Yanga wameanza kuonyesha matumaini

Yanga imeanza kurudi hii inatia moyo sana, wachezaji wameanza kurudisha ile tabia yao ya kufanya msako wa ushindi kipindi cha pili, safi sana. Washikilie bomba hapo hapo mechi zijazo msako uwe mkali zaidi kasi iongezeke, Yanga ni timu kubwa Africa kuifunga ni kuidhalilisha.

1. Subs zimetusaidia kwa kufanyika mapema big up sana Ramovich
2. Kukaba kitimu na kwa kasi kama zamani bado haijarudi
3. Kutoa pasi kwa haraka bado
4. Kupeleka mashambulizi ya kasi kama zamani bado haijarudi
5. Kutoa vyumba kwa haraka bado. Anao anao imezidi na inagharimu timu
6. Wachezaji kupenda kurudisha Mpira nyuma bado ni Tatizo
6. Wachezaji kutoa pasi mkaa bado ni Tatizo
7. Kuweza kupasua ngome kupitia katikati kwa pasi mpenyezo ndo imekufa kabisa
8. Wachezaji kuchoka baada ya dkk 45 bado ipo ila kocha kashawashtukia wanaochoka anawatoa haraka bila kujali jina, hii tayari big up sana Ramovich.
9. Viungo kupokea mipira kutokea nyuma kwa haraka na kuipeleka mbele kwa washambuliaji kwa haraka bado ni tatizo kubwa sana. Mabeki wanapasiana tu hakuna viungo wanaokuja kuchukua mipira, hii Imekufa kabisa.
10. Kocha kuanza kuielewa timu, kupanga kikosi kizuri na kufanya subs vizuri kwa Wakati sahihi hii imeanza tayari mdogo mdogo. Hongera sana Ramovich.


Yanga bingwa!
 
Mc alger akishinda game yake leo matumaini yanazidi kufifia
 
Mc alger akishinda game yake leo matumaini yanazidi kufifia
Hata akishinda yeyote yule au hata watoke sara lakini kinachotakiwa kwa Yanga ni kushinda mechi zake zote tatu zilizobakia.
 
Hizo zilizobaki,uhakika wa kufunga na kushinda zote upo.Leo morali ya timu imeamka baada ya pointi moja.
 
Leo mlikatika viuno mpaka dakika ya mwisho ndio mkapata kikombe cha uji kutoka kwa Mazembe
Sasa nyie mbumbumbu, mpo huko dampo mtaelewa Nini kuhusu mambo ya club bingwa
Hujui mechi za ugenini zinachezwaje upo Kwa akina mama
 
Sasa nyie mbumbumbu, mpo huko dampo mtaelewa Nini kuhusu mambo ya club bingwa
Hujui mechi za ugenini zinachezwaje upo Kwa akina mama
Mlijua hayo baada ya miaka 25 ninyi robo hamuendi labda mpate robo ya unga wa uji
 
Sasa nyie mbumbumbu, mpo huko dampo mtaelewa Nini kuhusu mambo ya club bingwa
Hujui mechi za ugenini zinachezwaje upo Kwa akina mama
Nenda huko wewe...simba imeshashiriki hyo club Bingwa back to back 4 good yrs...zezeta wa head...chura kiziwi wew...
 
mambo ya kupiga ramli hatutaki,wao washinde tu mechi zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…