Inajenga wala hainunui timu. Kwanini nimesema anajenga? Ni kwasababu kuna maingizo ya wachezaji wapya wengi zaidi ya watano, hawa wachezaji wapya na wa zamani waliosalia kwenye kikosi wamekaa pamoja kwa muda mfupi sana mpaka sasa hivyo bado hakuna maelewano baina ya wachezaji wapya na wa zamani hivyo hakuna muunganiko wa moja kwa moja baina yao. Kwenye mpira kuna kitu kinaitwa mfumo. Kocha anajua naingia na mfumo fulani ambao unaongozwa na mchezaji fulani. Huu mfumo ukigoma na switch mfumo mwingine kwa kumtoa fulani na kumeingiza fulani ili asaidiane na fulani na fulani asogee sehemu fulani.
Makocha wanatengeneza mifumo zaidi miwili kulingana na wachezaji walionao na utengeneze mifumo ni lazima umjue sifa na tabia za kila mchezaji ili ujue nani na nani wanaweza kutengeneza partnership. Msimu uliopita Yanga ilivyokuwa chini ya Kaze mwanzoni uliona hakukuwa na watu walielewana pamoja kwenye ushambuliaji lakini siku zilivyozidi kwenda kukatengeneza partnership kati ya Kaseke na Yacouba. Ndivyo mpira ulivyo ni lazima kuwe na muunganiko unaanzia kwenye wakabaji, viungo mpaka washambuliaji.