Yanga SC yavunja benchi lake la ufundi na kuachana na Kocha Mkuu, Cedric Kaze

Yanga SC yavunja benchi lake la ufundi na kuachana na Kocha Mkuu, Cedric Kaze

So disappointed...

Ni kama maamuzi ya kukurupuka hivi ukiwa na hasira, Kwa upande wangu naona "Benchi la ufundi" limeangushiwa jumba bovu, Kuna migogoro ndani ya uongozi wa juu kabisa na kwa baadhi ya wachezaji

Anyways ndio Yanga yetu acha ituue tu

Sent from my SM-J720F using JamiiForums mobile app
Pole sana mtani
 
Ubabaishaji tu huu, vipi kuhusu uongozi Wa timu unafaa kuendelea kuwepo!?
 
Kwangu mimi sidhani kama tatizo la Yanya ni Kocha...
Kwa mtazamo wangu wanalizunguka tatizo, kikosi walichonacho sio Bora, ndio maana kila siku wanapata sababu mpya.
Mwanzo ilikua marefa sasa ni benchi la fundi, ngoja tusubiri lawama zingine zitamwendea Nani.
 
Yanga wanataka kuwaaminisha Mashabiki wao na Wanachama kuwa wana wachezaji wa level za juu Timu imesajili wachezaji wa Mafungu ya nyanya mlitaka KAZE amfundishe nini mchezaji kama Nchimbi tangu aanze kucheza mpira timu zote alizopita hata Goli 15 hajawahi kufunga unataka afunge leo yupo Yanga ?? Sarpong, Yacouba, Fiston, Farid .........Mwambieni SENZO Awape ubingwa sasa na yule Engineer aliyewaaminisha ubingwa kama vile anacheza mpira yeye.
Kaze aondoke na watoto wa dada yake asiwaache.. SAIDO, FISTON.
 
Goli lenyewe lilofukuza benchi hili hapa.
 

Attachments

  • 157224227_120018326733006_7436983860762188926_n.mp4
    3.5 MB
Timu inaongoza ligi mnafukuza kocha. Nyie mbona mnatuchanganya mashabiki wa Simba?

Mi nahisi bado mnamtaka Morisson
 
Kwangu mimi sidhani kama tatizo la Yanya ni Kocha...
Kwa mtazamo wangu wanalizunguka tatizo, kikosi walichonacho sio Bora, ndio maana kila siku wanapata sababu mpya.
Mwanzo ilikua marefa sasa ni benchi la fundi, ngoja tusubiri lawama zingine zitamwendea Nani.
Kazi ya kocha ni nini na hawa wachezaji unadhani kawapendekeza nani kusajiliwa Yanga, kama siyo kaze
 
Uto kila mwaka wakiona ligi inakaribia kwisha wanafukuza kocha ili viongozi wawe huru kusajili wachezaji wanaowataka, wakimaliza kusajili ndio wanaleta kocha, kocha akija anakuta wachezaji wapya kibao anakabidhiwa awafundishe. Mpira hauendi hivyo

Mwenyekiti wenu Msolwa ni kocha kwa hiyo atatwaa mikoba ya Kaze, Mwakalebela na kitambi lake atamsaidia.
 
Back
Top Bottom