Kulikuwa hakuna namna. Kimsingi alishindwa kuwatumia wachezaji aliowakuta, na wale aliowasajili mwenyewe kwenye dirisha dogo. Timu ilikuwa inapandisha presha mpaka mpaka basi.
Nashauri mwishoni mwa msimu huu ufanyike usajili makini. Mpaka sasa ni wachezaji wasiozidi 6 pekee wa kigeni ndiyo wanasifa ya kubakia. Waliobakia wanatakiwa kupewa mkono wa kwa heri ili kuwapisha wachezaji wengine bora zaidi. Ukija kwa wazawa na kwenyewe ni hivyo hivyo. Kuna wachezaji wanakula tu mishahara, huku wakikosa nafasi ya kucheza kwa sehemu kubwa ndani ya msimu.