Yanga tumeshaingia kwenye mtego wa wachambuzi uchwara tayari

Yanga tumeshaingia kwenye mtego wa wachambuzi uchwara tayari

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
16,911
Reaction score
28,469
I salute you kinsmen.

Rejea uzi wangu uliopita niliposhauri kuwa tatizo la yanga hasa ni mkurugenzi wa ufundi bwana Moalim aliyeondoka..

Leo najaribu kuelewesha deep sana. Well let's goo.

Huyo bwana kitaalamu ni kocha kabisa na ana vigezo vya kusimama kwenye pitch line.

Huyu alikuwa na uzoefu na mechi na viwanja vyetu hivi the likes of sokoine.

Alifundjsha azam kisha KMC kisha yanga.

Huyu ndio alibeba ile identity ya yanga kumiliki mpira na soka safi huku magoli yakiwa ya kutosha .

Hamdi alipokuja hakupata shida kabisa jamaa akahamishiwa benchi pale wakawa wanasaidiana na Hamdi yaani ikawa kama kumsukuma mlevi.

Kwa msiojua kazi ya mkurugenzi wa ufundi ni hii.

Anabeba project ya team na anashirikiana kwa ukaribu na kocha mkuu kuhusu wachezaji, changamoto na namna ya ku overcome!
Kwa ulaya hawa ni watu muhimu sana.

Kwahiyo basi.
Folz amepata shida sana sababu amekuja na benchi jipya na mkurugenzi wa ufundi mpya ambaye naye anajribu kucope na team! Kiufupi wote wageni tu!

Benchi zima mtu mmoja tu meneja walter ndiye mwenyeji sasa huoni jamaa alipata ugumu sana??? Angemkuta moalim kazi ingekuwa nyepesi kwake!

Mfano folz alienda kucheza mbeya huku akiwa hajui hali ya uwanja husika na akajaribu kuweka mpira chini bado akafeli akahamia juu ndio kabisa!

Hakuna na homework nzuri, hili mkurugenzi wa ufundi angelimaliza mapema!

Tutofautishe hivi vitu, identity na formation.

Tukisema identity tunamaanisha nature ya Tema inachezaje bila hata kuangalia mfumo!
Mfano yanga soka Letu ni kumiliki mpira no matter what!

Alikuja Nabi akaweka mizizi kuhusu hilo, akaja gamondi nako ikawa hivyo hivyo tunamiliki mpira na magoli zaidi!

Gamondi hakupenda kutumia mawinga kama Nabi asilia zaidi Gamondi alipenda kutumia viungo lakini mpira ulikuwa ule ule wa kumiliki sana uwanja!

That's yanga identity!
Sasa tukija hapo kwenye hizo formation ndio sasa watu wanapoongelea hilo wakidhani ndio identity

Gamondi alikuwa akitumia 4-3-3 muda mwengine mpaka 3-4-3

Lakini bado soka lilibaki lile lile kumiliki mpira sana!

Guys hapa ndio tulibugi leo hata akija nabi tena ataanguka tu lazima maana atakutana na kazi ngumu sana pale!

Tukumbuke yanga kwa sasa inacheza for the sake of uwezo wa mchezaji mkoja mmoja tu!

Na pamba walituonyesha hilo ingawa tukashinda na kisha mbeya city wakapigilia msumari wa mwisho.!

Soka la folz ni pasi ndefu na team isikae na mpira sana! Sasa unadhani nani angemshauri namna ya kucheza? Injinia? No way . Matokeo yanga imekuwa ikicheza hovyo sasa kuliko hata pamba jiji!

Barcelona bado wanacheza kwa identity yao ile ile kilichobadilika ni mfumo tu pekee.

Kuna team yenye identity strictly kukiko Barcelona?? Wao Miaka yote wana namna yao ya kuendesha team ikiwemo kuchukua wachezaji kutoka La masia je Hans flick hajafanya hivyo??

Guys tutulie vizuri ingawa nakiri kila binadamu ana maoni yake ila that's a fact

Folz kashatimuliwa ila tayari tumeingia kwenye mkenge wa kutimua timua makosa acha tuone atakayeletwa angalau Hamdi akirudi lakini sio Nabi tena!
ngara23 Tate Mkuu Wakipekee
vibertz Aleyn
Jamaa ameshatimuliwa tupumzike sasa tusubiri matokeo ya kocha mpya

Its Pancho
images (6).jpeg
 
Kwa sasa yanga inacheza kwa uwezo wa mchezaji mmoja mmoja tu na si vinginevyo!
 
Mfano folz alienda kucheza mbeya huku akiwa hajui hali ya uwanja husika na akajaribu kuweka mpira chini bado akafeli akahamia juu ndio kabisa!🤣🤣🤣🤣.
Yaani utasema folz ndo anayechezaaa
 
Yaani utasema folz ndo anayechezaaa
Wachezaji wanacheza wanapotaka au kocha ndiyo anasema weka mpira chini au piga mipira mirefu?

Hukusikia game ile alikuwa napiga kelele anasema "on the ground! On the ground!"

Acha ushabikiwa kitoto kijana
 
Wamechelewa sana kumtimua tapeli Folz.

Huyu baada ya mechi 3 tu alitakiwa kutimuliwa.

Yanga sio timu ya majaribio.
Tayari kashaenda

Kilichofanya ionekane ana soka bovu ni sababu ya kutoka nje ya identity ya yanga tuliyoizoea siku zote kumiliki mpira sana

And of course ni soka bovu tumecheza
 
images (6).jpeg

Huyu ndio alikuwa mhimili mkubwa kwenye mafanikio ya Hamdi kwa muda mfupi aliokuja akakielewa kikosi haraka sana sababu ya huyu jamaa.

Unapata package kubwa ndani yake kocha na mtaalamu wa ufundi .

Tulimuacha yule video analyst msauzi yule tall na folz kaja na benchi lake ila video analyst wake alishindiwa hata kumpa ABC za huko mbeya uwanja ule mbaya na mbovu..
 
Ila niwe tu mkweli siku namuona Romain Folz kwa mara ya kwanza kwenye picha, eti ndiyo kocha mpya wa Yanga! Nilishangaa sana! Kuanzia muonekno wake, umri wake, CV yake ya kufundisha mpira nayo ilikuwa haieleweki kivile!! Aisee uongozi wa Yanga ulicheza kamari ya hovyo sana.

All in all, naamini wamejifunza kutokana na makosa yao. Na bila shaka kocha anayekuja atakuwa siyo mgeni tena kama huyu aliye timuliwa.
 
Tayari kashaenda

Kilichofanya ionekane ana soka bovu ni sababu ya kutoka nje ya identity ya yanga tuliyoizoea siku zote kumiliki mpira sana

And of course ni soka bovu tumecheza
Yeah soka bovu sana.

Yanga hatujazoea kucheza hovyo hata tukifungwa.

Wallahi tungeendelea nae tungeishia makundi.
 
Ila niwe tu mkweli siku namuona Romain Folz kwa mara ya kwanza kwenye picha, eti ndiyo kocha mpya wa Yanga! Nilishangaa sana! Kuanzia muonekno wake, umri wake, CV yake ya kufundisha mpira nayo ilikuwa haieleweki kivile!! Aisee uongozi wa Yanga ulicheza kamari ya hovyo sana.

All in all, naamini wamejifunza kutokana na makosa yao. Na bila shaka kocha anayekuja atakuwa siyo mgeni tena kama huyu aliye timuliwa.
Sijui hata walizingatia nini kumpa timu Folz.

Hata mimi nlishangaa sana.

Dogo kama Folz anayebahatisha bahatisha kumpa timu kama Yanga ni kuishusha thamani timu yetu.

Viongozi wawe makini next time.
 
View attachment 3484069
Huyu ndio alikuwa mhimili mkubwa kwenye mafanikio ya Hamdi kwa muda mfupi aliokuja akakielewa kikosi haraka sana sababu ya huyu jamaa.

Unapata package kubwa ndani yake kocha na mtaalamu wa ufundi .

Tulimuacha yule video analyst msauzi yule tall na folz kaja na benchi lake ila video analyst wake alishindiwa hata kumpa ABC za huko mbeya uwanja ule mbaya na mbovu..
Vipi kuhusu kocha mpya?

Nani anaweza kuchukua nafasi ya Folz?

Kuna tetesi ni Ramovic.
 
Wachezaji wanacheza wanapotaka au kocha ndiyo anasema weka mpira chini au piga mipira mirefu?

Hukusikia game ile alikuwa napiga kelele anasema "on the ground! On the ground!"

Acha ushabikiwa kitoto kijana
Mara ya mwisho kumfunga mbeya city ilikuwa ni LINI?
 
Sijui hata walizingatia nini kumpa timu Folz.

Hata mimi nlishangaa sana.

Dogo kama Folz anayebahatisha bahatisha kumpa timu kama Yanga ni kuishusha thamani timu yetu.

Viongozi wawe makini next time.
Binafsi nimepata wakati mgumu sana kumtetea huyu dogo! Tena kwa maslahi ya klabu.

Yaani unakuta eti timu kama Azam inamuajiri Florent Ibenge, kocha mwenye CV iliyoshiba kwa soka la Afrika! Halafu Yanga inamuajiri kocha ambaye tunaambiwa sijui alikuwa ni kocha msaidizi wa timu gani huko!!
 
Vipi kuhusu kocha mpya?

Nani anaweza kuchukua nafasi ya Folz?

Kuna tetesi ni Ramovic.
Inawezekana akawa yeye
Maana yeye na Hamdi wote wanapumulia mashine huko hata hivyo huyu Ramovich alitutolea shit aliposepa hafai
 
Binafsi nimepata wakati mgumu sana kumtetea huyu dogo! Tena kwa maslahi ya klabu.

Yaani unakuta eti timu kama Azam inamuajiri Florent Ibenge, kocha mwenye CV iliyoshiba kwa soka la Afrika! Halafu Yanga inamuajiri kocha ambaye tunaambiwa sijui alikuwa ni kocha msaidizi wa timu gani huko!!
Mkuu jamaa alikuja yanga kujenga CV wakati ibenge ameenda azam kushindana kama kawaida yake.
 
Folz hateteki mkuu, Gamondi alipokuja Yanga hakumkuta huyo Mollin lakini angalia mpira wake. Swala la aina ya mpira sio mkurugenzi wa ufundi ndio anapanga bali ni mfumo wa kocha mwenyewe na staili yake ya uchezaji. Hata angekuwepo huyo Mollin asingesaidia kitu kwasababu huo ndio aina ya mpira wa huyo kocha.

Ukitaka kujua Mollin hapangi aina ya uchezaji wa timu (falsafa) angalia Mollin alivyokuwa na Ramovich kisha alivyokuwa na Miloud Hamdi uchezaji wa timu haukulingana
 
Swala la aina ya mpira sio mkurugenzi wa ufundi ndio anapanga bali ni mfumo wa kocha mwenyewe na staili yake ya uchezaji.
Elewa mkuu wangu
Identity tunazungumzia gamondi sasa si ilitokea yanga walitafuta kocha ambaye mfumo wake ni unaendana na Identity ya team?

Tofautisha namna ya kucheza na Identity

Gamondi nimeelezea wazi alikuwa anapenda kutumia viungo kuliko.mainger nature kabisa lakini bado falsafa yake ilikuwa kumiliki mpira sasa sikuelewi unapobisha kitu

Ukiskia project ni nini? Project ni ya team husika inayobebwa na mkurugenzi kocha aifuate ikiwemo Identity ya team husika tofautisha mfumo na vitu kama hivyo hayo ni ya kocha ndugu..

Sijamtetea folz kama umeona nimesema kuwa soka lake halivutii sababu mfano wewe unataka acheze kama gamondi au nabi kwanini??? That's yanga identity kama unabisha

Basi sasa kwanini usiamini soka la Folz? Kama hata yanga wenyewe wamemtimua kwa kuona anaharibu Identity ya team iliyozoeleka??
 
Back
Top Bottom