Yanga yamfuta kazi Kocha Mkuu Pedro Gonçalves

Yanga yamfuta kazi Kocha Mkuu Pedro Gonçalves

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978

Young Africans Sports Club (Yanga) imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha mkuu wa kikosi cha kwanza, Pedro Gonçalves.​

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Mei 6, 2026, uongozi wa klabu hiyo umeeleza umechukua uamuzi huo kama sehemu ya mabadiliko ndani ya timu, bila kueleza sababu za kina zilizopelekea hatua hiyo.

Yanga imemshukuru Gonçalves kwa mchango wake alioutoa katika kipindi chote alichokuwepo klabuni hapo, na sasa kikosi hicho kitasimamiwa kwa muda na makocha wasaidizi, Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi, hadi mwisho wa msimu.

Soma Pia: Yanga kumtambulisha coach Pedro Valdemour Soares, muda wowote

Hatua hiyo inakuja katika kipindi ambacho klabu hiyo inaendelea na mashindano ya ndani.

YANGA.jpg
 
Kulikuwa hakuna namna. Kimsingi alishindwa kuwatumia wachezaji aliowakuta, na wale aliowasajili mwenyewe kwenye dirisha dogo. Timu ilikuwa inapandisha presha mpaka mpaka basi.

Nashauri mwishoni mwa msimu huu ufanyike usajili makini. Mpaka sasa ni wachezaji wasiozidi 6 pekee wa kigeni ndiyo wanasifa ya kubakia. Waliobakia wanatakiwa kupewa mkono wa kwa heri ili kuwapisha wachezaji wengine bora zaidi. Ukija kwa wazawa na kwenyewe ni hivyo hivyo. Kuna wachezaji wanakula tu mishahara, huku wakikosa nafasi ya kucheza kwa sehemu kubwa ndani ya msimu.
 
Back
Top Bottom