Yanga tumejifunza nini na uwezo wa kocha wa simba?

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Posts
2,180
Reaction score
1,291
UFUNDI WALIOUNESHA SIMBA kipindi cha kwanza hadi kufikia kupata bao la kuongoza ni tahadhali nzuri ya kujifunza kuelekea kuchukua bingwa mfululiizo. Huyu kocha wa SSC ni mzuri sana sana na inaonesha simba itaweza sana kuzifunga timu magoli mengi katika mechi zao kila watokapo uwanjani.

Hivyo kwa somo hilo Yanga inabidi kufanya ima faima kutotoka uwanjani bila ushindi wa magoli mengi katika kila mechi kujihami na uwezekano wa kupata bingwa kwa tofauti ya magoli.

Yanga ina kocha mzuri sana na mtaalamu wa kupindua meza hivyo washambuliaji wake lazima wapachike mabao mengi iwezekanavyo kila mechi wachezayo ili mwisho wa siku idadi ya magoli isije kutuanguasha.
 
Mkuu umeongea kweli tupu, huenda watu wasikuelewe, ni wazi kabisa ushindani wa mwaka huu ni mkubwa sana ni wakati sasa Nabii kuangalia uwezekekano wa kuwa na mfumo wa double straikers pale mbele.
 
Sijui ni kipi kilipelekea game kubadilika kipindi cha pili, haraka haraka nahisi ni kumpeleka Azizi K namba 10, na kuingia kwa Morisson. Hii Game Simba alikuwa anaimaliza first half.

Jamaa eneo la kiungo alituweza, feisal ni kama hakuna mchezoni na Sure Boy, Aucho alikaba zaidi. Simba aliingia na 4-5-1, hii iliipa wakati mgumu zaidi Yanga pale kati. Kwa mbinu tu, Simba kocha alianza vyema, pengine kwenye sub ndipo alipochemka.
 
Umesema kweli, kipindi cha kwanza; movement, reaction na pressing waliyokuwa wanafanya Simba wakati hawana mpira zilitunyima nafasi ya kuchezea mpira.

Sio wa kuwachukulia poa kwa kuwa tumewafunga.

Mpira wao wa kipindi cha kwanza uwe kama wake-up call kwa Yanga na bench la ufundi.
 
Simba iliizidi Yanga kwa kila kitu katika kipindi cha kwanza. Ni kikubwa ni kiungo ndio kilichozidiwa, pamoja na kwamba watu wanampongeza Nabi kwa kufanya sub lakini kwa upande wangu naweza sema msaada pekee wa Yanga kupata ushindi ni uzembe wa wachezaji wa Simba. Kipindi cha kwanza walipoteana mazima ilipaswa wapate magoli zaidi ya moja na kuumaliza mchezo. Kocha wa Yanga anapaswa ajifunze kuchukua maamuzi ya mapema pindi anapoona mapungufu. Asikariri eti mpaka halftime ndipo uje na plan B ya mchezo

Yanga tulishinda kutokana na uzembe wao wachezaji wa Simba kipindi cha kwanza.
 
Simba hatuko vzr. Tunahitaji CDM na striker wazuri. Kuhusu kocha ni mapema sana kumpa sifa. Anaweza akawa mzuri sana lakini ni mapema.
 
Simba iliizidi Yanga kwa kila kitu katika kipindi cha kwanza. Ni kikubwa ni kiungo ndio kilichozidiwa, pamoja na kwamba watu wanampongeza Nabi kwa kufanya sub lakini kwa upande wangu naweza sema msaada pekee wa Yanga kupata ushindi ni uzembe wa wachezaji wa Simba. Kipindi cha kwanza walipoteana mazima ilipaswa wapate magoli zaidi ya moja na kuumaliza mchezo. Kocha wa Yanga anapaswa ajifunze kuchukua maamuzi ya mapema pindi anapoona mapungufu. Asikariri eti mpaka halftime ndipo uje na plan B ya mchezo

Yanga tulishinda kutokana na uzembe wao wachezaji wa Simba kipindi cha kwanza.
Simba walifanya uzembe upi? Vp Yanga haikufanya uzembe Simba kupata goli kipindi cha kwanza??

KOLO unajifanya YANGA.
 
UFUNDI WALIOUNESHA SIMBA kipindi cha kwanza hadi kufikia kupata bao la kuongoza ni tahadhali nzuri ya kujifunza kuelekea kuchukua bingwa mfululiizo. Huyu kocha wa SSC ni mzuri sana sana na inaonesha simba itaweza sana kuzifunga timu magoli mengi katika mechi zao kila watokapo uwanjani.

Hivyo kwa somo hilo Yanga inabidi kufanya ima faima kutotoka uwanjani bila ushindi wa magoli mengi katika kila mechi kujihami na uwezekano wa kupata bingwa kwa tofauti ya magoli.

Yanga ina kocha mzuri sana na mtaalamu wa kupindua meza hivyo washambuliaji wake lazima wapachike mabao mengi iwezekanavyo kila mechi wachezayo ili mwisho wa siku idadi ya magoli isije kutuanguasha.
Yanga haiwezi kujifunza Kwa walioshindwa. Simba ndo wanatakiwa wajifunze Kwa Yanga.
 
Sijui ni kipi kilipelekea game kubadilika kipindi cha pili, haraka haraka nahisi ni kumpeleka Azizi K namba 10, na kuingia kwa Morisson. Hii Game Simba alikuwa anaimaliza first half.

Jamaa eneo la kiungo alituweza, feisal ni kama hakuna mchezoni na Sure Boy, Aucho alikaba zaidi. Simba aliingia na 4-5-1, hii iliipa wakati mgumu zaidi Yanga pale kati. Kwa mbinu tu, Simba kocha alianza vyema, pengine kwenye sub ndipo alipochemka.
Na ile formation ya Yanga kipindi Cha pili angeanza nayo kipindi Cha kwanza, nadhani Simba angekula hata goli 4
 
Mimi ni shabiki wa Simba nilivyoona kile kikosi na jinsu tulivyocheza nkasema kocha tuliye nae ni kocha mkubwa sana kwwnye swala la mbinu sema mashabiki oya oya hawawezi kuliona ilo kisa matokeo ys mwisho yalivyokua

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app

Tatizo kubwa la kocha wa Simba ni sub aliyofanya. Kumtia Kanoute, chama na Kibu. Hawa walikuwa ameubeba mchezo pale Katikati. Kanoute alikuwa anaharibu sana pale Katikati, chama alikuwa anapenyeza. Kibu alikuwa na power, nguvu
 
Sijui ni kipi kilipelekea game kubadilika kipindi cha pili, haraka haraka nahisi ni kumpeleka Azizi K namba 10, na kuingia kwa Morisson. Hii Game Simba alikuwa anaimaliza first half.

Jamaa eneo la kiungo alituweza, feisal ni kama hakuna mchezoni na Sure Boy, Aucho alikaba zaidi. Simba aliingia na 4-5-1, hii iliipa wakati mgumu zaidi Yanga pale kati. Kwa mbinu tu, Simba kocha alianza vyema, pengine kwenye sub ndipo alipochemka.
Kanoute substitution ndo ilimaliza game watu wanamlaumu ila alikuwa sahihi kumtoa kwasababu alikuwa na kadi ya njano na angeendelea angepata red card maana alikuwa anafanya makosa na rafu zinazojirudia ila kuwatoa kanoute na mkude ndani ya mda mchache ndo mpira ulibadilika hapo yule kanoute mtu sana akipunguza kucheza rafu atakuwa vizuri ni kama feisal wakati anaanza kucheza yanga alikuwa anacheza rafu kama kanoute.
 
Umesema kweli, kipindi cha kwanza; movement, reaction na pressing waliyokuwa wanafanya Simba wakati hawana mpira zilitunyima nafasi ya kuchezea mpira.

Sio wa kuwachukulia poa kwa kuwa tumewafunga.

Mpira wao wa kipindi cha kwanza uwe kama wake-up call kwa Yanga na bench la ufundi.
Moja kati ya vitu ambavyo vimebadilika kwa simba ni kucheza vizuri wakiwa hawana mpira man to man na back up ya mtu mmoja nyuma iliwasaidia sana kipindi cha pili.
 
Na ile formation ya Yanga kipindi Cha pili angeanza nayo kipindi Cha kwanza, nadhani Simba angekula hata goli 4
Wakati huo anakula nne mkude na kanoute wako wapi kilichobadilisha game ni sub za simba sio za yanga yaani kisa yanga imeshinda basi ndo mnajikuta al ahly ngojeni pataonekana panapovuja.
 
Pataonekana lini tena wakati pasha vuja
 
Wakati huo anakula nne mkude na kanoute wako wapi kilichobadilisha game ni sub za simba sio za yanga yaani kisa yanga imeshinda basi ndo mnajikuta al ahly ngojeni pataonekana panapovuja.
Wakati linakaa la kwanza walikuwa wapi hao watu?
 
Back
Top Bottom