Yanga yaihitimisha mzunguko wa kwanza kwa kuisambaratisha Ruvu Shooting magoli 2 kwa 1

Yanga yaihitimisha mzunguko wa kwanza kwa kuisambaratisha Ruvu Shooting magoli 2 kwa 1

Casuist

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2014
Posts
1,189
Reaction score
2,970
Ligi kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa klabu ya Yanga kuwakaribisha maafande wa Ruvu JKT uwanja wa Uhuru. Mechi hii itaashiria kufungwa rasmi mzunguko wa kwanza, mechi hii ni muhimu kwa klabu ya Yanga ili kupunguza zaidi tofauti ya alama na kinara wa ligi, Simba baada ya kuonja vipigo viwili mfululizo.

Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojiri shamba la bibi.

=====
FULL TIME: Yanga wanaondoka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 na kufikisha pointi 33.

Dakika ya 90 + 4: Muda wowote mchezo unaweza kumalizika.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.

Dakika ya 89: Yanga wanamiliki mpira muda mwingi.

Dakika ya 88: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Ngoma anaingoa Matheo.

Dakika ya 87: Said Dilunga anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo.

Dakika ya 75: Yondani anazungumza na refa akilalamika kilichotokea kuwa Dante alifanyiwa faulo.

Dakika ya 74: Ruvu wanafanya shambulizi lakini kipa wa Yanga, Kakolanya anaudaka. Wakati huo Dante yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kuumia wakati akiwania mpira.

Dakika ya 68: Tambwe anatupia mpira wavuni lakini mwamuzi anapuliza kipenga kuwa ameotea.

Dakika ya 58: Yanga wanaongoza ambao 2-1.

Dakika ya 52: Yanga wanapata bao la pili mfungaji akiwa ni Niyonzima. Kazi nzuri iliyofanya na Ngoma ambaye aliubabatiza mpira kisha akampa pasi Niyonzima akapiga shuti na kujaa wavuni.

Dakika ya 50: Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesimama anatoa maelekezo baada ya bosi wake Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm kupelekwa kwenye benchi na mwamuzi kutokana na kupishana kauli.

Dakika ya 48: Chirwa anapata nafasi, anapiga shuti lakini linapaa juu ya lango la Ruvu.

Dakika ya 46: Kipindi cha pili kimeanza.

=========
HALF TIME
45+8' Muamuzi anapuliza kipyenga kuashiria mpira unaenda mapumziko.
38' AbdulRahman Mussa yuko chini baada ya kupigwa kiatu, matokeo bado 1-1
31' Goooal: Simon Msuva anaisawazishia Yanga, Yanga 1-1 Ruvu Shooting
30' Tambwe anajaribu kuingia na mpira eneo la hatari la Ruvu lakini beki anambania.
20' Lango la Ruvu linashambuliwa kama nyuki na wanaonekana kuutafuta mpira kwa tochi.
18' Chirwa anajaribu kufumua shuti kali lakini kipa wa Ruvu anafanikiwa kuupangua.
12' Jabir Azizi anapiga mpira mzuri wa adhabu ndogo lakini unakua chakula chepesi kwa kipa ya Yanga.
11' Chande Magoja ameenda chini baada ya kuchezewa mchezo mbaya na beki wa Yanga
11' Obrey Chirwa amepaisha juuu baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Niyonzima
07' Abrahaman Mussa amefikisha bao la tatu kwenye ligi kuu baada kuachia shuti kali na kuipa uongozi Ruvu shooting.
07' Goooal, Ruvu shooting wanaweka goli la kwanza: Yanga 0-1 Ruvu shooting
03' Ruvu shooting wanajaribu kufika langoni mwa Yanga lakini wanashindwa kupanga hesabu zao vizuri
01' Muamuzi kapuliza kipyenga kuashiria mwanzo wa mchezo
 
wakimataifa leo tunapiga mtu kama kawa...taarifa zisizo rasmi toka mbeya ni kwamba mnyama bado yupo gerezani,maafande wa mbeya c watu wa mchezo mchezo hata kdg
 
Ligi kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa klabu ya Yanga kuwakaribisha maafande wa Ruvu JKT uwanja wa Uhuru. Mechi hii itaashiria kufungwa rasmi mzunguko wa kwanza, mechi hii ni muhimu kwa klabu ya Yanga ili kupunguza zaidi tofauti ya alama na kinara wa ligi, Simba baada ya kuonja vipigo viwili mfululizo.

Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojiri shamba la bibi.
=====

12' Jabir Azizi anapiga mpira mzuri wa adhabu ndogo lakini unakua chakula chepesi kwa kipa ya Yanga.
11' Chande Magoja ameenda chini baada ya kuchezewa mchezo mbaya na beki wa Yanga
11' Obrey Chirwa amepaisha juuu baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Niyonzima
07' Abrahaman Mussa amefikisha bao la tatu kwenye ligi kuu baada kuachia shuti kali na kuipa uongozi Ruvu shooting.
07' Goooal, Ruvu shooting wanaweka goli la kwanza: Yanga 0-1 Ruvu shooting
03' Ruvu shooting wanajaribu kufika langoni mwa Yanga lakini wanashindwa kupanga hesabu zao vizuri
01' Muamuzi kapuliza kipyenga kuashiria mwanzo wa mchezo
 
Kama nawaona wa matopeni hadi muda huu roho zao kwatu.
Dakika 90 tutajua mbivu na mbichi. Yanga lazima ashinde
 
Back
Top Bottom