Yanga vs Rivers United (0-1) | CAFCL | Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam

Hiki ni kikosi cha TPL pekee, wakikutana na mwarabu wanalambishwa mchanga nje-ndani.
 
Wadau nadhani Wote tunajua Mfadhili wetu Amemsajili Mchezaji HAJI MANARA kwa Ajili ya kuimarisha Timu yetu kwenye Mashindano haya ya KIMATAIFA
Kufungwa leo LAWAMA ZOTE Apewe KOCHA kwa Kutomchezesha huku Akijua ni Mchezaji HATARI sana
Angalia Orodha ya Wachezaji aliowapanga Hata wale wa AKIBA HAYUPO

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Mnaamini porojo kuliko uhalisia. Timu lenu bovuuu. GSM wapiga dili tu.
Au unataka wasilipe mishahara ya wachezaji na makocha

Au unataka wasilipe kambi ya timu pale Avic town

Au unataka wafanye usajili wa wachezaji kutoka ulaya

Au unataka wasilipe gharama za usafiri za timu

Ila point ambayo leo ukisema kwamba Yanga hawatakiwi kusajili wachezaji wengi kila msimu ningekuelewa na hicho ndo kinatucost kwa kukosa clear pattern ya timu yetu

Kwa hiki kikosi cha sasa tukitaka kusajili tena ni wachezaji wawili au watatu tu na sio kuvunja tena timu
 
Kwa dirisha la usajili lini tena twende tukasagule kule kongo
 
Nakubaliana na wewe, yanga Wana wachezaji wanaoweza kunyang'anya au kupokonya mipira na sio kucheza mpira.
Viungo wachezeshaji bado kabisa (8, 10, na 11) nguvu nyingi akili ya mpira kidogo.
 
Young Africans walikataa kupeleka kikosi bora Kagame Challenge Cup 2021 na kuitumia michuano hiyo kama pre season ya kutayarisha timu na wachezaji.

Sasa tunaona timu zilizokuwa serious na Challenge Cup kama Express ya Uganda wana utimamu wa mwili / physical fitness pamoja na utimamu wa bongo (mental preparedness) kwa ajili ya michuano mikubwa kama ya CAF Champion League 2021 na Confederation League Cup ya 2021.

Yanga inapenda sana kukacha michuano ya kikanda kwa kutopeleka timu au wachezaji wanaowatumainia na matokeo yake tunayaona Leo 12 September 2021. Azam FC , Biashara FC wameanza na mguu mzuri michuano ya Afrika 2021.
 
Ogopa Matapeli kuna Yanga tatu...Ile ya kwenye Mwanaspoti, Ile inayosimuliwa na Manara afu kuna hii Yanga yenyewe iliyofungwa mechi mbili mtawalia
Yanga ya kwenye Mwanaspoti kama una roho nyepesi unaweza dhani inafanana na Bayern Munich ya Ujerumani.
Yanga ya Maulid Kitenge, kama hujui Yanga unaweza kuifananisha na Barcelona.
Lakini ukija kuiona hiyo Yanga yenyewe sasa, hata Namungo ya Ruangwa ina nafuu
 
Huyu Duma ana ushemeji na Injinia Hersi nini?? Anapataje namba Yanga😂
Duma ni mkali akicheza kwenye timu za kawaida kama Mbeya City, Mwadui, Njombe Mji, Polisi Tanzania, nk. Ukimpeleka Azam au Yanga, anakimbia kimbia na kuruka ruka tu uwanjani!

Binafsi ameniangusha sana! Maana na mimi ni mmoja wa mashabiki wake alipokua Polisi Tanzania. Nashangaa benchi la ufundi lilimuacha vipi mchezaji kiraka kama Makapu na kumbakiza Nchimbi mzee wa kupuyanga uwanjani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…