Elpaul
JF-Expert Member
- Jan 19, 2018
- 922
- 692
Mchezaji yeyote ambaye anaitakia mema klab yake ya Young/mdogo African anatambua umuhimu wa mechi Hiyo hata bila kuambiwa Chochote.Ukiwa umecheza Mpira au unajua Kuuchambua Mpira au umesomea Ukocha basi nina uhakika wa 100% kuwa utanielewa GENTAMYCINE kwa hili ANGALIZO langu Tukuka kwa Yanga SC kuelekea Mechi yao muhimu na ya Kimaamuzi Jumamosi ijayo.
Nawaomba mno Yanga SC hasa Kocha wao Mkuu na Benchi la Ufundi wasiwaambie Wachezaji wao kuwa hii ni Mechi muhimu sana Kwao bali wawaambie tu kuwa hiyo Mechi ni ya Kawaida na waacheze bila Presha. Wakifanya hivi itawasaidia mno Kushinda Kiuwepesi.
Nawaomba sana Mashabiki wa Yanga SC waache Kuwatwisha Wachezaji mzigo (Mitandaoni na Mazoezini) mkubwa wa kuwataka Wajitoe hadi tone lao la mwisho la Jasho kwani watasababisha Wachezaji kujawa na Hofu na kuondoa Umakini.
Uongozi wa Yanga SC umtake mwana Simba SC 100% na mwana Yanga SC 0% Haji Manara atulie hasa kwa Kauli zake za Kuwajaza Mzigo wa Kimajukumu Wachezaji hasa kuelekea hiyo Mechi kwani Kiufundi kwa kufanya Kwake hivyo anawaharibu na watajiona wana Lundo la Matarajio kutoka kwa Watu maarufu na wenye Ushawishi.
Yanga SC wawe makini sana Asante.