Tetesi: Yanick Bangala muda wowote anatua Msimbazi

Tetesi: Yanick Bangala muda wowote anatua Msimbazi

Soloma TV Online

Senior Member
Joined
Jun 26, 2023
Posts
104
Reaction score
291
Soka la Bongo lina mvuto wake, unaambiwa kuwa wakati Timu ya Yanga ikitarajia kufunga usajili wake kwa kumleta Straika la magoli upande wa pili Timu ya Simba wanajiandaa kupeleka simanzi Jangwani kwa kumleta Mkongo aliyefanya vizuri na Wananchi hao ikiwa ni jibu la kubebwa kwa Mkude kuwafuta machozi mashabiki.

Tetesi zinasema Mwamba kagoma kupelekwa kwa mkopo Singida Fountaingate anachotaka yeye ni kuvunjwa kwa Mkataba tu.
 
Sioni tatizo kama Simba watampa hela ndefu anayotaka ambayo Yanga waliona haikustahili!

Mashindano ya usajiri kama haya husababisha pia wachezaji kujituma zaidi na kutupa burudani tunayotaka. Akitemwa na na timu moja basi anapoenda timu nyingine anajitahidi kuonyesha timu aliyoachwa kuwa bado yeye ni zaidi. Ntibazonkiza ni mfano mmoja ingawa sasa amefikia saa 12 jioni.
 
Soka la Bongo lina mvuto wake, unaambiwa kuwa wakati Timu ya Yanga ikitarajia kufunga usajili wake kwa kumleta Straika la magoli upande wa pili Timu ya Simba wanajiandaa kupeleka simanzi Jangwani kwa kumleta Mkongo aliyefanya vizuri na Wananchi hao ikiwa ni jibu la kubebwa kwa Mkude kuwafuta machozi mashabiki. Tetesi zinasema Mwamba kagoma kupelekwa kwa mkopo Singida Fountaingate anachotaka yeye ni kuvunjwa kwa Mkataba tu. View attachment 2697395
Chukueni wote, Bangala, Juma Shabani, Doumbia na Kisinda. No problem Yanga inasonga mbele.
 
Piga hesabu ya wachezaji wa kigeni Simba halafu sema nani aondoke ili Bangala aingie
Kama hizi ndo akili za Viongozi wa vilabu basi kumbe yeyote anaweza kuongoza Simba na Yanga. Simba Kwa Sasa wanajitahidi angalau Sakho na Banda waondoke hata Kwa mkopo ili kupata nafasi za LUIS 2. Halafu kumbe Muda huo huo kuna kiongozi anamfikiria Yanick Bangala?
Haya Mchambuzi tuambie anatoka Nani kumpisha mchezaji wa Mkomoano?
 
Hii habari Haina ukweli.

VIONGOZI wengi wa mpira HAWAJUI mpira.

Nimewashauri sana Baadhi ya VIONGOZI kuhusu.
Hatari ya kuwa na Mabeki wawili tu wenye UWEZO,

Nimewaomba sana wamuongeze Bangala kama kiungo mkabaji na Beki.

SIMBA INGEMPATA BANGALA INGECHEZA FAINALI CAFCL.
 
Si maslahi wala kushuka kwa kiwango,bangala anaachwa Yanga sababu zake ni sawa sawa na chama kwa makolo,alichokua anafanya bangala ndicho anachofanya chama na viongozi wa simba wanajua ila wanaogopa kuchukua maamuzi sbb huko koloni mchezaji yuko juu zaidi ya klabu Yanga kama iliweza kufukuza timu nzima ndio ishindwe kwa mchezaji snitch m1
 
Soka la Bongo lina mvuto wake, unaambiwa kuwa wakati Timu ya Yanga ikitarajia kufunga usajili wake kwa kumleta Straika la magoli upande wa pili Timu ya Simba wanajiandaa kupeleka simanzi Jangwani kwa kumleta Mkongo aliyefanya vizuri na Wananchi hao ikiwa ni jibu la kubebwa kwa Mkude kuwafuta machozi mashabiki.

Tetesi zinasema Mwamba kagoma kupelekwa kwa mkopo Singida Fountaingate anachotaka yeye ni kuvunjwa kwa Mkataba tu.

View attachment 2697395
Uyo bangala wanamsajiri kwenda kuchukua nafasi ya nani pale simba?
Washakamilisha idadi na ikapitiliza mpaka wawatoe banda na sakho ndio wabaki 12, labda akacheze michuano ya kimataifa na sio ligi ya ndani
 
Siku hizi JF imekuwa hovyo sana. Ipo wazi sana kuwa Simba haiwezi kumsajili Bangala kwa sasa. Idadi ya wachezaji wa kigeni imeshatimia na Simba imeshaongeza viungo wawili wakabaji mmoja wa kigeni na mmoja wa ndani watakaosaidiana na waliopo. Isitoshe kwa nafasi ya beki wa kati wameshaongeza wachezaji wawili mmoja wa kigeni na mwingine wa ndani. Ili Simba imsajili Bangala maana yake kati ya Phiri au Saidoo mmoja atemwe kitu amabacho si rahisi kiasi hicho.
 
Wachezaji wa kigeni.

1. Jefferson Luis goal keeper.
2. Ngoma
3. Kramo
4. Malone
5. Onana.
6. MIQUESSON.

7. Inonga
8. Kanute
9. Saido.
10. Baleke.
11 Chama.

( 12. Phili. )

...............................................
13. SACKHO.
14 . Banda .

WANGEKUWA NA AKILI WANGEMTOA KAFALA PHILI AJE BANGALA.
au phili ashiriki mashindano ya kimataifa tu.
 
Simba ilikuwa wampate Bangala Tangu Mwaka 2019.

Kulikuwa na tofauti na sintofahamu Baina ya uongozi na Bangala.

Sven akiwa KOCHA wa FAR RABAT.
ALIWAUNGANISHA SIMBA KUMSAJILI Bangala.

Ila ALIWAONYA kuwa Mchezaji mzuri mno ila anamatatizo ya kinidhamu.
 
Piga hesabu ya wachezaji wa kigeni Simba halafu sema nani aondoke ili Bangala aingie
Aondoke yule mchezaji wa kung fu na kinara wa yellow card-sadio kanute. Mwingine wa kupewa Thank you ni mcheza mayenu-Henock Inonga
 
Soka la Bongo lina mvuto wake, unaambiwa kuwa wakati Timu ya Yanga ikitarajia kufunga usajili wake kwa kumleta Straika la magoli upande wa pili Timu ya Simba wanajiandaa kupeleka simanzi Jangwani kwa kumleta Mkongo aliyefanya vizuri na Wananchi hao ikiwa ni jibu la kubebwa kwa Mkude kuwafuta machozi mashabiki.

Tetesi zinasema Mwamba kagoma kupelekwa kwa mkopo Singida Fountaingate anachotaka yeye ni kuvunjwa kwa Mkataba tu.

View attachment 2697395
Yy ndiye anaye vunja mkataba, so Yanga wanachotaka ni hela yao ya kuvunja mkataba, kama mnayo njooni tuongee biashara.
 
Back
Top Bottom