwa na uhaba wa pesa si mchezo yani kiufupi walihenya hivyo basi kwa heka heka hizo hatuna budi kuwapongeza. .mimi Simba dada

Nije kwnye lile nalotaka kulizungumzia..Yanga mnajikweza na kujimwambafy na kujiona mmefika eti kisa tuuu mmechukua kombe mara 28 hivi hili nalo ni la kuliongelea kila leo? Wakati makombe mengine mmechukua hata member wengine hawajazaliwa humu kiasi kwamba mnaridhika na matokeo haya ya ligi kuu kimataifa mnatupwa huko.

Sasa unajisifu ww ni bingwa mara 28 hujulikani hata kwny ramani ya soka la Africa huoni kwamba unapoteza muda na mashabiki zako humu humu au wenzetu hamtaki soka la biashara soka la kiushindani?.yani nyie kombe la ligi kuu mkichukua mnanyanyua miguu juu hebu amkeni safari hii hatutaki aibu hayo makombe yenu yasadifu uhalisia.

Halafu hivi hapa nchini timu zetu zina kombe moja tuu ambalo linahesabiwa?.ukijumuisha yote Simba baba lao ana makombe mengi zaidi au nyie hayo hayawahusu? Mimi nakerwa sana mtu unamkuta anaanza kwa kusema sisis Yan'ga mabingwa wa kihistoria sasa nani anaetaka kujua historia hapa wakati hata shule somo la historia limefutwa. Tunachotaka kujua maendeleo ya timu hapa namaanisha timu kwa sasa inavyoperfom na matokeo yake,uwekezaji wake, na inatuwakilishaje kimataifa na sio porojo za sisi ni mabingwa kihistoria.

Hapa pia mjifunze kwa Simba hawadharau mechi au mashindano yoyote kama kuna mashindano ya kugombea kombe lolote inajitoa na sio kukamia ligi kuu ndo maana wanawazidi kwa makombe ya mjumuisho. Sema tuu upepo mbaya umeipitia timu yangu msimu huu tumeondoka na kombe la mapinduzi pekee.

Mwisho niwakumbushe msimu ujao utakua wa motoooo yani motooo mjiandae kisaikolojia msikariri kuwa kila msimu tunaachiana misimu 4 mi 4 safari hii huu mmoja unawatosha.

Adhuhuri njema.

Kalpana
Dada usikasirike sana, kila mtu na kamuhogo kake, wakati wengine wamezoeshwa chips na makorokocho wenzao wakipata kiporo wanatamba mtaa mzima.

Vv
 
Hivi wana simba mnapata wapi ujasiri wa kuishauri club ya YANGA mambo ya huko kimataifa kama vile nyinyi mna mafanikio huko?
Kuwa na point 28 huko caf huku mwingine akiwa na point 0.5 na kufanikiwa kuingiza timu 4 katika mashindano ya CAF tayari ni mafanikio.

Lini mchezaji wa Namungo , Biashara n.k. angepanda ndege kwenda nje ya nchi kucheza mechi za kimataifa kama siyo mafanikio ya simba.

Tatizo la utopolo ni kukariri kwamba mafanikio ni kombe tu.
 
Hatuna ila juhudi zetu siku moja zitazaa matunda

Nikajua mmechukua kombe la afrika kumbe kuishia darasa la 4 na kufeli ni mafanikio hayo?? Mbona simba hamjifunzi walau kutoka hapo kwenye robo kwenda hata nusu fainal?? Simba kiburi cha kuicheka yanga mnatoa wapi wakati huna kombe lolote ambalo yanga hana.
 
Sijakataa ni bingwa ila.neno wa kihistoria linatumika vibaya. Either linawafanya mvimbe bila sababu la linawafanya mbweteke..kuna watu waliongoza miaka yote ya shule ila haimaanishi kule kuongoza kwao kumewasaidia lolote au kuwapa cha maana imebakia historia tuu fulani jamani alikua anaongoza ila kwa sasa ni chapombe.
Narudia tena,Yanga ni Mabingwa wa Kihistoria uwe unataka au hutaki.
 
Kuwa na point 28 huko caf huku mwingine akiwa na point 0.5 na kufanikiwa kuingiza timu 4 katika mashindano ya CAF tayari ni mafanikio.

Lini mchezaji wa Namungo , Biashara n.k. angepanda ndege kwenda nje ya nchi kucheza mechi za kimataifa kama siyo mafanikio ya simba.

Tatizo la utopolo ni kukariri kwamba mafanikio ni kombe tu.
Hizo to points 28 zichukueni ziwasadie kua mabingwa
 
Sasa huyu nae kaandika nini?

Nyie ndio mashabiki oya oya huko ukoloni
Itakua ime kutouch. Ila ww unavyoandika threads za Simba ushabiki oya oya wa huko utopoloni huwa huuoni?
 
Nikajua mmechukua kombe la afrika kumbe kuishia darasa la 4 na kufeli ni mafanikio hayo?? Mbona simba hamjifunzi walau kutoka hapo kwenye robo kwenda hata nusu fainal?? Simba kiburi cha kuicheka yanga mnatoa wapi wakati huna kombe lolote ambalo yanga hana.
Anzeni nyie japo kushinda makundi tuu nyie mabingwa wa mali kale
 
Kuwa na point 28 huko caf huku mwingine akiwa na point 0.5 na kufanikiwa kuingiza timu 4 katika mashindano ya CAF tayari ni mafanikio.

Lini mchezaji wa Namungo , Biashara n.k. angepanda ndege kwenda nje ya nchi kucheza mechi za kimataifa kama siyo mafanikio ya simba.

Tatizo la utopolo ni kukariri kwamba mafanikio ni kombe tu.
Tena kombe la ligi kuu tuuu hahaha
 
Back
Top Bottom