Yanga tumeshaingia kwenye mtego wa wachambuzi uchwara tayari

Yanga tumeshaingia kwenye mtego wa wachambuzi uchwara tayari

Wachezaji wanacheza wanapotaka au kocha ndiyo anasema weka mpira chini au piga mipira mirefu?

Hukusikia game ile alikuwa napiga kelele anasema "on the ground! On the ground!"

Acha ushabikiwa kitoto kijana

Hujatambua kitu hapa
Hatulaumu sare kabisa kabisa hatujaumia na sare

Kilichotuuma ni mpira uliochezwa mbovu sana tulicheza
Sababu timu mbovu sio uwanja.mbona tulishasema muda kuwa yanga hii ni mbovu ina shinda Kwa uwezo binafsi wa wachezaji na Wala sio mbinu za kocha wewe ilikuwa wapi?shida ya yanga ni injinia hersi ana amini mpira unachezwa zaidi nje ya uwanja kuliko uwanjani.kocha kwake ni ziada tu.
 
Folz hateteki mkuu, Gamondi alipokuja Yanga hakumkuta huyo Mollin lakini angalia mpira wake. Swala la aina ya mpira sio mkurugenzi wa ufundi ndio anapanga bali ni mfumo wa kocha mwenyewe na staili yake ya uchezaji. Hata angekuwepo huyo Mollin asingesaidia kitu kwasababu huo ndio aina ya mpira wa huyo kocha.

Ukitaka kujua Mollin hapangi aina ya uchezaji wa timu (falsafa) angalia Mollin alivyokuwa na Ramovich kisha alivyokuwa na Miloud Hamdi uchezaji wa timu haukulingana
Haoa bado unatoka nje ya concepts kabisa

Nadhani hukufuatilia vizuri msimu ule kwanza unajua kuwa Moalim anafanya kazi na Ramovich now?.unadhani kwanini alimchukua?

Jamaa alikuwa ni msaada mkubwa sana unadhani pale benchi alikuwa anakaa tu?

Mwanzo alikuwa anashinda ofisini tu yanga wakamuweka awe anakaa benchi sio wajinga Moalim ni kichwa anampa ushauri Hamdi kuhusu sub nk

Mfano mechi ile ya mwisho wa ligi na simba sub ile ya mzize ni Moalim ndio alimshauri kocha Hamdi na mzize akaingia na kubadilisha matokeo.

Uzuri muda utaongea tu
 
Sababu timu mbovu sio uwanja.mbona tulishasema muda kuwa yanga hii ni mbovu ina shinda Kwa uwezo binafsi wa wachezaji na Wala sio mbinu za kocha wewe ilikuwa wapi?shida ya yanga ni injinia hersi ana amini mpira unachezwa zaidi nje ya uwanja kuliko uwanjani.kocha kwake ni ziada tu.
Huu ulioleta sio uchambuzi ni ushabiki tu

Tueleze yanga mbovu sehemu gani au eneo gani?

Na je team gani bora kuzidi yanga hapa Tanzania? Kama yanga akiwa mbovu na wengine si wanakuwa taabani kabisa?
 
Mkuu, unamzungumzia huyo jamaa kana kwamba hakuwahi kufeli Azam na KMC... Kana kwamba kabla yeye hajaja basi Yanga haikuwahi kufanya vema
 
Mkuu, unamzungumzia huyo jamaa kana kwamba hakuwahi kufeli Azam na KMC... Kana kwamba kabla yeye hajaja basi Yanga haikuwahi kufanya vema
Kule alikuwa kocha tu
Azam ilikuwa Haina resources sahihi ikiwemo wachezaji

Akaenda KMC sasa kmc pale si hata aje pep bado hawawezi kufanya vizuri ni mid table team.
 
Elewa mkuu wangu
Identity tunazungumzia gamondi sasa si ilitokea yanga walitafuta kocha ambaye mfumo wake ni unaendana na Identity ya team?

Tofautisha namna ya kucheza na Identity

Gamondi nimeelezea wazi alikuwa anapenda kutumia viungo kuliko.mainger nature kabisa lakini bado falsafa yake ilikuwa kumiliki mpira sasa sikuelewi unapobisha kitu

Ukiskia project ni nini? Project ni ya team husika inayobebwa na mkurugenzi kocha aifuate ikiwemo Identity ya team husika tofautisha mfumo na vitu kama hivyo hayo ni ya kocha ndugu..

Sijamtetea folz kama umeona nimesema kuwa soka lake halivutii sababu mfano wewe unataka acheze kama gamondi au nabi kwanini??? That's yanga identity kama unabisha

Basi sasa kwanini usiamini soka la Folz? Kama hata yanga wenyewe wamemtimua kwa kuona anaharibu Identity ya team iliyozoeleka??
Hoja yako ipo kwa Mollin kutokuwepo kuwa ndio chanzo cha Folz kufeli. Jambo ambalo mimi nakukatalia.
 
Kule alikuwa kocha tu
Azam ilikuwa Haina resources sahihi ikiwemo wachezaji

Akaenda KMC sasa kmc pale si hata aje pep bado hawawezi kufanya vizuri ni mid table team.
Kwamba akiwa kocha tu haiwezi kufanya kazi ipasavyo katika timu hadi awe mkurugenzi wa ufundi ndio timu ifanye vizuri? Hujui kama kuwa kocha ndio una husika moja kwa moja na timu?
 
Sijui hata walizingatia nini kumpa timu Folz.

Hata mimi nlishangaa sana.

Dogo kama Folz anayebahatisha bahatisha kumpa timu kama Yanga ni kuishusha thamani timu yetu.

Viongozi wawe makini next time.
Eng.Hersi alishauriwa na Kocha Arsene Wenger amchukue Folz.
Unajua huyu Folz Ni mkufunzi anayetambuliwa na kutumiwa na FIFA kufundisha makocha.
 
Kule alikuwa kocha tu
Azam ilikuwa Haina resources sahihi ikiwemo wachezaji
Kwahiyo tumekubaliana hata Folz akipata resources sahihi (wachezaji) hatamuhitaji tena huyo Msomali, si ndivyo?
Na kama sivyo...
Hiyo KMC na Azam wakipata kocha afu wamrejeshe huyo msomali aje afanye kama alivyofanya Yanga, zingetoboa?
 
Kwamba akiwa kocha tu haiwezi kufanya kazi ipasavyo katika timu hadi awe mkurugenzi wa ufundi ndio timu ifanye vizuri? Hujui kama kuwa kocha ndio una husika moja kwa moja na timu?
Tufanye simple tu mchukue gamondi mpeleke KMC akuoe ubingwa kama rahisi

Then twende sawa
 
Kwahiyo tumekubaliana hata Folz akipata resources sahihi (wachezaji) hatamuhitaji tena huyo Msomali, si ndivyo?
Na kama sivyo...
Hiyo KMC na Azam wakipata kocha afu wamrejeshe huyo msomali aje afanye kama alivyofanya Yanga, zingetoboa?
Yanga tayari ina resources wachezaji sahihi resource iliyokosekana ni Moalim tu iwe kama simu uliopita
 
Mimi kama mwanachama wa Yanga nilishaandika Uzi hapa kuwa Folz ni tapeli na na coach kilaza duniani

Mimi naipenda Yanga Kwa dhati ila huyo Coach hapana

Hajui afanye Nini? Wakati Gani?
Hana falsafa mf. Mpira wa kasi, counter attacks, kuchezesha wings n.k

Yaani Yanga tunacheza kama timu ya shule

Huyu Coach akikutana na Ahly yenye Ali Malool, Rami Rabia, Reda Slim, Mohamed Hany, kalaba. Unadhani watamuuliza maswali ya Mbeya City ambayo hakuyajibu

Huko mbele Kuna makocha anakuja na mbinu unabaki unashangaa hapa huo mtego unautoaje

Eng Hersi Said amenisikilza amefukuza takataka
 
Ila niwe tu mkweli siku namuona Romain Folz kwa mara ya kwanza kwenye picha, eti ndiyo kocha mpya wa Yanga! Nilishangaa sana! Kuanzia muonekno wake, umri wake, CV yake ya kufundisha mpira nayo ilikuwa haieleweki kivile!! Aisee uongozi wa Yanga ulicheza kamari ya hovyo sana.

All in all, naamini wamejifunza kutokana na makosa yao. Na bila shaka kocha anayekuja atakuwa siyo mgeni tena kama huyu aliye timuliwa.
Kila mwenye akili timamu aliona hilo. Derby tulicheza within first 10 minutes, kuna muda timu ilikuwa haieleweki.

Mimi naona kumchukua folz kuna ujanja wa upigaji ulitumika. Huwezi chukua kocha wa 34 years kumkabidhi timu kubwa zaidi Afrika Mashariki na kati.
 
Folz hateteki mkuu, Gamondi alipokuja Yanga hakumkuta huyo Mollin lakini angalia mpira wake. Swala la aina ya mpira sio mkurugenzi wa ufundi ndio anapanga bali ni mfumo wa kocha mwenyewe na staili yake ya uchezaji. Hata angekuwepo huyo Mollin asingesaidia kitu kwasababu huo ndio aina ya mpira wa huyo kocha.

Ukitaka kujua Mollin hapangi aina ya uchezaji wa timu (falsafa) angalia Mollin alivyokuwa na Ramovich kisha alivyokuwa na Miloud Hamdi uchezaji wa timu haukulingana
Upo sahihi kwa 100% ila jamaa atakuja kukupinga, ana ubishi fulani ulioambatana na ujuaji.
 
Kwamba akiwa kocha tu haiwezi kufanya kazi ipasavyo katika timu hadi awe mkurugenzi wa ufundi ndio timu ifanye vizuri? Hujui kama kuwa kocha ndio una husika moja kwa moja na timu?
Mleta mada ana hoja nyepesi sana.
 
Back
Top Bottom