Yanga yakubali kichapo cha kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara

Yanga yakubali kichapo cha kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara

TANGAZO KWA MASHABIKI WA UTO

ninauza dawa yakuhama yanga, ukiitumia ndani ya 24hrs utajikuta mwanasimba na maisha ya furaha yataendelea.
Hatuhami YANGA... tumeipenda wenyewe
 
Sirikali ifike pahala iwaongezee ulinzi coastal aisee wamejua kunifurahisha mamaeee
Screenshot_20210304-180349.jpg
 
Amesukumwa beki wa Coastal akaanguka ni faulo ya wazi na bado mpira umedunda ameushika Kisinda, refa ameacha tu, wangekuwa wao kesho Press Conference.

Mwamuzi ameamua kuwapa bao Uto
Kabisaa mkuu huo ndio ukweli hili sio goli sio goli kabisaa.

Mbeleko imechanika hii, sasa sijui watasingizia nini leo mana na penalt wamepewa.

Haya tambo za unbeaten zimekwisha rasmi nchi itakuwa na amani sasa
 
Baada ya mzunguko wa kwanza Yanga kuifunga Coastal union bao 3-0, leo Coastal Union wamesema wanachezea heshima kwa uwanja wake wa nyumbani na kocha Mgunda amejigamba atakuwa wa kwanza kuifunga Yanga msimu huu.

Yanga inahitaji matokeo kuendelea kujiweka vizuri kileleni lakini uwanja wa Mkwakwani umekuwa haumpi matokeo ya uhakika kwenye misimu ya karibuni.

Kuwa nami kukujuza yatakayojiri uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

=======

Mechi zilizochezwa mapema leo

FT' Polisi Tanzania 1-0 KMC | Sheikh Amri Abeid

FT' Mtibwa Sugar 0-0 Biashara UTD | Jamhuri

FT' Tanzania Prisons 1-1 Mbeya City FC

=======

00' Mwamuzi anapuliza kipenga kuashiria mwanzo wa mcho na Coastal wanaanza kusukuma guzi

06' Yanga inapata penati baada ya Kipemba wa Coastal kumuweka chini mchezaji wa Yanga

08' Tuisila Kisinda anashindwa kufunga penati, mlinda mlango wa Coastal anasimama imara na kuidaka penalt.

10' Coastal wanaweka bao la kwanza baada ya Erick Msagati kupiga shuti mpira uliokuwa unaamba goli la Yanga ulioanzia mpira wa adhabu ndogo

19' Feisal Salum anajaribu shuti la kushtukiza lakini mlinda mlango wa Coastal alikuwa yuko makini na kuuondoa kwenye hatari

32' Yaqub anaingia kuchukua nafasi ya Sarpong kwa upande wa Yanga

37' Tuisila Kisinda anasawazisha, Coastal Union 1-1 Yanga

40' Farid Mussa anashindwa kuongeza bao la pili kwa Yanga baada ya kubaki na mlinda mlango

45' Mpira unaenda mapumziko

46' Mpira umesharejea kutoka mapumziko, Coastal 1-1 Yanga

53' Deus Kaseke anajaribu kupiga shuti lakini mpira unapaa juu ya lango la Coastal Union

64' Mfungaji wa Goli la Coastal, Erick Msagati anakwenda bench na nafasi yake kuchukuliwa na Issa Abusheikh

72' Omari Majimengi najaribu kuitanguliza Coastal kwa mkwaju mkali lakini mlinda mlango wa Yanga anasimama imara

83' Mudathir Abdallah anaweka goli la pili kwa shuti kali lililopita na wavu na kuipa uongozi Coastal Union

90' Dakika tano zinaongezwa kumaliza mtanange

90+5' Coastal Union inatamba uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Yanga magoli 2-1.

Yanga inashindwa kutamba uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Coastal union kwa mwaka wa sita mfululizo na inapoteza mechi yake ya kwanza ligi kuu Bara, majaliwa ya Yanga kubaki kileleni ni kuchacha kwa viporo vya Simba
Kusema ukweli mie kwa Yanga huwa sioni futiboli zaidi ya mbio tu.
 
Back
Top Bottom