Yanga wameanza kuonyesha matumaini

Yanga wameanza kuonyesha matumaini

Yanga imeanza kurudi hii inatia moyo sana, wachezaji wameanza kurudisha ile tabia yao ya kufanya msako wa ushindi kipindi cha pili, safi sana. Washikilie bomba hapo hapo mechi zijazo msako uwe mkali zaidi kasi iongezeke, Yanga ni timu kubwa Africa kuifunga ni kuidhalilisha.

1. Subs zimetusaidia kwa kufanyika mapema big up sana Ramovich
2. Kukaba kitimu na kwa kasi kama zamani bado haijarudi
3. Kutoa pasi kwa haraka bado
4. Kupeleka mashambulizi ya kasi kama zamani bado haijarudi
5. Kutoa vyumba kwa haraka bado. Anao anao imezidi na inagharimu timu
6. Wachezaji kupenda kurudisha Mpira nyuma bado ni Tatizo
6. Wachezaji kutoa pasi mkaa bado ni Tatizo
7. Kuweza kupasua ngome kupitia katikati kwa pasi mpenyezo ndo imekufa kabisa
8. Wachezaji kuchoka baada ya dkk 45 bado ipo ila kocha kashawashtukia wanaochoka anawatoa haraka bila kujali jina, hii tayari big up sana Ramovich.
9. Viungo kupokea mipira kutokea nyuma kwa haraka na kuipeleka mbele kwa washambuliaji kwa haraka bado ni tatizo kubwa sana. Mabeki wanapasiana tu hakuna viungo wanaokuja kuchukua mipira, hii Imekufa kabisa.
10. Kocha kuanza kuielewa timu, kupanga kikosi kizuri na kufanya subs vizuri kwa Wakati sahihi hii imeanza tayari mdogo mdogo. Hongera sana Ramovich.


Yanga bingwa!
 
Mc alger akishinda game yake leo matumaini yanazidi kufifia
 
Mc alger akishinda game yake leo matumaini yanazidi kufifia
Hata akishinda yeyote yule au hata watoke sara lakini kinachotakiwa kwa Yanga ni kushinda mechi zake zote tatu zilizobakia.
 
Ili Yanga iwe na uhakika wa kufuzu na asiwe omba omba wa kutaka matokeo ya wenzake yawe vipi ni lazima ashinde mechi zake zote tatu zilizobakia. Tarehe. 3 anacheza taifa dhidi ya Mazembe na tarehe 10 ni dhidi ya Al Hilal. Hizo mechi mbili zinazofuata ni lazima ashinde kwanza.
Hizo zilizobaki,uhakika wa kufunga na kushinda zote upo.Leo morali ya timu imeamka baada ya pointi moja.
 
Leo mlikatika viuno mpaka dakika ya mwisho ndio mkapata kikombe cha uji kutoka kwa Mazembe
Sasa nyie mbumbumbu, mpo huko dampo mtaelewa Nini kuhusu mambo ya club bingwa
Hujui mechi za ugenini zinachezwaje upo Kwa akina mama
 
Sasa nyie mbumbumbu, mpo huko dampo mtaelewa Nini kuhusu mambo ya club bingwa
Hujui mechi za ugenini zinachezwaje upo Kwa akina mama
Nenda huko wewe...simba imeshashiriki hyo club Bingwa back to back 4 good yrs...zezeta wa head...chura kiziwi wew...
 
Haichukui nafasi ya daktari lakini kusema ukweli Yanga wameanza kuonyesha matumaini. Huenda wakaingia robo fainali kwa kushinda mechi zote 3 zilizo baki huku ikitegemea na matokeo ya mechi nyingine.

Mechi ijayo ya Yanga na Mazembe kwa Mkapa uwanja utajaa sana mashabiki kwenda kuipa sapoti timu yao. Tuombe usiku leo Ibenge Fc washinde pamoja na mechi ya marudiano
mambo ya kupiga ramli hatutaki,wao washinde tu mechi zote.
 
Back
Top Bottom