Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Chei chei!
Timu ya Yanga inakwenda kuumaliza mwendo katika kombe la waliofeli kwani wanakwenda kukutana na miamba mitatu ambayo isingependa kukutana nayo. Yanga amemaliza kama kinara wa kundi Dada....ila anakwenda kukumbana na hatari kubwa mbele yake kwani alitegemea labda atapata vibonde ambao watashika nafasi ya pili kwenye kundi A,b na c ila mambo yamekuwa ndivyo sivyo kwani nafasi za pili zimeshikwa na wauaji...
Nafasi ya pili kundi A imeshikwa na miamba ya Algeria, USM Alger, kundi B imekamatwa na miamba ya soka ya Nigeria ambao waliwatoa Yanga katika kombe la klabu bingwa Afrika kwa kuibugiza mabao nyumbani na ugenini, naizungumzia RIVERS UNITED huku kundi C nafasi ya pili ikikamatwa na miamba ya soka ya nchini Misri, Pyramids fc.
Kiufupi natanguliza salamu za rambirambi kwa Eng.Hersi na timu yake nawaambia asanteni kwa kushiriki katika michuano ya kombe la shirikisho afrika.Tuonane tena msimu ujao.