SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Wakati timu zitakazoshiriki duru la kwanza la mashindano mapya ya CAF linajulikana, na zimechaguliwa kutokana na ubora wake wa miaka ya hivi karibuni, katika hali ya kushangaza, timu ya Yanga kupitia kwa serikali imewapigia magoti CAF kuomba ipewe nafasi pia ya kushiriki mashindano hayo.
Wajuvi wa mambo tukishawahi kuonya kuwa wanasiasa wanaweza kutumika ili kushawishi au kushurutisha Yanga nayo ipewe nafasi katika mashindano hayo.
Ikumbukwe kuwa katika miaka 10 ya mashindano ya CAF CUP ambayo Simba walicheza hadi fainali mwaka 1993, Yanga hawakuwahi kuvuka hatua ya kwanza. Pia ni miaka 25 sasa imepita toka Yanga waingie hatua ya Robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika wakati Simba wamefanya hivyo mara 3 ndani ya miaka hii 5 iliyopita.
Wanasiasa waache kuingilia masuala ya mpira. Hii ni moja ya sababu tunapata mikwamo kila siku katika mpira wetu.