Yanga mjitathmini na ubingwa wenu wa kihistoria

Wasalaaam wana jukwaaa..kwanza nipende kuwapongeza watani kwa kuchukua kombe msimu huu baada ya kuhenyeka kwa miaka minne bila bila? Yani achana tu na kukosa kombe walipigwa na uhaba wa pesa si mchezo yani kiufupi walihenya hivyo basi kwa heka heka hizo hatuna budi kuwapongeza. .mimi Simba dada

Nije kwnye lile nalotaka kulizungumzia..Yanga mnajikweza na kujimwambafy na kujiona mmefika eti kisa tuuu mmechukua kombe mara 28 hivi hili nalo ni la kuliongelea kila leo? Wakati makombe mengine mmechukua hata member wengine hawajazaliwa humu kiasi kwamba mnaridhika na matokeo haya ya ligi kuu kimataifa mnatupwa huko.

Sasa unajisifu ww ni bingwa mara 28 hujulikani hata kwny ramani ya soka la Africa huoni kwamba unapoteza muda na mashabiki zako humu humu au wenzetu hamtaki soka la biashara soka la kiushindani?.yani nyie kombe la ligi kuu mkichukua mnanyanyua miguu juu hebu amkeni safari hii hatutaki aibu hayo makombe yenu yasadifu uhalisia.

Halafu hivi hapa nchini timu zetu zina kombe moja tuu ambalo linahesabiwa?.ukijumuisha yote Simba baba lao ana makombe mengi zaidi au nyie hayo hayawahusu? Mimi nakerwa sana mtu unamkuta anaanza kwa kusema sisis Yan'ga mabingwa wa kihistoria sasa nani anaetaka kujua historia hapa wakati hata shule somo la historia limefutwa. Tunachotaka kujua maendeleo ya timu hapa namaanisha timu kwa sasa inavyoperfom na matokeo yake,uwekezaji wake, na inatuwakilishaje kimataifa na sio porojo za sisi ni mabingwa kihistoria.

Hapa pia mjifunze kwa Simba hawadharau mechi au mashindano yoyote kama kuna mashindano ya kugombea kombe lolote inajitoa na sio kukamia ligi kuu ndo maana wanawazidi kwa makombe ya mjumuisho. Sema tuu upepo mbaya umeipitia timu yangu msimu huu tumeondoka na kombe la mapinduzi pekee.

Mwisho niwakumbushe msimu ujao utakua wa motoooo yani motooo mjiandae kisaikolojia msikariri kuwa kila msimu tunaachiana misimu 4 mi 4 safari hii huu mmoja unawatosha.

Adhuhuri njema.

Kalpana
Kwanza Asante Kwa pongezi,pili Bado sisi ukubali ukatae ni mabingwa wa kihishoria,kuhusu lini ubingwa utarudi kwenu Kwa uchache hesabu miaka Saba ijsyo/misimu .Habari ya kimataifa tunaenda kuwaduwaza,mlisema mnacheza pira biliani,Sasa sisi kwenye Hilo hatuna maneno mingi.Kaa mkao wa kushuhidia🏃🏃🏃🏃
 
Sijakataa ni bingwa ila.neno wa kihistoria linatumika vibaya. Either linawafanya mvimbe bila sababu la linawafanya mbweteke..kuna watu waliongoza miaka yote ya shule ila haimaanishi kule kuongoza kwao kumewasaidia lolote au kuwapa cha maana imebakia historia tuu fulani jamani alikua anaongoza ila kwa sasa ni chapombe.
Ila hizo Dua za🐔🐔🐔🐔🐔🐔
 
Kwanza Asante Kwa pongezi,pili Bado sisi ukubali ukatae ni mabingwa wa kihishoria,kuhusu lini ubingwa utarudi kwenu Kwa uchache hesabu miaka Saba ijsyo/misimu .Habari ya kimataifa tunaenda kuwaduwaza,mlisema mnacheza pira biliani,Sasa sisi kwenye Hilo hatuna maneno mingi.Kaa mkao wa kushuhidia🏃🏃🏃🏃
Sawaaa kila la heri
 
Hahahaa! Ujue bana Mtani zipo njia nyingi sana za upunguzaji wa maumivu.

Ivo cha zaidi namsifu sababu hajataka kubaki nayo moyoni. 😅
😃😃maumivu yapi mtani?
 
Simba tunachukua kombe mwakani hiyo historia yenu iliishapita miaka 20 nyuma.
 
☝️☝️ Haya ndo maumivu nasemea 😅 kukosa Kombe Mtani. We Msimu mpya hata haujaanza ushajipigia hesabu za kulichukua. Lol

Tengeneza timu kwanza haya ya ubingwa tuachie mabingwa wa kihistoria. 😂
 
Timu yetu ilishatengenezwa kitambo sema ni vile msimu ulikua mbaya tuu na unajua wazi kabisa ratiba ilivyokua ngumu kwetu. Hivyo kupanga ni kuchagua na tumechagua kuchukua kombe msimu ujao wala sio maumivu.
 
Wasalaaam wana jukwaaa..kwanza nipende kuwapongeza watani kwa kuchukua kombe msimu huu baada ya kuhenyeka kwa miaka minne bila bila? Yani achana tu na kukosa kombe walipigwa na uhaba wa pesa si mchezo yani kiufupi walihenya hivyo basi kwa heka heka hizo hatuna budi kuwapongeza. .mimi Simba dada

Nije kwnye lile nalotaka kulizungumzia..Yanga mnajikweza na kujimwambafy na kujiona mmefika eti kisa tuuu mmechukua kombe mara 28 hivi hili nalo ni la kuliongelea kila leo? Wakati makombe mengine mmechukua hata member wengine hawajazaliwa humu kiasi kwamba mnaridhika na matokeo haya ya ligi kuu kimataifa mnatupwa huko.

Sasa unajisifu ww ni bingwa mara 28 hujulikani hata kwny ramani ya soka la Africa huoni kwamba unapoteza muda na mashabiki zako humu humu au wenzetu hamtaki soka la biashara soka la kiushindani?.yani nyie kombe la ligi kuu mkichukua mnanyanyua miguu juu hebu amkeni safari hii hatutaki aibu hayo makombe yenu yasadifu uhalisia.

Halafu hivi hapa nchini timu zetu zina kombe moja tuu ambalo linahesabiwa?.ukijumuisha yote Simba baba lao ana makombe mengi zaidi au nyie hayo hayawahusu? Mimi nakerwa sana mtu unamkuta anaanza kwa kusema sisis Yan'ga mabingwa wa kihistoria sasa nani anaetaka kujua historia hapa wakati hata shule somo la historia limefutwa. Tunachotaka kujua maendeleo ya timu hapa namaanisha timu kwa sasa inavyoperfom na matokeo yake,uwekezaji wake, na inatuwakilishaje kimataifa na sio porojo za sisi ni mabingwa kihistoria.

Hapa pia mjifunze kwa Simba hawadharau mechi au mashindano yoyote kama kuna mashindano ya kugombea kombe lolote inajitoa na sio kukamia ligi kuu ndo maana wanawazidi kwa makombe ya mjumuisho. Sema tuu upepo mbaya umeipitia timu yangu msimu huu tumeondoka na kombe la mapinduzi pekee.

Mwisho niwakumbushe msimu ujao utakua wa motoooo yani motooo mjiandae kisaikolojia msikariri kuwa kila msimu tunaachiana misimu 4 mi 4 safari hii huu mmoja unawatosha.

Adhuhuri njema.

Kalpana
YANGA BINGWA
 
Mbona ubingwa wenu wa kihistoria mlishindwa kuuendeleza kwa miaka 4 mfululizo Shadeeya
 
Timu yetu ilishatengenezwa kitambo sema ni vile msimu ulikua mbaya tuu na unajua wazi kabisa ratiba ilivyokua ngumu kwetu. Hivyo kupanga ni kuchagua na tumechagua kuchukua kombe msimu ujao wala sio maumivu.
Sawa Mtani kama huna maumivu tukutane Msimu ujao. 🤝
 
Back
Top Bottom