Yanga na Singida Big Stars kubadilishana wachezaji

Yanga na Singida Big Stars kubadilishana wachezaji

Wenye Akili tunajua kuwa Singida Big Stars ni Yanga SC B hivyo hapa hakuna Kipya Kwetu.

Baada ya kuona Simba SC ina Mzungu Dejan na Wao pia wanalazimisha wawe na Mzungu wao yaani ni Full Kuigana tu kama walivyotuiga Simba Day nao wana ( wakaja ) na Siku ya Wananchi.
Huyu si mzungu ni mwafrika mwenzetu mbrazil ni kama Neymar tu...sasa utasema Neymar ni mzungu?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Hebu mpunguze wivu basi! Mbona na nyinyi mliuziwa Habib Kiyombo baada ya kupanda dau? Iweje nongwa kwa Yanga kufanya mabadilishano na huyo Mbrazil?

Halafu mbona mnasahau mapema hivi! Kipindi kile mmiliki wa Azam FC, na ambaye ni mwanachama wa simba! Alishawahi pia kuwa kiongozi wenu miaka ya nyuma;

alipowapa wachezaji takribani wanne kwa mkupuo (Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni na John Bocco) kiasi cha kuwafanya muwe mabingwa kwa miaka minne mfululizo! Tulimsema kwa namna yoyote ile?

Let us be fair sometimes. Mwigulu Nchemba hana tofauti na mmiliki wa Azam FC.
Hapana, Mwigulu na mmiliki wa Azam FC wana tofauti kubwa sana, sijawahi kumuona huyo mmiliki wa Azam FC popote akipiga kelele yeye ni fan wa Simba SC, kama Mwigulu anavyofanya..

Juzi wakati akisoma bajeti bungeni, maneno ya kuisifia Yanga SC yalikuwa mengi zaidi ya mambo yanayohusu wizara yake, yule ni mnazi aliyepitiliza.
 
Punguza mihemko, huyo Kyombo mwenyewe aliwaomba Singida Big Starz wamuache aende Simba SC timu kubwa Tanzania,ndio wakaona aibu wakamuachia, walijua hata kama wangemgomea Simba SC tusingekuwa na hasara yoyote.
😂😂😂 kyombo kwenda kwa makolo kumbe aliomba 😂😂😂. Ila yanga kumsajiri mchezaji wa singida stars nongwa 😂😂
#wachawifc#
 
Hapana, Mwigulu na mmiliki wa Azam FC wana tofauti kubwa sana, sijawahi kumuona huyo mmiliki wa Azam FC popote akipiga kelele yeye ni fan wa Simba SC, kama Mwigulu anavyofanya..

Juzi wakati akisoma bajeti bungeni, maneno ya kuisifia Yanga SC yalikuwa mengi zaidi ya mambo yanayohusu wizara yake, yule ni mnazi aliyepitiliza.
Lakini baadhi ya hizo sifa si zilikuwa na ukweli Bwashee! Mfano za kuwa Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Mabingwa wa Ligi kuu, na pia Mabingwa wa kombe la Shirikisho la Azam!

Yaani ni sawa na mimi hapa nikiamua kumsifia hadharani Irene Uwoya kama mwanamke mzuri na mrembo! Utasema nimepitiliza kumpa hizo sifa?
 
Hayo yote ni kwa mujibu wa Jemedari Said Kazumari. Kama itatokea kweli basi yatajirudia ya Feitoto alivyotolewa na Singida Utd kwenda Yanga.

View attachment 2319554
Sioni tatizo lolote juu ya hilo Kama litatokea, na wala sio mada ya kujadili hapa, makubaliano ya mikataba ya wachezaji husika yanahusu klabu na klabu sioni shida hapo
 
Pia ni simba b mbona waliwapa kyombo? Mnajitoaga ufahamu eti? Wangekaza kwa kyombo mngempata?
Kyombo alisaini sehemu mbili kwa tamaa kwa hiyo kwa vyovyote ilikuwa lazima aiachie moja, huyu anahamishwa
 
Mbona kawaida yao hao Singida Big Stars, enzi zile wakiitwa Singida Utd waliwapa Yanga SC Fei Toto halafu wao wakashuka daraja.

Mwigulu ni mshamba mmoja hivi mwenye kiherehere cha kumiliki timu akishapiga dili zake.
Kwani ni Kosa kisheria kumiliki timu ya mpira watanzania tunashida kubwa sana
 
Thank you yanga b singida kwa ushirikiano wenu,
Tunaomba mtupe na mangalo kabisa
 
Yaani unipe kokoto nikupe dhahabu????c undezi huo au????
Kama timu mbili zimekubaliana kubadilishana wachezaji, shida iko wapi? Maana hakuna tofauti na timu mbili hizo hizo kuamua kuuziana wachezaji.
 
Hapana, Mwigulu na mmiliki wa Azam FC wana tofauti kubwa sana, sijawahi kumuona huyo mmiliki wa Azam FC popote akipiga kelele yeye ni fan wa Simba SC, kama Mwigulu anavyofanya..

Juzi wakati akisoma bajeti bungeni, maneno ya kuisifia Yanga SC yalikuwa mengi zaidi ya mambo yanayohusu wizara yake, yule ni mnazi aliyepitiliza.
Mi sielewi ata hoja yenu ni ipi apo, Singida Kama wamefanya biashara ya mchezaji na yanga kuna tatizo gani apo? Mchezaji auzwe na singida alafu povu liwatoke wengine ni maajabu ya mwaka aya!!!
 
Mi sielewi ata hoja yenu ni ipi apo, Singida Kama wamefanya biashara ya mchezaji na yanga kuna tatizo gani apo? Mchezaji auzwe na singida alafu povu liwatoke wengine ni maajabu ya mwaka aya!!!
Hawa watu wana shida mpaka basi. Wanaumia utafikiri wana hisa kwenye hiyo timu ya Singida Big Stars!

Ya kwao yanawashinda, wanahangaika na mambo ya watu wengine!
 
Kyombo alisaini sehemu mbili kwa tamaa kwa hiyo kwa vyovyote ilikuwa lazima aiachie moja, huyu anahamishwa
Una uhakika alisaini sehemu mbili? Maana sisi tulimuona kwa mara ya kwanza akitambulishwa Singida Big Stars!

Na baadaye tukasikia kutoka kwa msemaji wa hiyo timu ya kwamba wamefikia makubaliano na klabu ya simba. Na kwa sababu wangependa pia huyo mchezaji kupata sehemu yanye malisho mazuri zaidi, wamemruhusu!

Sasa unataka tuamini maneno ya msemaji wa timu, au tukuamini wewe?
 
Lakini baadhi ya hizo sifa si zilikuwa na ukweli Bwashee! Mfano za kuwa Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Mabingwa wa Ligi kuu, na pia Mabingwa wa kombe la Shirikisho la Azam!

Yaani ni sawa na mimi hapa nikiamua kumsifia hadharani Irene Uwoya kama mwanamke mzuri na mrembo! Utasema nimepitiliza kumpa hizo sifa?
Hapana, tatizo la mahaba ya Mwigulu kwa Yanga SC yameanzia enzi zilee za Fei Toto hata mwaka siukumbuki!
 
Mi sielewi ata hoja yenu ni ipi apo, Singida Kama wamefanya biashara ya mchezaji na yanga kuna tatizo gani apo? Mchezaji auzwe na singida alafu povu liwatoke wengine ni maajabu ya mwaka aya!!!
Hiyo biashara unayo risiti utuwekee hapa?
 
Back
Top Bottom