Yanga yamtaka Fei Toto arudi klabuni haraka na pia klabu ipo tayari kumuuza

Msingi wa barua upo hapa wasijifanye kuvimba wanamuhitaji sana huyu dogo mengine ni umbea tu.

"Aidha, Klabu ya Yanga iko tayari kumpokea Feisal Salum na kumjumuisha kwenye kikosi, na kwa kuzingatia sera na utaratibu wa Klabu ya Yanga katika kuwaongezea mikataba wachezai wake wanaofanya vizuri, Uongozi wa Yanga uko tayari kuendelea na mazungumzo na Feisal Salum Abdallah na wawakilishi wake juu ya kuboresha mkataba wake, kama wataridhia"🤣
 
Sasa wewe umekua nani unawapangia TFF mda wa kutoa adhabu. umejuaje kwamba hataadhibiwa?
Kwasababu adhabu ni pamoja na mkataba kuvunjika na sio kurudishwa tena kwenye Club

Yani mchezaji aliyevunja mkataba bila kufuata utaratibu atahesabiwa kuwa mkataba umevunjwa ila amekiuka sheria

Hivyo adhabu ni kulipishwa faini pamoja na kufungiwa

Sasa Feisal ndio kwanza tunaona na barua ya wito kutoka kwa Club ikimtaka Feisal arejee kambini

Sheria hiyo haipo
 
Poor, kwanini asiende juu zaidi kama ana uhakika yupo sahihi Kwa alichokifanya??
 
Wapo tayari kuboresha maslahi yake. Mpira umerudi kwa Fei, kama ishu ni maslahi anaboreshewa pamoja na yote yaliyotokea.

Fei anachotaka mpaka sasa ni mkataba uvunjike na hakuna timu iliyosema inamtaka.
Anaweza kua free agent, sio lazima timu imtake mkataba kuvunjika.
 
Reactions: Tsh
Poor, kwanini asiende juu zaidi kama ana uhakika yupo sahihi Kwa alichokifanya??
Gharama ni kubwa,vile vile inachukua muda pia kwa hiyo kabla ya kwenda lazima haakikishe option zote za chini amemaliza.
 
Halafu kuna watu bado watasema Yanga inamng'ang'ania huyo mchezaji! Tamko limejitosheleza kabisa.
 
Wamechelewa kufanya haya maamuzi, hawatafanikiwa kumuuza fei, fei atavunja mkataba wataishia kupata fidia ambayo ni kidogo kuliko matarajio yao.
 
Hataki kuboresha hayo maslahi
 
Waache waendelee kumlazimisha kurudi kambini. Atarudi halafu ataenda kukojolea sufuria la maharagwe. Famasihara nini.
 
Yanga imeonyesha udhaifu mkubwa sana kumng'ang'ania fei.
 
Kwahiyo ulitaka achukuliwe hatua katika lipi sasa
Nimesema "Hazijatoa maamuzi kwenye barua aliyoiwasilisha leo kuhusu kuvunja mkataba"

Sijui unaelewa nilichokiandika hapo?
 
Ngazi za chini tayari sasa zishatoa maamuzi ambayo inaonekana hajatidhika nayo kwanini sasa asiende huko?
Mimi nakwambiaga sana una kichwa kigumu. Scars Amesema tena na tena kuwa suala lililokuwa TFF na maamuzi yaliyofanyiwa review jana yalikuwa ni kumtambua Feisal kama mchezaji wa Yanga. TFF wameepuka kutoa maelezo in public kwa nini wameamua hivyo kwa sababu ni wazi ingegusia uamuzi wa Feisal kurudisha zile pesa.

Sasa Feisal anaona ok, yoyote yaliyopita fresh tu kama nilikosea poa ila sasa anawarudia TFF kuwaambia anavunja mkataba. Tunarudi kulekule kwamba sasa Yanga na Feisal watakaa chini huku TFF akiwa msuluhishi ili kuvunja mkataba huo kwa jinsi mkataba unavyosema inatakiwa kufanyika. Hapa Feisal ni dhahiri harudi nyuma, piga ua.
 
Baada ya hapo anakuja kuuliza tena "Kwahiyo ulitaka achukuliwe hatua katika lipi sasa"

Huyu mtu sijui kama anaelewa nachomuandikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…